Gharama za kupiga plasta nyumba

Bulamba

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
13,649
12,939
Najenga nyumba ya vyumba vitatu Kigamboni.Naomba kujua gharama za makisio za ufundi za kupiga plasta nyumba ya vyumba vitatu.

Na pia kama kuna fundi mzuri Kigamboni Dar.
 
Fundi wangu anataka Milioni 1.7 kufanya plasta ndani na nje pamoja na kupiga skimming.

Kutengeneza floor ametaka laki sita pamoja na kuweka timanzi.

Je hizi ni bei halisia kwa nyuma ya vyumba vitatu na sebele na jiko na choo cha public?
Kati ya vile vyumba vitatu viwili ni self contained.
 
Laki mbili? Kwa nyumba ya vyumba vitatu ufundi hauwezi kupungua laki6. Ukitaka kazi nzuri, kupiga plaster ndani na nje pamoja na skimming ya kuta zote na dari pamoja na kupiga msasa, mpe milioni moja. Hiyo ni kazi ya wiki mbili kwa mfundi wa3 au wa2 na msaidizi mmoja.
 
Hapo itahitajika mifuko 6 cement kwa ajiri ya kupiga ndani tu ukitaka mpaka nje ongeza ifike 11.pesa ya ufundi ntakufanyia laki nne kwa ndani na ukihitaji mpaka nje ntakufanyia jumla laki saba
Je kama Nahitaji kumwaga jamvi ni mifuko mingapi ya cement kwa ajili ya jamvi tu kwa nyumba hiyo ya vyumba vitatu?
 
Mafundi wanawaibia sana watu,kupiga floor ni laki 6? Kupiga plasta hadi milioni vyumba vi3? Poleni mnaoibiwa,kuna mafundi wapo mitaani wazuri na wanapiga kwa bei nzuri,ukienda kichwa kichwa gari kubwa lazima upigwe...mie kuna Fundi alinipigia floor chumba na sebule/chumba mita nne kwa mita nne kwa elfu 40.
 
Kuna jamaa hpa jukwaani ni kazi yke hiyo,aliweka uzi ambao mpaka leo unaendelea na kashafanya kazi na bbadhi ya watu alokutana nao hapa jukwaani,jina analotumia hapa jf ni pmoses95 search hilo jina alafu mtumie messege atakusaidia na yeye yupo mitaa ya kigamboni kama sikosei.
 
Back
Top Bottom