sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Nachukua fursa kumshukuru Mungu kwa uwezo wake Karima kutuamsha na kutuwezesha kupumua kwani ni wengi wetu hawajapata fursa hii adhimu,pia ni waombe dua njema kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa neema watu wa Mtwara ili aweze kuwajalia siha njema na kuzirehemu roho za waliotangulia mbele ya haki kwa kudai/kupigania neema waliyojaliwa na Mungu kwa minajili ya kuwanufaisha kwanza Mtwara na kisha taifa kwa umoja wake.
Baada ya dua hii hapo juu,nitumie fursa hii kuwashirikisha Watanzania wenzangu na kulitafakari jambo hili kwa kina kutokana na chuki iliyo ndani ya wana wa Mtwara na watendaji wa vyombo vya dola katika kadhia nzima.Jambo hili halikustahili nguvu kubwa ambayo mwisho wa siku busara imekosa mkondo wake.Anguko hili la hekima dhidi ya kupigania haki za wananchi limepelekea damu za wasio na hatia kumwagika na kuwatia umasikini mkubwa wakazi wa maeneo hayo na vitongoji vyake.
Nini tufanye kuondoa kutu inayojijenga miongoni mwa Watanzania kutokana na kadhia hiyo,kutumia nguvu kubwa kunakofanywa na serikali kuhakikisha ina kata mapembe ya wanaoitwa wachochezi ni aina nyingine ya mgogoro ambao serikali ama kwa kupungukiwa umakini au kwa makusudi inaenda kuupandikiza kwa kiwango kikubwa mgogoro ambao utazua kuviziana kati ya askari na raia.Kauli hizi ambazo tayari ni mwiba kwa wanafamilia wa Mtwara ambazo miongoni mwao wamemwaga damu zitasababisha kuwa chachu ya ugomvi na matukio mbalimbali ya kustukiza ambayo yataigharimu serikali yetu sikivu.
Kwa maoni yangu mediation katika ya wana wa Mtwara na serikali ni kukaa meza moja na kufuta tofauti zao kwa makubaliano yenye kujenga bila kutaka kuukomoa upande mmoja,lakini hali hii ikiachiwa kama ilivyo itabidi serikali itangaze hali ya hatari ambayo mwisho wa siku wananchi na nchi nzima wataikata serikali yao sikivu kwa njia mbadala mbali na sanduku la kura.
Watanzania wenzangu,Tanzania ni yetu sote,tulijadili kwa kina nini cha kufanya ili kuondoa vita vingine ambavyo vitakuwa si vya gesi tena bali ni kulipiziana kisasi kutokana na uhanga wa vita vya gesi ambavyo vinaweza kuzalisha civil war ambayo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu.Niwaombeeni sana wanajamvi tuliangalie kwa umakini hili,nawakilisha Mungu ibariki Tanzania na watu wake