DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 302
- 274
Wanabodi,
Miradi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya sita inafanywa kwa dhumuni la kuwasaidia wananchi na kutuvusha kutoka kwenye hali tuliyonayo sasa hivi kuelekea kwenye hali nzuri zaidi. Siku zote, serikali hukusudia mema kwa wananchi wake na kwasababu hiyo ni vyema kuipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu katika kusimamia miradi mingi ya maendeleo nchini.
Katika kukubali mambo mema yanayofanywa na serikali, sikubaliani kwa kiasi kikubwa na njia inayotumiwa na serikali kutekeleza miradi hii ya maendeleo. Ni muhimu kuelewa kwamba siku zote, serikali ndiyo hutumia fedha nchini kuliko mtu au kundi lolote la watu na katika kutumia kwake huwezesha wananchi kunufaika kiuchumi. Lakini swali kuu la kujiuliza ni, hizi fedha za kuendesha miradi hii zinatoka wapi?
Katika kipindi cha nyuma kidogo, serikali iliamua kuchukua hatua ya kukopa fedha kutoka mashirika ya fedha duniani ikiahidi wananchi kwamba mikopo hii niya gharama nafuu na kwamba ina manufaa zaidi katika kukamilisha miradi ya maendeleo hata kama itaichukua serikali miaka ishirini au zaidi kulipa. Siku ya Jumanne, tarehe 13 mwezi wa tisa, makamu wa Rais, Phillip Mpango alizindua stendi iliyopo kata ya Nyamongholo jijini Mwanza nakusema kwa mradi huu uliigharimu serikali bilioni 26.65.
Aliye mtaalam zaidi kwenye masuala ya ujenzi anaweza akafanya tathmini kwasababu gharama hiyo kubwa sana kwa ajili ya stendi tu. Ukijaribu kuchunguza kwa kina zaidi fedha zinazo endelea kutumiwa na serikali kwa miradi mbalimbali, utagundua kwamba gharama za miradi hii, haswa za ujenzi, haziendani na hali halisi iliyopo mitaani. Kutoka kwenye stendi ya mabasi ya bilioni 26.65, miradi ya maji iliyo gharimu milioni 500, shule zilizo gharimu bilioni moja, masoko yaliyo gharimu milioni 500 au zaidi, je kwa mikopo hii tutafika?. Je gharama hizi zina ashiria matumizi mabaya ya rasilimali za serikali?
Kama binadamu, ninapenda kusisitiza umuhimu wa kuishi ndani ya uwezo wako na kwasababu hiyo, nina ndoto ya kuona taasisi zote za serikali zinaji tegemea, ndoto ya kuona nidhamu katika nyadhifa zote za uongozi serikalini, ndoto ya kushuhudia siasa safi nchini. Labda kuna mambo ya ziada ambayo hatufahamu kama wananchi, labda kukopa fedha kutoka kwa wananchi kwa njia ya bonds badala ya kukopa kwenye mashirika ya fedha ingeleta ahueni kwa pande zote mbili, labda mikopo inatupotosha.
Ni muhimu kufanya tathmini ya miradi yote ya serikali ili kufahamu kama kodi za wananchi zimetumika ipasavyo na kama maamuzi ya serikali kutupeleka kwenye mkondo huu ni sahihi.