Ndugu zangu wana JF,Mimi kijana mwenzenu naomba kuchukua nafasi hii kuomba kujuzwa gharama halisi za kuandaa
sherehe ya harusi,
nimeona nitumie jukwaa hili kwa kuamini ya​ kwamba nitapata maoni na taarifa kutoka kwa watu ambao wameshapita kwenye hatua hii na pia itakuwa msaada kwa ambao wanajiandaa kuingia kwenye hatua hii kama mimi,nimekuwa kwenye mahusiano na mwenzangu kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu sasa na sio kwamba muda wote huo nilikuwa sitaki kuoa ila kila nikifikiria gharama za sherehe zinanikwamisha hasa nikiangalia kipato changu,nimekuwa nikisema ngoja nisevu pesa kwaajili ya jambo hili lakini mwisho wa siku yanatokea mambo yanaharibu mipangilio yangu.
kwa sasa nimeona liwalo na liwe, nimepanga kuoa mwakani mwezi wa tisa mungu akipenda,kwahiyo kwa kutumia jukwaa hili naomba kujuzwa bajeti ambayo inatosha kuandaa sherehe ya kawaida ambayo tunaweza tukajumuika na kufurahi ambayo haitakuwa na mbwembwe nyingi kwa maana ya kwamba mimi kama bwana harusi nahitaji kuwa na kiasi gani?maana nikiangalia uwezo wa familia na watu wa wangu wa karibu ni mdogo,maana nataka niangalie kama naweza ningependa nusu ya gharama ya bajeti nijigharamie mwenyewe,natumini nitapata maelekezo chanya kwa maana ya wapi nitapata ukumbi,mc,vinywaji,nakadhalika ambavyo vitakuwa standard lakini kwa bei ya kawaida.
kwa ufupi ni hayo,kama kuna makosa ya uwasilishaji na uandishi mtanisahihisha.
naomba kuwasilisha kwenu,
NB,gharama ziwe za sherehe ya ukumbini
Nipo DSM,kuhusu dini mimi muislam mwenzangu mkristo,kuhusu pombe zitakuwepo.Uko mji gani? Na je unafunga ndoa ya aina gani? Kiislamu, Kikristo, ya Kimila au Bomani? Je kwenye sherehe ya harusi ungependa pombe ziwepo au lah?
Ndio maana nataka kujua gharama zisizoepukika ni kiasi gani nijiandae kabisa.Kaa ukijua hakuna sherehe ndogo so gharama haziepukiki
Kumbuka pia kueka hela ya emergency
Labda unisaidie hapo kidogo,niuandaeje moyo?usisahahu pia kuandaa moyo wako,,,
wengi tunaandaa mambo ya nje nivae shela harusi kubwa ... tunaandaa kufurahisha jamii huku tukisahahu kujifanyia evaluation in detail je kweli moyo wangu upo tayari kuishi na huyu binti na je nitamvumilia mangapi kwa mda gani? na je yeye kajiandaa kiasi gani kukubaliana na mapungufu yangu? na je ni kweli kuna chemistry between you too au mnaoneana huruma au mnafanya tu bila kujua kwa nini mnafanya? lingine mmemtanguliza Mungu kiasi gani katika kusimamia ndoa yenu au Mungu anapewa nafasi ndogo ndiyo maana hata kwenye kadi mnawaambia watu mkutane ukumbini huku tendo muhimu la ibada hamataki jamii ishiriki ,, na pia ninyi mpo pale kama misanamu tu huku mkiwa na mawazo sijui ukumbini kumepelea nini? sijui mtu wa keki kafika ? sijui kamati imekaaje?Labda unisaidie hapo kidogo,niuandaeje moyo?
Uko sawa,sasa nahitaji kujua mavazi yatakuwa bei gani?kama ni dukani au kwa designer?wenye uzoefu waweke madesigner wazuri wenye bei inayowezekana,kama ni ukumbi upi utanifaa na utakuwa affordable?yani mwisho wa sikugharama zisizoepukika kutoka mfukoni mwako na ili bibi arusi akuheshimu niiiiiiiiii;
Gharama za mahari
Mavazi ya bibi harusi
Mavazi yako mwenyewe
Gharama za honey moon
Pesa ya kuanzia maisha baada ya ndoa
Uko sawa,sasa nahitaji kujua mavazi yatakuwa bei gani?kama ni dukani au kwa designer?wenye uzoefu waweke madesigner wazuri wenye bei inayowezekana,kama ni ukumbi upi utanifaa na utakuwa affordable?yani mwisho wa siku
nikitoka hapa niwe na picha ya bajeti itakavyokuwa
wengi tunaandaa mambo ya nje nivae shela harusi kubwa ... tunaandaa kufurahisha jamii huku tukisahahu kujifanyia evaluation in detail je kweli moyo wangu upo tayari kuishi na huyu binti na je nitamvumilia mangapi kwa mda gani? na je yeye kajiandaa kiasi gani kukubaliana na mapungufu yangu? na je ni kweli kuna chemistry between you too au mnaoneana huruma au mnafanya tu bila kujua kwa nini mnafanya? lingine mmemtanguliza Mungu kiasi gani katika kusimamia ndoa yenu au Mungu anapewa nafasi ndogo ndiyo maana hata kwenye kadi mnawaambia watu mkutane ukumbini huku tendo muhimu la ibada hamataki jamii ishiriki ,, na pia ninyi mpo pale kama misanamu tu huku mkiwa na mawazo sijui ukumbini kumepelea nini? sijui mtu wa keki kafika ? sijui kamati imekaaje?
muhimu ni kuandaa mioyo zaidi kuliko sherehe za masaa mawili wakati ndoa ni maisha ..........
Unafikiri una uwezo wa kuwa na shilingi ngapi? Hapo ndio mwanzo
duh si mingi kwa sababu mingi mmefichana...... mi gharama za harusi sina.. mimi naweza kukushauri achana na harusi funga ndoa tu kalale home japo ni ngumu kukubaliHiyo ni point,lakini kwasasa tuongelee gharama za sherehe maana naamini kwa miaka mitatu tumeshapitia mitihani mingi
na imenitosha.
Nipo DSM,kuhusu dini mimi muislam mwenzangu mkristo,kuhusu pombe zitakuwepo.
kawaida unatakiwa uwe na ngapi labda?
duh si mingi kwa sababu mingi mmefichana...... mi gharama za harusi sina.. mimi naweza kukushauri achana na harusi funga ndoa tu kalale home japo ni ngumu kukubali
kufunga ndoa muhimu .. ila kufanya harusi si muhimu...labda nikuulize,wewe ungekubali kuwa kwenye uhusiano kwa miaka mitatu na zaidi na mwenzako muwe mnachunguzana bado?kuhusu kufunga ndoa mimi kwangu ningetaka iwe hivyo lakini mwenzangu,ndugu zangu za jamaa
hawawezi kunikubalia.