Gesi yakosa soko: Uzalishaji wazidi Matumizi

Elimu ya Gesi inahitajika sana kwa watanzania.

Kwa uelewa wenu gesi tunayojivunia nayo ni for industrial, home domestic au hospital??

Au yote??

Ipo inatumika? Au ni installation kwanza?

Tuanzie kwanza hapa!!
 
gesi yenyewe juu kama nini, halafu kila kitu dar tu! Wacha tuendelee kutumia mkaa

Mikoani upatikanaji wa gesi hauaminiki. Majuzi baada ya BP kusimamisha shughuli zake, tumebaki na mitungi ambayo hatujui tuipeleke wapi na hivyo tumepata hasara. Walaji nchi hii hatuna haki!
 
Swala gesi ni gumu bila kupata suluhisho la kuweza kushusha bei ya jiko na mitungi ya gesi.Wananchi wa kawaida bado wanalala chini kwa kushindwa kununua vitanda vya bei ya chini,watawezaje kununua jiko la gesi la laki...kifupi demand ya gesi kwa Tanzania iko chini.Wengi wanaitaka na kuipenda lakini hawana uwezo.Na hili bei ishuke bila kuathiri wazalishaji itabidi pato la mwananchi wa kawaida lipande ili watu wengi zaidi wawe na uwezo wa kununua gesi.Otherwise tuendelee na mkaa wetu...

kasome tofauti ya LNG na LPG. inayouzwa mtaani ni LPG, iliyogunduliwa Mtwara ni LNG
 
Tofautisha kati ya gesi ya kupikia aina ya LPG (Liquified Petroleum Gas) ambayo huzalishwa kutokana na mafuta ghafi na mara nyingi huuzwa kwenye mitungi kwa ajili ya kutumia majumbani na gesi asili (natural Gas) ambayo hupatikana chini ya ardhi na hutumika zaidi kuzalisha umeme, matumizi viwandani na ukitaka kutumia majumbani, mara nyingi inabidi uisafirishe kwa mabomba.
 
Hawa watu wapuuzi sana,yaan wanasema mahitaji ya gesi ni kidogo??ahhh acha tu nisije kupewa ban...

Wallah kusingekuwa na bun ningefunguka neno moja tu kwa serikali ya dhaifu angalau hasira yangu ingepungua,hv hii gesi inavyouzwa kwa bei ya anasa hapa mjini ina maana hawaioni?kama kweli wangekuwa wanathamini wananchi kwa nini wasishushe bei kila mtu atumie badala ya mkaa na kuni kunusuru mazingira yetu?ama kweli dhaifu ni dhaifu tuu....
 
Jamani kwani kama gesi hyo ikizalisha umeme mwingi na bei itashuka tu na itatumika kwa watu wengi
Pia ikisambazwa viwandani mbona bidhaa tutapata kwa bei nzuri.
Miundombinu ni lazma sio kwamba tunailaumu serikali ila kumbuka umeme una muda gani na takwimu za watu na maeneo wanayo lakin nn kimefanyika. Nenda katazame reli, bomba la mafuta (TAZAMA) kwa nini tusiseme iwapo walitupiga kwenye madin na utalii hata hivi vyanzo vipya tuache viuwawe kwa sababu tutaonekana watu wa malalamiko?
Historia ni MWALIMU MZURI
 
kasome tofauti ya LNG na LPG. inayouzwa mtaani ni LPG, iliyogunduliwa Mtwara ni LNG

Haya ni mambo ya kemia ya gas, vitu kama calorific value( cv) huangaliwa pia, kama sijakosea hii natural gas iliyogundulika ina carbon moja yaani methane na inayotumika kwa wingi huko mjini kwa kupikia ina carbon zaidi ya moja,mara nyingi huwa ni Butane. Naomba watalaam wa CV watupe shule hapa ili mjadala uwe wa manufaa. Kama nimekosea nisamehewe bure.
 
umenena vyema mkuu, tatizo tumezoea kulaumu na kukosoa tu.

Mtu anashindwa kuelewa hata kuna ujenzi wa bomba kubwa la gesi kutoka mtwara kuja dar.

Mkuu nini kingeanza,kujenga miundo mbinu kama hayo mabomba kwanza au unaanza kuchimba gesi afu ndo unajenga bomba? Natatizika hapo. Nafikiri baada ya utafiti kwamba kuna gesi ya kutosha miundo mbinu ingeanza kuwekwa sawa kuliko ilivofanyika sasa.
 
Nani anaongeahuu *****?!! kama ni nyingi means kuna surplus why isishuke bei basi ili itumike sana tuokoe miti inayoisha kwa uchomaji mkaa!!
 
mkuu Malila amenena vizuri sana kuhusu gesi,ukisoma btn the line utaelewa tofauti kati ya oryx gas na hiyo iliyopo huko mtwara
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nini kingeanza,kujenga miundo mbinu kama hayo mabomba kwanza au unaanza kuchimba gesi afu ndo unajenga bomba? Natatizika hapo. Nafikiri baada ya utafiti kwamba kuna gesi ya kutosha miundo mbinu ingeanza kuwekwa sawa kuliko ilivofanyika sasa.

Mfano mzuri tafiti zimeonyesha kuna mafuta mengi sana ziwa tanganyika utashangaa yanachimbwa halafu miundombinu tutabangaiza sio kuanza sasa.
 
Hapo ndio utakapoona kwamba viongozi na wataalam wetu wanapokosea. Kwanza miundo mbinu kutoka Kigoma kuja sehemu nyingine haiko sawa. Barabara ndo inategemewa kwa sasa na bado haijakamiliza vizuri. Njia ya reli ndio ambayo ni rahisi kusafirisha mizigo in bulk lakn imekufa. Sasa wataanza kuchimba mafuta na gesi halafu jinsi kuipeleka sehemu nyengine ni mgogoro.
 
Hoja nyingine na wachangiaje wengine utadhani hawana ubongo. Mlitegemea serikali ijenge kwanza miundombinu ya kusambaza gesi kabla ya kufahamu kuwa ipo, na ipo wapi na kiwango gani? Haiingii akilini hata kidogo kuanzisha uzi usioweza kujisimamia kama huu.

Sijahi sikia mama hata mmoja anunuaye nguo za mtoto ilihali hata ujauzito hana. Sasa mlitegemea serikali ianze kujenga mabomba ya kusafirisha geni na kuisambaza majumbani pasipokuwa takwimu?

Rafiki yangu nadhani kwa swala hili hulielewi kabisa! Yaani we kwa mawazo yako unadhani kugundua gesi ni sawa na kuokota gesi kama bahati nasibu. Utafiti wa gesi na madini unafanyika kwa miaka mingi na kuna hatua(stages). Unakuwa na miaka mingi ya kujiandaa na kama serikali iko makini inakuwa imekwishaelewa kwa miaka mingi! Hivyo inakuwa na miaka mingi ya kujiandaa. Ila kwa serikali dhaifu ndio hivyo tena! Halafu takwimu ya wingi wa gesi inapatikana hata kabla ya kuanza kuvuna, ndio maana unaambiwa hapa tuna reserve ya gesi kiasi kadhaa na pale kiasi kadhaa..
 
kasome tofauti ya LNG na LPG. inayouzwa mtaani ni LPG, iliyogunduliwa Mtwara ni LNG
Ok.unadhani nini kinakwamisha Hio LNG kufika kwenye market?Hudhani kuwa bado demand iko chini kuweza kujustify wazalishaji kuingilia gharama za kuweka pipelines all over the country hasa ukizingatia jinsi nchi yetu ilivyo kubwa...
 
Haya ni mambo ya kemia ya gas, vitu kama calorific value( cv) huangaliwa pia, kama sijakosea hii natural gas iliyogundulika ina carbon moja yaani methane na inayotumika kwa wingi huko mjini kwa kupikia ina carbon zaidi ya moja,mara nyingi huwa ni Butane. Naomba watalaam wa CV watupe shule hapa ili mjadala uwe wa manufaa. Kama nimekosea nisamehewe bure.

Asante sana Malila uko sahihi kabisa. Ni kweli LPG (liquified petroleum gas) ina calorific value zaidi ya natural gas kwa mbali tu. Sijui kiswahili sahihi cha calorific value lakini tunaweza sema ujoto wake unaotoa ikiungua na oksijeni. Hivyo kwa kifupi moto wa LPG (oryx, mihan, Bp, Lake gas) ni mkali zaidi kuliko natural gas.

Methane
has just a single carbon atom and four hydrogen atoms (CH[SUB]4[/SUB])
Butane
has four carbon atoms and ten hydrogen atoms (C[SUB]4[/SUB]H[SUB]10[/SUB])
Propane
has three carbon atoms chained together with eight hydrogen atoms (C[SUB]3[/SUB]H[SUB]8[/SUB])

Kikubwa nadhani watu wengi hatuna elimu ya gesi au ufahamu japo kidogo. Ni kweli gesi ya oryx, lake gas na mihan zinatoka uarabuni kama mchangiaji hapo juu alivyosema. Zinatoka Uarabuni sababu ni zao la petroleum na huko ndiko inapopatikana. Hivyo kufikia hapa tuondoe notion kichwani kuwa mbona oryx Gas mjini bei juu wakati tunaichimba Mtwara, gesi inakuwa imported na meli kama yalivyo mafuta mengine hivyo mafuta kwenye soko la dunia yakipanda lazima gesi nayo ipande. LPG ni zao la kwanza petroleum inapoingizwa kwenye refinery kuwa heated. Inaanza propane na butane at just 20c then inafuatia petrol, mafuta ya taa, dizeli nk. Mtungi wa gesi ulionao nyumbani ni mchanganyiko wa butane na propane. Kama ni mteja wa oryx unaweza kusoma kwenye kola ya mtungi utaona wamekuandikia all technical details pale. Kama oryx wao butane ni 80% na Propane ni 20% (hapa ikumbukwe propane is more expensive and calorific ndio maana margin yake iko chini kidogo)

Lpg ukiiCompress kwenye mtungi inageuka liquid hivyo safe kusafirisha hata misukosuko inahimili ndio maana tukienda kununua tunanunua kwa kilo. Natural gas ni tofauti kuicompress ni mbinde na haiwezi kuwa total liquid zaidi ya just compressed gas na huwezi kuiweka kwenye mtungi wa chuma wa kawaida tu kama gesi nyingine. Compressed natural gas kwenye cylinder ni bomu tosha. Mtungi wake ni expensive kama utataka uiweke kwenye mtungi maana umetengenezwa kama thermos ya chai, yani several layers kabla ya kufikia kichupa cha gesi yenyewe.. Hivyo natural gas ina changamoto zake vilevile.

Kama mlaji nafurahia uwepo wa gesi asilia ambayo itasambazwa majumbani kwa bei nafuu kama wanavyosema. Lakini kikubwa kwangu ni usalama. Tumejipanga vipi katika suala zima la kuhakikisha kuwa tuko salama na ajali zihusianazo na milipuko ya gesi kama tumeshindwa kujipanga katika miundo mbinu mingine isiyolipuka hapa hapa mjini. Tazama mifuniko ya barabarani inavyoibiwa, nyaya za umeme mchana kweupe, mabomba ya maji yanavyokatwa na watu kujiunganishia, alama za kuonyesha bomba la gesi la sasa linapita nyingi zishaibiwa tayari nenda gerezani watu wanaziyeyusha kutengeneza spacer za magari za aluminium. Je kwenye mabomba ya gesi itakuwaje? Kibaka Athumani ataelewa kuwa hili ni bomba la gesi liko nje nje nisilikate au nilikate niuone mchana...
 
Asante kwa somo lako mkuu umeniongezea uelewa kuhusiana na maswala ya gas.Ni kisimu tu like ingekuhusu.

Kwanini wasingezalisha umeme huko Mtwara mpaka walete bomba mpaka dar hii nchi inatia hasira sana.Gharama zingine ni kwa sababu za siasa tu.

Back
Top Bottom