Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 3,036
- 8,394
hapo tu ndipo napo shindwa kuelewa kwa kweli .. hili swala la kuchangishana harusi sendoff niliachwe kabisa....
gharama zisizoepukika kutoka mfukoni mwako na ili bibi arusi akuheshimu niiiiiiiiii;
Gharama za mahari
Mavazi ya bibi harusi
Mavazi yako mwenyewe
Gharama za honey moon
Pesa ya kuanzia maisha baada ya ndoa
mkuu mimi hapa mama yangu akiongelea hayo mambo tunapishana kwa sababu tu mimi naamini ndoa na sitaki harusi.... kwa hiyo nimeshaamua na hapa nilipo najaribu kumshawishi huyu mpenzi wangu kuwa aachane na maswala ya harusi tufunge ndoa.. na namshukuru Mungu tupo karibu kuelewana japo anahisi kama kuna jambo namficha... ninakajukumu cha kuendelea kumshawishi mpaka tuelewane tu... mwenzangu akinielwa anakazi na yeye yakuelezea wazazi wake pia waelewe... now days bwana wazazi ndiyo wamekuwa watu wa kwanza kushurutisha harusi mara send off sababu kubwa atakuambia kuwa amechangia harusi nyingi na yeye anatakiwa achangiwe ambapo to me ni hoja jepesi tu hiii ... any way msimamo wangu siubadilishi sababu sitendi dhambi ila nafanya lile la msingi
hapa umesema la maaana ila ukiona mtu anatangaza nia ni kwamba karidhika na mwenzakewengi tunaandaa mambo ya nje nivae shela harusi kubwa ... tunaandaa kufurahisha jamii huku tukisahahu kujifanyia evaluation in detail je kweli moyo wangu upo tayari kuishi na huyu binti na je nitamvumilia mangapi kwa mda gani? na je yeye kajiandaa kiasi gani kukubaliana na mapungufu yangu? na je ni kweli kuna chemistry between you too au mnaoneana huruma au mnafanya tu bila kujua kwa nini mnafanya? lingine mmemtanguliza Mungu kiasi gani katika kusimamia ndoa yenu au Mungu anapewa nafasi ndogo ndiyo maana hata kwenye kadi mnawaambia watu mkutane ukumbini huku tendo muhimu la ibada hamataki jamii ishiriki ,, na pia ninyi mpo pale kama misanamu tu huku mkiwa na mawazo sijui ukumbini kumepelea nini? sijui mtu wa keki kafika ? sijui kamati imekaaje?
muhimu ni kuandaa mioyo zaidi kuliko sherehe za masaa mawili wakati ndoa ni maisha ..........
kama karidhika na mwenzake mafigisu figisu baada ya ndoa yanatokaga wapi? kwa baadhihapa umesema la maaana ila ukiona mtu anatangaza nia ni kwamba karidhika na mwenzake
kama karidhika na mwenzake mafigisu figisu baada ya ndoa yanatokaga wapi? kwa baadhi
Unaona tatizo hilo?yani kwanza uanze kuwaelewesha wazazi wako,pili umueleweshe wenzio halafu nayeye akawaeleweshe wazazi wake duh!japo naona inakuwa rahisi kwa upande wa kiume kukubali.mkuu mimi hapa mama yangu akiongelea hayo mambo tunapishana kwa sababu tu mimi naamini ndoa na sitaki harusi.... kwa hiyo nimeshaamua na hapa nilipo najaribu kumshawishi huyu mpenzi wangu kuwa aachane na maswala ya harusi tufunge ndoa.. na namshukuru Mungu tupo karibu kuelewana japo anahisi kama kuna jambo namficha... ninakajukumu cha kuendelea kumshawishi mpaka tuelewane tu... mwenzangu akinielwa anakazi na yeye yakuelezea wazazi wake pia waelewe... now days bwana wazazi ndiyo wamekuwa watu wa kwanza kushurutisha harusi mara send off sababu kubwa atakuambia kuwa amechangia harusi nyingi na yeye anatakiwa achangiwe ambapo to me ni hoja jepesi tu hiii ... any way msimamo wangu siubadilishi sababu sitendi dhambi ila nafanya lile la msingi
Unaweza kumpata mwelewa tatizo likawa kwa wazazi na ndugu,ukingalia tayari tushatofautana dini.Mwenzangu sio mtu wa kupenda masherehe makubwa makubwa kwa hiyo tulikibaliana vizuri tuu wala hakukuwa na shida.
Hatukutaka kuanza kukimbizana na watu michango ya harusi mpaka iwe kero, au tumalize harusi tuanze maisha na madeni kwa sababu ya sherehe ya masaa machache tuu. Hasa ukizingatia kuwa uwezo wetu kiuchumi ulikuwa ni.mdogo pia. Tulifanya kitu simple sana.
Bajeti ilikuwa kwa watu 60; ambao walikuwa ni ndugu zetu wa karibu ma close friends wachache.
Pesa kubwa ilienda kwenye chakula na vinywaji; ukumbi tulipewa bila kuulipia as i said hoteli ya nemax royal iliyopo kinondoni(kwa sababu vinywaji na msosi tulichukua hapo hapo).
Hakuna cha maids wa bibi harusi zaidi ya matron wa bi harusi na mpambe wangu.
Gharama nyingine ndogo ndogo zilikuwa ni keki,picha,shampeni. Ukumbi walitupangia tuu viti na meza vizuri na high table(no mapambo complicated).
MC akawa dada yangu, na tulitumia Public addressing system ya ukumbi tuka connect our laptop bro akawa DJ.
Mimi binafsi nilipenda sana jinsi ilivyokuwa kiukweli,it was nice and no stress!!! Na,hata waliohudhuria walisema nimefanya,kitu kizuri sana.
Bajeti(kadri ninavyokumbuka)
1.chakula
20,000 @ plate X 60=1200000
2.vinywaji(bei ilikuwa ni moja, Tshs 2,000 kwa bia au soda)
Kwa bia 4 @ 2000X 40=320000(kwa watu wetu tuliowaalika coz ni wa karibu,tunawajua personally,i tulijua wanywaji hawatazidi 40)
Kwa soda 3@ X 2000 X 20=120000
Picha za mnato=140,000
Keki= 250000
Usafiri wa wakwe(tulichukua noah ya mshikaji tukampa 40,000 na kuijaza mafuta)
Gari ya maharusi tulitumia ya kwangu.
Kupambwa bi harusi + kupamba gari ya maharusi 150,000
Champane @ 15,000 X 3=45,000
TOTAL 2,265,000. CHOCKSTIC