Gereji na oil nzuri kwa Nissan Dualis

Kuna fundi mmoja mtaalam sana wa magari alinishauri kitu akaniambia achana na hizi nissan,akanisistiza endelea na toyota ukichoka hamia kwenye European Car.

Nimeandika kama kibwagizo,gereji nzuri ni pale kwa jerry mikocheni kama unaelekea kairuki hosp,ukifika wao wataikagua gari ni kukwambia nini kinatakiwa kubadilisha
Alikudanganya. Shida yake ni hazijui hizi gari so anaziogopa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Nissan Dualis tumia oil ya Castro 5W~40, maji ya wiper usitumie yenye chlorine ya DAWASA, yanaweka punjepunje fulani nyeupe baadae inafanya tundu za wiper zizibe, tumia maji ya chupa atlist kwa mwaka 1 bajeti ikibana rudi na maji ya dawasco
Hii unaua injini
 
nenda total sheli.
Tanzania hakuna Sheli, haya majina yanapendwa kutumiwa na watu wa mikoa ya Kaskazini sababu miaka ya nyuma kulikuwepo na vituo vya mafuta vya kampuni ya Shell, inawezekana wakati huo ndio vilivyokuwa vingi sasa watu wamezoea kituo chochote cha mafuta hata kama ni Total, Puma, Oryx wanaviita Sheli.
 
Kuna fundi mmoja mtaalam sana wa magari alinishauri kitu akaniambia achana na hizi nissan,akanisistiza endelea na toyota ukichoka hamia kwenye European Car.

Nimeandika kama kibwagizo,gereji nzuri ni pale kwa jerry mikocheni kama unaelekea kairuki hosp,ukifika wao wataikagua gari ni kukwambia nini kinatakiwa kubadilisha
Hao mafundi wa chini ya mwembe hachana nao.

Fundi unakuta ameishia darasa sijui la 7 alafu unakwenda kwake kupata ushauri, inasikitisha sana@
 
Tafuta Manual ya hiyo gari ujue nini kimekuwa recomended kuweka.
Umempa ushauri mzuri sana.

Mimi kabla ya kununua gari natafuta Manual yake kwenye mtandao nasoma alafu ndio naagiza gari.

Watanzania tuwe na tabia ya kusoma hizi Instruction Manuals ya vitu tunavyo vinunua kama Magari, TV, Music System. Fridge, nk.
 
Kwa Nissan Dualis tumia oil ya Castro 5W~40, maji ya wiper usitumie yenye chlorine ya DAWASA, yanaweka punjepunje fulani nyeupe baadae inafanya tundu za wiper zizibe, tumia maji ya chupa atlist kwa mwaka 1 bajeti ikibana rudi na maji ya dawasco
Sio kweli.

Kwenye wipers natumia maji ya bombani nachanga na zile sabuni za kuoshea glass na wala matundu hayajawahi kuziba.
 
Gari haijaharibika garege ya nini? Miye napeleka pale Total last time 85k walibadili kila kitu hadi upepo waliongeza na kikaratasi juu mwisho lini niliweka Km5000
 
Gari haijaharibika garege ya nini? Miye napeleka pale Total last time 85k walibadili kila kitu hadi upepo waliongeza na kikaratasi juu mwisho lini niliweka Km5000

Kwanini wamekuwekea km 5,000?

Kama hujui basi pitia hii thread utapata uelewa wa aina za oil.

Thread 'Zifahamu Engine oil' Zifahamu Engine oil
 
Nipe ujuzi mkuu, miye sina uelewa wa hayo magri na oil, nilienda pale kwa ajili ya servise nikapewa km za oil na bei zake nikavhukua hiyo
Huo uzi hapo juu upitie utapata shule nzuri sana, mfano hii ni kwenye post #13 ya hiyo thread.

Screenshot_20220830-175236_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom