Gharib Mzinga apunguze kutoa historia kwenye mechi, atangaze mechi bhana

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
19,226
Reaction score
68,242
Jamaa anatangaza bolu dakika tano, dakika 40 anasimulia mambo ambayo hayana hata umuhimu, kipindi kinakuwa kimeisha anaboa sana.

“ametokea stade malieee akiwa MVP, akaenda kwenye kikosi cha kocha Gamondi akiwa na depu”

“Djigui Diarra alienda kumfata refa pale maana anatabia za uongozi alikua captain stade malien”

😂😂😂

Badilika mwanetu Kilwa Finest
 
Dunia nzima huo utangazaji ndivyo unavyokuwa,gharib the kilwa finest piga kazi mwanangu
 
Habari za kuaminika zinasema kuwa bwana Gharib Mzinga alishawahi kusifiwa humu JF na secretarybird, kuwa anajua kutanga boli kutokana na kuwa na jadi ya kutoa historia ya timu na wachezaji wakati wa matangazo ya moja kwa moja.

Inasemekana sifa hizo alizopewa na Ayatollah wa JF zilimlevya hata akawa anatoa tu historia ya wachezaji kuanzia dakika ya kwanza hadi ya tisini jambo ambalo sasa linaboa watazamaji wa mpira.

Hii inadhihirisha Ile methali inayosema 'Mgema akisifiwa tembo, hulitia maji'.
 
Jamaa anatangaza bolu dakika tano, dakika 40 anasimulia mambo ambayo hayana hata umuhimu, kipindi kinakuwa kimeisha anaboa sana.

“ametokea stade malieee akiwa MVP, akaenda kwenye kikosi cha kocha Gamondi akiwa na depu”

“Djigui Diarra alienda kumfata refa pale maana anatabia za uongozi alikua captain stade malien”

😂😂😂

Badilika mwanetu Kilwa Finest
Mimi napenda huo uwezo wake wa kutoa history so .NAOMBA AENDELEE MAANA NDICHO KIMEMPA MASHABIKI WENGI NIKIWEMO
 
Naona anataka aonekane kuwa anajua..
Ila me mwenyewe nakubali kuwa anajua kufukunyua historia 😁
 
Duniani kote huo mdio utangazaji wa kisasa wa kwenye televisheni. Mpira pale wote tunau9na kwa macho hivyo hakuna haja yeye awe amatangaza kila move wakati tunaiona. Amachofanya ni kuyashabihisha matukio tunayoyaona mchezoni na taarifa mbali ili kunogesha experience ya watazamaji.

Yuko vizuri sama Kilwa finest
 
Mkuu, upo sahihi sana! Utangazaji wa Radioni na kwenye TV, ni tofauti. Wapo watangazaji wa kwenye TV, hawajui hilo, wao wanatangaza hata mchezaji anaporuka juu na kupiga kichwa mpira, au hata beki anaporudisha nyuma mpira kwa golikipa. Kwenye TV, haya yote sisi watazamaji, tunaona!
Jamaa yupo vizuri sana, na wengine wajifunze!
 
Jamaa anatangaza bolu dakika tano, dakika 40 anasimulia mambo ambayo hayana hata umuhimu, kipindi kinakuwa kimeisha anaboa sana.

“ametokea stade malieee akiwa MVP, akaenda kwenye kikosi cha kocha Gamondi akiwa na depu”

“Djigui Diarra alienda kumfata refa pale maana anatabia za uongozi alikua captain stade malien”

😂😂😂

Badilika mwanetu Kilwa Finest
Acha wivu wewe. Watu wengi wamemjua na kumpenda kwa sababu hiyo unataka aache identity yake? We vipi bana...!!
 
Mpira wa UEFA na EPL unatangazwa hivyo sio anakwenda na mpira mara goo wao wanatoa history ya kila mchezaji inaonekana mpira wa Nje unaangalia tu ila hausikilizi au kuelewa kinachotangazwa usingeandika haya.
 
Jamaa anatangaza bolu dakika tano, dakika 40 anasimulia mambo ambayo hayana hata umuhimu, kipindi kinakuwa kimeisha anaboa sana.

“ametokea stade malieee akiwa MVP, akaenda kwenye kikosi cha kocha Gamondi akiwa na depu”

“Djigui Diarra alienda kumfata refa pale maana anatabia za uongozi alikua captain stade malien”

😂😂😂

Badilika mwanetu Kilwa Finest
Kwani unasikiliza redio
 
Atangaze boli kwani we huoni mkuu?? Yaani Diara kadaka mpira wewe huoni mpaka Mzinga akwambie "Diara adaka mpira pale"
 
Mkuu, upo sahihi sana! Utangazaji wa Radioni na kwenye TV, ni tofauti. Wapo watangazaji wa kwenye TV, hawajui hilo, wao wanatangaza hata mchezaji anaporuka juu na kupiga kichwa mpira, au hata beki anaporudisha nyuma mpira kwa golikipa. Kwenye TV, haya yote sisi watazamaji, tunaona!
Jamaa yupo vizuri sana, na wengine wajifunze!
Kama ishu ni kiona tu, watazamaji huona kila kitu, kwahiyo commentary na commentator haitajiki.

Mzinga anafanya vema kudokeza na historia fupi. Lakini siku hizi amekuwa mpaka anakera, imefikia hatua anashindwa kujua wapi atoe historia na wapi aendelee na commentary.. muda mwingine anazungumza hata visivyokuwa na mantiki..
 
Back
Top Bottom