Gharama za kwenda Cape Town na kukaa siku moja?

Gharama za kwenda Cape Town na kukaa siku moja?

Naomba kujua nauli ya ndege kutoka Dar to Cape Town ni kiasi gani kwa pesa ya madafu ya madafu, utaratibu wa kupata visa upoje na miji gani ya kiutalii ninayoweza kuitembelea mtu wa hali ya chini... natanguliza shukrani
 
Watanzania kwenda South Africa hatuhitaji kuwa name visa,ilishatolewa issue ya visa
 
pusha la magogoni
Mambo vp?..Kuna kama Harbouredge Apartments ni kama 120,000/=
Spring Tide In 75,000/=tzs...Vile vile ukitalii mitaa ya camps bay na sea point utapata za bei ya chini zaidi na ubora wake ni mzuri tu.Karibu sana dizonga pusha.

Umenikumbusha mitaa ya Camps Bay nilikuwa nakatiza tu kwenda Cape University na W & A
 
Beba na ugali wako kuokoa garama .maana unaelekea unapenda bwerele sana wewe
 
Hata mimi nimekuwa napafikiria sana capetown nikaione ile ncha ya africa ambapo bahari mbili zinaungana asante kwa aliyeko huko kwa kutujuza gharama si kivilee kawaida tu.
 
Ujiandae kupigwa "tero" sana maana kijana ukitokea Bongo unaonekana ni mtu wa "Ngada".
 
Da huwa natamani sana kwenda kuspend south na Nairobi lakini sasa naogopa kweli basi tu
 
Utabakia hivyo hivyo!!!!

Mkuu siwezi baki hivihivi.
Sehem za kutembelea zimeisha kwani?
maeneo ya namna hiyo mimi naenda kikazi tu.
Lakini siyo kwa kuzichanga.
kwa taarifa yako hata hali ya kisiasa ilivyo huko bongo kuelekea uchaguzi mkuu imepunguza kasi ya watalii kuingia nchini.
kwahiyo usinione mi mshamba saana kwa kuogopa makwerekwere.
 
Mkuu siwezi baki hivihivi.
Sehem za kutembelea zimeisha kwani?
maeneo ya namna hiyo mimi naenda kikazi tu.
Lakini siyo kwa kuzichanga.
kwa taarifa yako hata hali ya kisiasa ilivyo huko bongo kuelekea uchaguzi mkuu imepunguza kasi ya watalii kuingia nchini.
kwahiyo usinione mi mshamba saana kwa kuogopa makwerekwere.

Makwerekwere ndio kitu gani mkuu?
 
Back
Top Bottom