Gharama za ujenzi wa lodge

Bwegemsela

Member
Aug 30, 2019
39
125
Habari za jioni wana jamvi mm ni kijana wa kitanzania ambaye napambana na hili janga la umasikini, nina bajeti ya 50ml nahitaji kujenga Lodge ya kiwango cha kati Room zisizopungua 7 reception na counter vyumba vyote self, gharama za kiwanja pembeni, naombeni wajuzi mnisaidie kwa ushauri na maelekezo pia
 
Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
877
1,000
Ushauri (kitonga): vuta umeme na maji site halafu tenga 10m nunua mashine ya tofali na mixer na material za tofali kisha fyatua tofali weeeeeeeeeeeeeeee. Halafu tumia hizo tofali zako kujengea. Utapunguza 40% ya gharama.

NB: Gharama inategemea na michoro ya gesti yako. Kama upo mkoani jenga kwa tofali za kuchoma, kisha piga plasta KWISHA KAZI!
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,235
2,000
Bajeti yake ni 50m. 10m ni 20% ya bajeti yake. Aingie gharama ya 10% kwanza halafu aje aokoe 40%? Kwani matofali ni 40% ya gharama za ujenzi? Matofali ni sehemu ya Boma ambalo linaweza kugharimu chini ya 30% ya gharama za nyumba nzima.

Kwanini asinunue tu matofali kuliko kuhangaika kufyatua mbaya zaidi anunue na mashine?
 
Kagi Rasta

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
250
500
Inatoshaaaa sana kama uko mkoan au nje ya mji jengea tofali za kuchoma tumia molam ndio iwe kama siment kwenye piga renta ndio tumia nondo na siment kisha piga lipu mzee utajikuta jengo limeinuka lote afu ata 10M haijaisha, ila jitahd kwny bat uweke japo za rang maana muonekano wa lodge ndio pesa yenyewe nunua yale mabat ya geji 30 yanakuwa mwng hv afu ubapige kuna rang za mabati yapake uweke muonekano mzur
 
Bwegemsela

Member
Aug 30, 2019
39
125
Nashukuru kwa ushauri wako mzuri
Inatoshaaaa sana kama uko mkoan au nje ya mji jengea tofali za kuchoma tumia molam ndio iwe kama siment kwenye piga renta ndio tumia nondo na siment kisha piga lipu mzee utajikuta jengo limeinuka lote afu ata 10M haijaisha, ila jitahd kwny bat uweke japo za rang maana muonekano wa lodge ndio pesa yenyewe nunua yale mabat ya geji 30 yanakuwa mwng hv afu ubapige kuna rang za mabati yapake uweke muonekano mzur
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,006
2,000
Unampoteza mwenzio ,huo ni ujenzi wa miaka ya nyuma sana sio sasa, route unayomshauri atapoteza muda , pesa na unaweza na asipokuwa lakini hata quality ya tofali itakuwa mbovu
Ushauri (kitonga): vuta umeme na maji site halafu tenga 10m nunua mashine ya tofali na mixer na material za tofali kisha fyatua tofali weeeeeeeeeeeeeeee. Halafu tumia hizo tofali zako kujengea. Utapunguza 40% ya gharama.

NB: Gharama inategemea na michoro ya gesti yako. Kama upo mkoani jenga kwa tofali za kuchoma, kisha piga plasta KWISHA KAZI!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
877
1,000
Unampoteza mwenzio ,huo ni ujenzi wa miaka ya nyuma sana sio sasa, route unayomshauri atapoteza muda , pesa na unaweza na asipokuwa lakini hata quality ya tofali itakuwa mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hii mbinu ya kizamani ambayo niliiona ni mbinu ya kimagumashi halafu inapoteza muda sana. Ila kwa siku za karibuni imeanza kurudi kasi. Mimi binafsi katika kuzururazurura nikauliza kwa nini wanafanya hivyo na wahusika wakaniambia mbinu hiyo ya kizamani inapunguza gharama sana.

Mimi nimetoa maoni tu kwa mtazamo wa mtaani na yeye pia afanye utafiti wa mbinu ipi inayofaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom