Gesi yakosa soko: Uzalishaji wazidi Matumizi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gesi yakosa soko: Uzalishaji wazidi Matumizi.

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by babalao 2, Oct 7, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Pamoja na matumaini makubwa ya kupata gesi hapa nchini na kutokuwa na sera madhubuti kuhusu gesi, limeibuka tatizo jingine katika miradi ya gesi nchini. Visima vingi husalisha kiasi kidogo kwani mahitaji ni machache mno.
  Tatizo hilo limekuja kufuatia hazina kubwa kuzidi kuvumbuliwa kila kukicha ilihali matumizi yake hapa nchini yakiwa kidogo.
  Hii imetokana na serikali kushindwa kusambaza gesi hyo katika mikoa mingi hapa nchini. Sasa kumbe kuwa na gesi ni jambo moja na jinsi ya kuitumia ni kitendawili kingine.
  Mchango wako nini tuifanyie gesi yetu tusijechekwa na walimwengu.
  Chanzo: IPPMEDIA.
   
 2. m

  mokti Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani ungeangalia tovuti ya Wizara husika na TPDC ili upate picha ya mipango iliyopo ya kupanua soko la matumizi ya gesi asili nchini. Moja ya miradi mikubwa ambayo imeanza kutekelezwa hivi sasa ni ujenzi wa bomba kubwa lenye kipenyo cha nchi 36 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Karibu
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo ya energy yanataka uwe na sera nzuri za usambazaji na matumizi lakini pia gesi ni substute ya umeme sasa maeneo ambayo hamna umeme lakini uchumi wa watu uko vizuri ni kuhimiza matumizi ya gesi sambamba na kupiga marufuku matumizi ya mkaa na kuni maeneo ya mijini,kushusha bei ya gesi na kuongoza mawakala wa kusambaza hiyo gesi
   
 4. b

  blueray JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo itakuwa ni serikali dhaifu Na mipango dhaifu.

  Gesi ikose matumizi! wakati gesi hiyo inaweza kuzalisha umeme, kuendesha mitambo moja kwa moja viwandani, wananchi kupikia badala ya kuendelea kutumia kuni Na mkaa, kutumia kwenye magari badala ya petroli nk, nk.

  Hebu fikiria bei ya gesi ya kupikia ilivyo ghali mitaani halafu wanatuambia gesi yetu inapotea huko porini haina matumizi! kwa nini wasipakie kwenye mitungu washushe bei, watengeneze majiko mengi ya gesi kwa wingi ya bei nafuu, wawaelimishe wananchi waachane Na kuni?
  Yaani wao gesi kupata matumizi mbaka wazungu waje kuchukua kama wanavyochukua dhahabu?

  pamoja Na udhaifu wao angalau waamke kidogo...
   
 5. salito

  salito JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Hawa watu wapuuzi sana,yaan wanasema mahitaji ya gesi ni kidogo??ahhh acha tu nisije kupewa ban...
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Weka link tukaisome hiyo habari.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  gesi yenyewe juu kama nini, halafu kila kitu dar tu! Wacha tuendelee kutumia mkaa
   
 8. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hoja nyingine na wachangiaje wengine utadhani hawana ubongo. Mlitegemea serikali ijenge kwanza miundombinu ya kusambaza gesi kabla ya kufahamu kuwa ipo, na ipo wapi na kiwango gani? Haiingii akilini hata kidogo kuanzisha uzi usioweza kujisimamia kama huu.

  Sijahi sikia mama hata mmoja anunuaye nguo za mtoto ilihali hata ujauzito hana. Sasa mlitegemea serikali ianze kujenga mabomba ya kusafirisha geni na kuisambaza majumbani pasipokuwa takwimu?
   
 9. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  kwani toka wamegundu gasi inapatikana ni mda gani?
   
 10. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Nimekupata kiongozi ila nafikiri gesi iende sambamba na miundombinu yake mpaka kwa mlaji kwani hiyo ni biashara si huduma ya bure.
  Hata shirika la ndege wana mipango mikubwa kuliko KLM AU EMIRATES kwenye tofuti zao lakini utekelezaji tunaujua wote
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nikuulize wewe kwanini leo tunajenga bomba la kipenjo cha 35 sasa na sio katika mradi uliopita ambao sasa ndio unaotumika kufua umeme hapa Dar? Uvumbuzi wa gesi umeendelea taratabu na sasa maeneo mengi zaidi yameendelea kugundulika kuwa na gesi na ndio ineyotengeneza mazingira ya kuwa na wigo mpana zaidi wa matumizi.

  Kwanini mpaka leo tunatumia gesi ya Oryx kutoka Arabuni wakati gesi inapatikana nchini?
   
 12. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Kumbe tuna gesi nyingi mpaka inakosa soko, sasa tunagombea nini na Malawi si wamuachie tu na yeye ya ziwa Nyasa?
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Miradi kama hiui nayo inasababisha kuzidi kuturudisha nyuma kwa kuongeza gharama zisizo na msingi. Kwa nini kutilia mkazo kwenye ujenzi wa biomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar wakati tunaweza kuanza na kuzalisha umeme palepale Mtwara na kuusafirisha sehemu nyingine. Kama ni bomba la kuleta gesi Dar kwa ajili ya matumizi mengine ni mradi ambao ungetrekelezwa baadaye wakati huo tukiwa na uhakika kuwa gesi hiyo imeshaanza kutumika.
  Pale Mtwara tunaweza kutafuta wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji na kuhakikisha gesi inatumika vema.
   
 14. Lonestriker

  Lonestriker JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Swala gesi ni gumu bila kupata suluhisho la kuweza kushusha bei ya jiko na mitungi ya gesi.Wananchi wa kawaida bado wanalala chini kwa kushindwa kununua vitanda vya bei ya chini,watawezaje kununua jiko la gesi la laki...kifupi demand ya gesi kwa Tanzania iko chini.Wengi wanaitaka na kuipenda lakini hawana uwezo.Na hili bei ishuke bila kuathiri wazalishaji itabidi pato la mwananchi wa kawaida lipande ili watu wengi zaidi wawe na uwezo wa kununua gesi.Otherwise tuendelee na mkaa wetu...
   
 15. peri

  peri JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  umenena vyema mkuu, tatizo tumezoea kulaumu na kukosoa tu.

  Mtu anashindwa kuelewa hata kuna ujenzi wa bomba kubwa la gesi kutoka mtwara kuja dar.
   
 16. N

  Njele JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mipango duni ya serikali yetu kuwa kwenye makarabasha bila kuwafikiwa wananchi.

  Ubunifu wa soko la ndani badala ya kuanza kwa kupunguza bei ili kuwavutia wananchi watumiaji, serikali inapunguza mshiko wa wawekezaji toka nje kwa kufutia kodi, je, hawa wawekezaji wa kutoka nje ndio watakao nunua gas?

  Tuna bahati ya kuwa na bidhaa adimu muhimu kwa matumizi ya binadamu, kwani kuna mataifa yanayotuzunguka na mengineyo yamekosa bidhaa hiyo, kwa nini tusitafute soko la export gas hiyo ili kuliingizia taifa pesa na kusaidia kuiingiza tanzania kwenye medani ya ushindani wa kibiashara?
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  samahani kidogo. Najua kwa maelezo yako nami nimo. Nawe kwa ubongo wako uliokamilika unadhani kwa nini matumizi yako chini ya kiwango cha uzalishaji wa sasa?
   
 18. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  ueleweki upo upande gani mkuu...haya yote ni matokea ya serikali dhaifu ya ccm,kuna watu wangap stili wapo huko inapozalishwa na bado wanatumia mkaa na kuni? Mipango dhaifu ya serikali ndo inayolete hapa...kwanini walikimbilia kuchimba while hawajajipanga...?
   
 19. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tushazoea kibongo bongo, tukineemeshwa na kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!
   
 20. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Heee hii mupya, kumbe gesi ya Oryx inatoka uarabuni?
   
Loading...