Gharama halisi za power tiler kutoka China

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,283
7,834
Wakuuu,nimejaribu kupitia nyuzi mbalimbali zinazohusu power tiler lakini nyingi ni 2012 kurudi nyuma. Pia watu wengi wameshamaliza mizigo hiyo. Sio kwamba hazipo mtaani,zipo ila bei si rafiki sana,nimejaribu kuangalia mitandaoni nimeona kuna uafadhari iwapo itaagizwa moja kwa moja.

Kupitia alibaba bei zina range US$80-150 kwa used, na 500-1200 kwa mpya kwa seti moja. Kilichofanya nije hapa ni kubadilishana mawazo juu ya njia bora ya kununua hizi mashine.
Mtaani bei ni Tsh 3.5mil-11mil,ukiangalia hizi bei ni km Mara tatu ya zile za mtandaoni.TUSAIDIANE KATIKA
a344311792c0abd01369a4f5d3964f32.jpg
:

GHALAMA NA TARATIBU ZA USAFIRISHAJI

Watu wanaoagiza magari anaweza kuagiza moja na akaletewa,je kwa upande wangu naweza kuagiza seti moja tu! Na nikaletewa?. Pia nimeangalia mizigo mikubwa huwa kwenye makontena,lakini powertiler set moja ni box moja tu la mbao,je kunauwezekano wa kusafirishwa katika hali hiyo?

Pia ghalama za bandalini zipoje kwa upande wa powertiler au hupigwa hesabu kwa kontena zima?

Tusaidiane maana isije kuwa ghalama ni kubwa kuliko za mitaani au nikalizwa tu mitandaoni

af7a4b04d56768de5cc6e462e563258e.jpg

UPDATES: NIMEPATA POWER TILLER MPYA

Nawashukuru wadau wote kwa michango ya mawazo na wengine mliokuja PM kunipa muongozo n.k. nilipoona mipango imeyumba niliipeleka hela kwenye kilimo. Mwaka huu nimepata 8mil na katika pita pita mtaani nikapata taarifa juu ya power tiller zinazoizwa na mbunge wa mbarali kwa bei ya 2 mil ikiwa full kila kitu eg disc plough, Rotavator, iron/Cage wheels+trailer.

Mwezi may 27 2018 Nimechukua hiyo na mpaka sasa inapiga kazi za kusomba mchanga,tofari na mazao nimerudisha kwa hiyohiyo.

Nimenunua Amec 18 HP

Nawashukuruni sana kwa michango yenu ya mawazo , kama nawe utahitaji nitakusaidia uipate

Picha zinagoma kupanda
 
Last edited:
kama umeona mtandaoni jaribu kuwasiliana na kampuni inayo uza kama wanaweza kukuuzia 1 set.kuhusu utumaji wake unaweza ukawapa address wakutumie TZ ,kisha ikifika utalipia ushuru.ama wakutumie kwenye kampuni za kusafirisha mizigo toka china kwenda Tz.ukitumia njia ya pili nadhani ni rahisi kwani utoaji wa bandarin watatoa wao.wewe ni utafata ware house kwao mzgo ukisha fika.
kila la kheri mkuu
 
Kuna mzee flani yuko huko kilimanjaro nilimuona tv1 ametengeneza tractor dogo zuri yani over imporeted katumia engine ya pikipiki na linalima heka 3-4 kwa siku kutegemea na eneo lilivyo.
yani ni zuri kama vile limekuwa impored mtafute akutengenezee.
sijui kwanini serikali haiwekezi kwa watu kama hawa
 
kama umeona mtandaoni jaribu kuwasiliana na kampuni inayo uza kama wanaweza kukuuzia 1 set.kuhusu utumaji wake unaweza ukawapa address wakutumie TZ ,kisha ikifika utalipia ushuru.ama wakutumie kwenye kampuni za kusafirisha mizigo toka china kwenda Tz.ukitumia njia ya pili nadhani ni rahisi kwani utoaji wa bandarin watatoa wao.wewe ni utafata ware house kwao mzgo ukisha fika.
kila la kheri mkuu
Ok ahsante kwa mawazo yako mkuu, wanauza kuanzia set moja
 
Kuna kampuni zipo dar unalipia wao wanakuletea mzigo hadi ulipo wanakupa gharama zote kuanzia ununuzi,usafiri, ushuru na nk wao nachukua commission nimeona ofisi zao na mabango km Tatu hivi kariakoo sijawahi huduma hiyo na sijajua usalama wa Pesa Uko VIP.
 
OK nitajaribu kuwatafuta
 
Ok ahsante kwa mawazo yako mkuu, wanauza kuanzia set moja
agiza power tiller kwa supplier anaeaminika.usitume hovyo pesa.
Chagua power tiller yenye nguvu ya kulingana na mahitaji yako.Chagua power tiller ambayo pia utaweza kufunga matairi ya chuma,utaitumia kama water pump,utaitumia kama gari ya mizigo kwa kufunga tela na utaweza pia kuitumia kama generator!
Power tiller yenye uwezo mkubwa tu na vikolombwezo vyote hivyo inaweza kukugharimu usd 1,000 fob,ikifika utalipa 18% ya vat tu
 
Ok nashukuru sana Kwa mchango wako wa mawazo
 
Back
Top Bottom