Gharama za ujenzi banda la mbuzi

PresidentSalum

Senior Member
Dec 3, 2006
189
21
Ndugu zanguni, natumaini wote wazima wa afya. Naomba kujua gharama za ujenzi wa banda la mbuzi zipo vipi. Nimepanga kuanza na mbuzi 10 maeneo ya kibaha. Lakini iwapo nitafanya vizuri kwenye ufugaji, ningependa kuexpand lakini kwa sasa nitaanza na hao mbuzi 10. Asanteni sana.

Pia kama mtanisaidia na bei za mbuzi nitashukuru. Bei za mbuzi wa umri wa kati, yaani sio mtoto na sio mzee nitashukuru. Na wapi naweza kupata kwa bei nafuu. Natanguliza shukrani.
 
Kwa kuwa na mimi nina wazo la kufanya hii project,ningependa kujuzwa mambo kadhaa;
1.Changamoto za ufugaji wa mbuzi i.e magonjwa,ukubwa wa eneo nk hasa katika maeneo ya Dar
2.Gharama tangu udogoni hadi kufikia rika la kuuzwa i.e chakula,dawa nk
3.Masoko yakoje hasa kwa watu wanaoishi Dar
4.Aina bora ya mbuzi ukizingatia lengo ni kukuza kipato na si ufahari.
5.Tangu kuzaliwa hadi kukomaa wanachukua muda gani,pia wanazaa kila baada ya muda gani?

Ni hayo tu wadau,
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Ndugu zanguni, natumaini wote wazima wa afya. Naomba kujua gharama za ujenzi wa banda la mbuzi zipo vipi. Nimepanga kuanza na mbuzi 10 maeneo ya kibaha. Lakini iwapo nitafanya vizuri kwenye ufugaji, ningependa kuexpand lakini kwa sasa nitaanza na hao mbuzi 10. Asanteni sana.

Pia kama mtanisaidia na bei za mbuzi nitashukuru. Bei za mbuzi wa umri wa kati, yaani sio mtoto na sio mzee nitashukuru. Na wapi naweza kupata kwa bei nafuu. Natanguliza shukrani.

Mambo mkuu. Vp kuhusu hii project yako?mpaka sasa.na kuhusu mbuzi wanao zaa mapacha cheki na huyu mtu.
5bfcbd3944ac52776c6b980135cf5250.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom