Gharama za uongozi

Gharama za uongozi

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,739
Reaction score
5,703
GHARAMA ZA UONGOZI
Ni watu wachache sana wanaotambua adha, shida, manyanyaso, upweke, matusi, dharau, na mambo mengine magumu wanayopitia viongozi. Wengi wanapofikiri kuhusu majukumu na nafasi ya Uongozi wanavuta taswira ya heshima na utukufu dhana ambayo siyo sahihi hasa kama Uongozi huo unatoka kwa Mungu. Musa ni Kiongozi Mkuu aliyeheshimika sana na Mungu na wanadamu. Pia aliogopewa na maadui au nchi za jirani. Aliongoza taifa lililokuwa likiogopewa na kuheshimika na kutetemekewa sana. Uchumi wa nchi yake ulipoporomoka na baa la njaa lilipoingia, alitenda muujiza wa kuwalisha na pia kuwapa maji watu wake. Zaidi ya yote, alikuwa ndiye Baba wa Taifa la Israel aliyeongoza harakati za kulitoa taifa lake kutoka katika makucha au ukoloni wa Wamisri. Pamoja na hayo yote, wasaidizi wake wakuu tena ndugu zake (Haruni na Miriamu) waliongoza magenge ya kumpiga vita, kumtukana, kumchafua, na hata uasi uliozaa mapinduzi dhidi ya Kiongizi Mkuu Musa. Maasi na mapinduzi yale yalikuja kuzimwa na Mungu mwenyewe. Mungu alipotaka kuwaua wasaidizi wale ambao sasa waligeuka kuwa mwiba Musa aliwaombea msamaha kwa machozi hadi Mungu akawasamehe (Soma tukio zima katika Kutoka 12). Viongozi wengi wa Kanisa, jamii, siasa na hata serikali wanapitia katika changamoto za kutukanwa, kugeukwa, kuonewa wivu, kunyanyaswa, kuchafuliwa, na hata kusingiziwa! Kwamba hayo yanafanywa ma marafiki na sio maadui ndicho kinaongeza maumivu zaidi. Jaribu kubwa kwa kiongozi anayepitia changamoto hizo ni kutaka kujaribu kujibu mapigo jambo ambalo linapelekea uongozi wake uchuje mbele ya safari.
Ninao ujasiri kumtia moyo kila mtu anayetimiza majukumu na wajibu wa Uongozi ili atambue kuwa kashfa, matusi, wivu, na dharau dhidi ya wale walioitwa kutumikia wajibu wa Uongozi ni baadhi ya mitihani ambayo hatuna budi kuipitia. Kamwe tuepuke majaribu na misukumo inayotutaka tujibu mapigo. Zaidi ya yote tuepuke kutumia nafasi zetu ili kupambana nao au kuwanyamazisha. Kati yao wapo watakaotujia tena baadaye kwa kutaka kuomba ushauri na msaada. Tuwe tayari kuwasaidia na hatimaye Mungu atawatumia hao hao kutusafisha matope waliyoturushia. Furaha na kipimo cha Uongozi ni pamoja na kuwahudumia kwa furaha na upendo watu wote wakiwemo wale walioshiriki kutuchafua na kurarua mioyo yetu.
 
Heshima Comrade.

Uongozi una gharama kubwa Sana. Moja ya gharama kubwa za uongozi kwa nyakati zingine (Panapostahili) Ni kuutoa uhai wako kwa ajili ya wengi.

Hua namtafakari Sana Mungu. Ni kwanini aliamua kumtoa mwanaye wa pekee kwa ajili ya dhambi zetu na si kingine?. Hakukuwa na mbadala zaidi ya Yesu kufa/ ishara ya kumwaga damu ili tukomboke?.

Nadhani ipo hivi (Naweza nisiwe sawa ila tafadhali niache nisivyostahili kulingana na Mimi mwenyewe), Ishara ile ilikuwa na maana moja "Hakuna ukombozi pasipo kumwaga damu".

Damu ya Yesu ilibidi imwagike pale msalabani ili tupate wokovu na si kingine (Nb; kwa wanaoamini). Kwa wenye misimamo iso ya kiorthodox si lazima muunge mkono hili, You may agree or dis-agree.

Zamani uongozi ulikuwa na adha zake. Leo uongozi Ni kimbilio la karibu kila mtu huku kila mmoja wetu akiwa na dhamira yake inayomuongoza.

Baba zetu wa Kiimani, kuanzia kina Musa, Yusufu, Suleimani, Ezekiel, Yeremia nk hawakuwa wakiutaka uongozi kwa makusudi kwakuwa walifahamu fika Gharama za Uongozi. Mungu anamtuma Musa kuwa kiongozi ili akawaokoe wana wa Israel kule Misri lakini Musa anakuwa mgumu Sana kuelewa.Kwanini?..kwa sababu uongozi una gharama zake. Musa alikuwa akijaribu kukwepa hizi Gharama.

Tatizo si kuwa kiongozi, Tatizo Ni vipi utatatua kero za wananchi bila kuendelea kuwaongezea matatizo?..

Uongozi si kuwa na Ofisi. Uongozi Ni utatuzi wa matatizo.
 
Jamani mnalinganisha usiku na mchana!! Ni vitu viwili tofauti!! Uongozi wa kinaMusa haukuwa wa kugawanya watu, visasi na chuki dhidi ya wengine, haukuwa na upendeleo wa watu (kabila)wa karibu yake . Ile ilikuwa leadership lakini huu ni utawala
 
Back
Top Bottom