Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Niliwahi kuamini kuwa Gerson Msigwa ni Mtu makini sana na ana hofu ya Mungu, kumbe sio nilivyofikiri.
Gerson Siasa za kuendelea kupata madaraka katika serikali zimekufanya usahau ulipotoka, tatizo nini nyie wenzetu ambao mpo huko mnatuongoza?
Ni kweli kabisa hamfahamu maisha halisi ya watanzania? Kuweni na huruma
Kwa nguvu na ulazima mmeweka hizo tozo na kuhakikisha hilo linaendelea unasema kabisa kuwa hiyo ni sheria haibadiliki.
Gerson ni kweli ndugu zako wote wana maisha mazuri kiasi kwamba haya mabadiliko hayawaumizi? Wenzetu nyie mtakaa na hivi vyeo milele?
Leo umelinganisha maisha ya watu wa ulaya na watanzania, tena unasema kabisa hata ulaya bando ghali hivyo watu waache kulalamika.
Gerson ni kweli wastani wa kipato cha mtu wa ulaya ni sawa na cha watanzania huku? Hili hulifahamu au siasa za madaraka zimekufanya uwe hivi?
Bado nipo katika mshangao kuona mtu Kama wewe unashindwa kujua hali halisi ya maisha ya mtanzania na maisha ya watu wa huko ulaya.
Gerson naomba msiwe na hizi dharau, haya maisha ni ya kupita tu
Mkiwa na nafasi kubwa huko serikalini wafikirieni na ambao hawana kitu na ambao ndio idadi kubwa ya watanzania.