JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Akizungumza katika mahojiano na Kituo cha UTV, leo Jumatatu Oktoba 13, 2025, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa anasema:
‘Watanzania wawe na amani, kila kitu kitu kinaenda swa, Oktoba 29 waende wakapige kura, kwa sasa wasikilize wagombea ili ikifika siku hiyo wakafanye maamuzi sahihi.’
Kuhusu maandamano
Anasema hakuna Mtanzania anayeweza kufanya hivyo kinyume na utaratibu.
Katiba inaeleza kuhusu haki ya kufanya maandamano, kama mnasisitiza watu watumie haki yao kupiga kura, kwanini mnazuia haki ya kuadamana?
“Serikali haijazuia haki ya Mwananchi, mkitaka kuandamana kukusanyika upo utaratibu wa kufuata na kuzingatia.
“Vyombo vya Usalama vinawajibu wa kuangalia lengo la mkusanyiko ni lipi? Kama kuna nia mbaya basi hawataruhusu hilo.
“Unapokuja na hoja ya kuwa utazuia uchaguzi unategemea Serikali iache na iruhusu hilo? Ni jukumu la Serikali kuwahakikishia taifa lipo salama.
“Jukumu la kwanza na la msingi la Serikali ni kuhakikisha Watu wanapata haki zao na Taifa linakuwa salama.”