Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,195
- 10,709
Habari wanajukwaa! Poleni na hongera kwa harakati za maisha. Kuna jambo ningependa sana kulileta ili tutazame namna ya kupeana ushauri kuhusu biashara.
Hivi karibuni kumekuwa na watu wengi wanaofanya biashara ya kutoa huduma ya kuweka ama kubandika wallpaper kwenye kuta ndani ya nyumba ama vyumba, na wanatumia mtandao kutangaza huduma hii na mfano bora wa matangazo yao huwa katika namna hii:
Karibuni tunatoa huduma ya kubandika wallpapers ndano ya nyumba na vyumba. Wallpaper zinazovutia sana na kukiweka chumba chako kikiwa na na muonekano mzuri na wenye kuvutia sana.
Tsh 25 000/= kwa roller moja
Urefu mita 10
Upana 53 cm
Gundi 10,000
Ufundi sh 10,000 kwa kila roller moja.
Tupo mtaa wa Kariakoo Dar es salaam.
Tatizo ambalo nimekuwa nikiliona kwenye matangazo mengi ni kuweka mchanganuo wa bei tatu, yaani bei ya roller ya Wallpaper, kisha bei ya gundi halafu mwisho kuweka na bei ya fundi.
Nadhani hii kitu ni afadhali angeweka kuwa bei ni 45,000 ili mtu ajue kuwa akitoa hiyo pesa anapata huduma ya kubandikiwa roller moja. Gundi ya 10,000 kubandika roller moja inaleta walakini kwa mtu ila akisema kuwa kubandikiwa wallpaper roller moja ni 45,000 mtu anakuwa na uelewa wa moja kwa moja.
Kwa mchanganuo wa bei ambazo zipo kwenye matangazo mengi ni sawa na kusema kama mtu anataka kubandika roller 4 ambazo ni mita 40 basi atahitajika kuwa na 180,000, ama ni sawa na uelewa kuwa ukichukua roller tatu basi watakuwepo mafundi watatu na kila fundi atakuwa na gundi yake ambayo ni elfu 10.
*Nawasilisha!