Gereza lina umuhimu gani katika harakati za uhuru na ukombozi?

Sep 5, 2018
86
132
Ameandika Pro Sarara

Ni sikieni enyi wapigania haki na Mabadiliko wa Tanzania. Nisikieni enyi Vijana na wazee wenye Shauku ya haki na maendeleo, Nisikilizeni enyi waume na wake mnaolia machozi ya Damu ndani ya Mioyo yenu Mkiisubiri Nchi ya Ahadi.

Sikieni kwakuwa Hii sio Busara yangu Nami nimeiba kutoka kwa wazee wetu walioteseka wakipigania uhuru wa Bara Letu na Nchi zetu, Waliouwawa wakiipigania Afrika huru ambayo Muafrika angeishi kwa uhuru katika Ardhi yake na kwa uhuru angeiendeleza Nchi yake.

Gereza ni paradiso ya Mpigania Haki, Naam Gereza ni Nyumba ya Ibada, Gereza ni Msalaba wa ukumbozi Kama ule wa wakristo , Gereza ni Msikiti ambao tunakutana na Kutafakari Mustakabali wa Nchi yetu.

Mandela anasema, "No one Truly knows the Nation until one has been inside its Jail"

Gereza ni Chimbuka la Fikra mujaruba kwaajili ya Mabadiliko, Wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walitumia Gereza kufundishana Historia ya Nchi yao, Wakafundishana historia ya Vyama vyao, Elimu ya Siasa na Uchumi.

Gereza ni Chombo cha kuwaunganisha wapigania Uhuru, Gereza huondoa ukabila, Udini, Ukanda, na Uvyeo Ndani ya Gereza Wapigania haki hujengwa kuwa kitu kimoja na kusahau tofauti zao.

Gereza ni Roho mtakatifu wa Mungu Mwenye kuimarisha imani na Mioyo juu ya mabadiliko gereza huondoa ulegelege wa mwanamapinduzi, Gereza huimarisha akili na Roho, Gereza ni tanuri la moto Linalosafisha dhahabu(Mpigania haki)

Gereza ni kielelezo cha Umaana na umuhimu wa kile tunachopigania, kwakuwa Gereza ni kielelezo kwamba Mapambano yetu yamesikika na Ujumbe wetu umeingia mioyoni mwa watesi wetu.

Gereza Ni Shule ya Uongozi.kama wasemavyo wahenga kwamba "A nation Should not be Judged by how it treats its highest citizens but its lowest ones" katika Gereza ndiko Kiongozi mzuri hufuliwa naam ni katika Gereza ndipo Kiongozi anapata wasaa wa kuijua Nchi yake.

Gereza halitutenganishi na Familia zetu La hasha bali gereza hutuunganisha zaidi na familia na Ndugu zetu katika mageuzi, Ndugu zetu katika ukombozi Hii ndio familia ya Mpigania haki.

Nalipenda Gereza.
Gereza la Mandela
Gereza la Mugabe
Gereza la Nyerere
Gereza la Samora Machel
Gereza la Nkrumah
Gereza la Augustino Neto
Gereza la Sedar Senghor
Gereza la Walter Sisulu
Gereza la Freeman Mbowe.

Gereza ndio uhuru wetu, Gereza ni Nyumba ya Ibada karibu Gerezani for out of biterness comes freedom and equality.
 
Back
Top Bottom