Gia ya angani, kadi # 1, na kauli mbiu ya “ulipo tupo” ni matokeo ya siasa za ufuasi

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Salaam wanabodi;
Nilichojifunza hadi sasa ni kwamba siasa za Tanzania hazina misingi ya kiitikadi bali zinaendeshwa kwa HASIRA na VISASI vya “wanasiasa wakubwa” ambao wanajaribu kuonesha nguvu zao (wafuasi wao) dhidi ya “mfumo” fulani uliowatenga au waliojitenga nao. Kwa maneno mengine, vyama vya siasa, hasa vya upinzani vinatumika kama majukwaa na wanasiasa wanaojitenga au kutengwa kuonesha nguvu zao au ushawishi walionao dhidi ya hiyo mifumo.

Kwa bahati nzuri au mbaya, wanasiasa wakubwa wote wanasifa zinazofanana. Moja ya sifa zao ni kwamba walishawahi kushika nafasi za juu za uongozi serikalini au kwenye vyama hasa CCM. Hivyo basi kutokana na nafasi za uongozi walizopitia, walipata nafasi nzuri ya kujenga ushawishi na kujitengenezea wafuasi. Sifa ya pili ni kwamba wanasiasa hao, kutokana na hulka zao za kupaparikia urais walikuwa wanatumia mbinu chafu (ukabila, udini, undugu au ukanda) dhidi ya washindani wao wa ndani ambazo hazikubaliki kwa misingi ya vyama vyao hadi wakaishia kujitenga au kutengwa na vyama vyao halisi. Sifa yao nyingine muhimu wanasiasa wakubwa ni kwamba wamekuwa na ndoto ya kushika nafasi ya urais katika nchi hii na hii ndio maana halisi ya kujijengea kwao wafuasi.

Wanasiasa hao hawakati tamaa. Bali wanapokosa fursa ya kugombea urais kupitia majukwaa yao ya asili (vyama) hutafuta majukwaa mengine ili watimize ndoto zao. Wanasiasa hao wakubwa wanapojiunga na vyama vingine, wale wafuasi wao wanakuwa hawana namna bali ili wasibaki wapweke huamua kumfuata “mtu wao” na huu ndo msingi wa kauli mbiu “ULIPO TUPO”. Kwa bahati mbaya sana vyama vya siasa vimebaki kutegemea nguvu za wanasiasa wakubwa wanaohamahama na kwahiyo wenyeji wa vyama hivyo wako tayari KUBADILI GIA ANGANI, KUTOA KADI No. 1 au kusema “KARIBU NYUMBANI” kwa wanasiasa wakubwa wanaohamia.

Matokeo yake kwavile wanaingiza makundi makubwa ya wafuasi wao “ugenini” wanasiasa hao nao hawako tayari kuwa chini ya wenyeji waliowakuta, bali wanajiona kuwa ni wanachama wenye hisa kubwa na hivyo wanataka wabaki kuwa “top and influential” dhidi ya wenyeji wao. Kubadili gia angani, kutoa kadi # 1 na kauli mbiu ya “ulipo tupo” na ile ya “karibu nyumabani” maana yake ni wenyeji kukubali kuacha itikadi na misingi ya vyama vyao na kuwa tayari kuwatukuza na kuendeshwa na utashi wa wageni wao ambao msingi wake ni HASIRA na VISASI dhidi ya mifumo walioihama. Kwakuwa mbali na jina, utambulisho muhimu wa chama cha siasa ni itikadi ambayo ndo msingi wa sera za chama husika, chama kinapobadili gia angani ili kiendane na “hisia” za wageni hupoteza utambulisho wake ambao ndo msingi wa umaarufu wake.

Kwahiyo siku hizi viongozi wa siasa wenye utashi wa kuendeleza kwa kujenga itikadi za vyama vyao kwa wanchi ni wachache sana. Viongozi tulionao ni “opportunistic” kwa maana uwezo wao ni kutumia fursa za kuwapokea wanasiasa wenye hasira na waliojitenga dhidi ya vyama vyao vya asili. Zaidi, tunachokiona ni kutamalaki kwa USALITI (kujivua uwanachama) miongoni mwa makada wa vyama. Hii maana yake ni kwamba wanachama wako “too loose” kwa maana hawajajengeka KIITIKADI bali KIUFUASI wa wanasiasa wakubwa.

Kwa bahati mbaya sana wanasiasa hawajui kwamba mtindo huu wa siasa unadhihirisha rangi zao za asili kwamba hawako pale kutetea wananchi na kuwaletea mabadiliko bali kutafuta maslahi yao binafsi. Bali siasa hizi zinasababisha wanasiasa wanaohamahama kupwaya na kupoteza mvuto kwa sababu wanawangeusha wananchi kutokana na misimamo yao inayobadilika kila msimu. Matokeo yake wananchi (wenye akili) wanahisi hakuna mwanasiasa “mwenye jipya” na ndio maana idadi ya wapiga kura katika chaguzi zinaendelea kushuka.

Hata hivyo ni matumaini yangu kwamba mtindo huu wa siasa utafutika baada ya kizazi cha "wanasiasaa wakubwa" waliojijengea wafuasi kwisha.
 
Ukimaliza hii mada yako ndefu tueleze na wale wanaopata madaraka kwa kutumia vyombo vya dola na udhaifu wa tume ya uchaguzi.

Kwani mada yangu inaongelea watu gani?
 
Hivi bado unateseka ...Alipokuja Mkapa mlituaminisha ndie mtakatifu kuliko wote waliopita tukakubali maana alijisifu ni mkweli na muwazi tukaitikia hewalla ...kaja Kikwete na Ari mpya nguvu mpya ...baadae akaongeza na kasi zaidi tukakubali ...kaja Magufuli mkamtaja Kama Masihi alieahidiwa ...akatuambia hapa kazi tu tumeitikia hewallah tumekubali ...hii yetu sisi shusha tanga pandisha tanga mbona inakuteseni ...tukuaminini nyinyi tu ...kuwaamini wengine iwe hatia ...Kama una Elimu ya PhD hemu itendee haki ...usiwe hivyo ndugu ...kupenda chama au mtu ni hiyari yake isiwe hatia na katiba si inaruhusu!!!
 
N
Hivi bado unateseka ...Alipokuja Mkapa mlituaminisha ndie mtakatifu kuliko wote waliopita tukakubali maana alijisifu ni mkweli na muwazi tukaitikia hewalla ...kaja Kikwete na Ari mpya nguvu mpya ...baadae akaongeza na kasi zaidi tukakubali ...kaja Magufuli mkamtaja Kama Masihi alieahidiwa ...akatuambia hapa kazi tu tumeitikia hewallah tumekubali ...hii yetu sisi shusha tanga pandisha tanga mbona inakuteseni ...tukuaminini nyinyi tu ...kuwaamini wengine iwe hatia ...Kama una Elimu ya PhD hemu itendee haki ...usiwe hivyo ndugu ...kupenda chama au mtu ni hiyari yake isiwe hatia na katiba si inaruhusu!!![/QUOTE

Ndomana nikasema siasa zetu ni za kufuata misimamo ya wanasiasa wakubwa na sio kuangalia itikadi na sera za vyama. Sasa ulipoletewa Mkapa, Kikwete na Magufuli ukawachagua kwa vile ulishawishiwa ufuate itikadi zao za uwazi, ari mpya na hapa kazi tu badala ya kuangalia misingi ya kiitikadi ya chama chao.

Leo mtu kasema SHUSHA TANGA PANDISHA TANGA unashobokea ukidhani kuna jambo jipya bila kujua kwamba huo sio msimamo au iitikadi ya chama bali ni ya mwanasiasa. Yaani leo umeipenda ACT ghafla kwavile kaingia Seif na si kwasababu ya itikadi ya kijamaa ya chama hicho.
 
Sasa mlitaka Maalim Seif astaafu Siasa?

Mmemtumia mamluki wenu Lipumbavu kumfukuza kwenye chama chake: yeye na wapambe wake, sasa wakijiunga na chama kingine mlitakaje?

Halafu unaandika mambo marefu yasiyo na kichwa wala miguu!

Sent from my CMR-AL09 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada, umesahau kujitambulisha kuwa hata wewe “unaunga juhudi za mheshimiwa Rais”. Umesahau pia sera ni sehemu ndogo sana ya ushawishi kwa wapiga kura - kauli mbiu ndio hubeba wanachama. Unakumbuka “Hapa Kazi Tu”, “Haki Sawa kwa Wote” nk??? Au “Ulipo Tupo” inachoma sana??

Umesahau hili pia, kama hushawishiwi na kauli mbiu hii - acha iwashawishi wengine. Ajabu unaweza kuwa mmoja wa wanaoona “Make America Great Again” kama nayo ni gia ya angani.
 
Masaa 6 bado hayajesha, wacha niendelee na serengeti zangu hapa nikuwachie wewe na uzi wako mbovu uliojaa propaganda za kijinga za CCM.
 
Back
Top Bottom