Gereji gani nzuri na nafuu kufanya service ya gari DAR

blackhawk

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
262
573
Habari,

Hapa majuzi Mungu amenipa baraka katika shughuli zangu nimepata chochote kitu ambacho kilitosha kununua gari ndogo ya matumizi yangu binafsi familia na kazi zangu

Nimenunua gari yangu ya kwanza Toyota Raum kutoka yard ya Jan Japan international nishaichukua ila sinaifanyia service yoyote maana sina uelewa sana wa magari

Naomba kwa yoyote aniambie garage gani nzuri na affordable kwa hapa Dar es salaam kwa mimi ambaye sijui sana magari

Pia nahitaji kui modify kama kubadili tyres na kufunga sport rim , muziki na lights nzuri

Nawasilisha
 
Huna haja hata ya kwenda garage cha kwanza kamwage oil incase itakuwa imeshakatika isije kuharibu components za engine. Maana gari za Yard zinakaaga mda mrefu sana parking.
Mkuu unasema tu ...ila gari jipya na la kwanza weeeeeh

Japo ushauri wako ni mzuri na unakomboa gharama
 
Mkuu unasema tu ...ila gari jipya na la kwanza weeeeeh

Japo ushauri wako ni mzuri na unakomboa gharama
Yeah mkuu service muhimu ni ya engine tu. Maana ikifa hio ni msiba. Kuna jamaa aliagiza gari kupitia kampuni ya sbt. Kaletewa na kukabidhiwa kumbe ile gari haina oil. Kapiga misele day 1 kidogo akapaki!

Day 2 akapiga misele nayo parefu baada ya muda anaskia kama harufu ya plastic inaungua inaingia ndani ya cabin. Kupaki akafungue bonet aone nini shida. Kucheki coolant ipo, Akachomoa dipstick loh, kuicheki ni kavu kama vile spoku ya baskeli mpya. Kumbe chombo haina oil hata tone bana.

Ndio kuagiza oil ikaletwa na kuwekwa. Ila angeparangana aendelee kuiburuz ilikuwa inapiga Knock ya hatari.

Sasa imagine bei ya 1KR engine ni sh. ngapi ingemtoka. Na ndo gari ya kwanza kaunga unga vihela kanunua.
 
Yeah mkuu service muhimu ni ya engine tu. Maana ikifa hio ni msiba. Kuna jamaa aliagiza gari kupitia kampuni ya sbt. Kaletewa na kukabidhiwa kumbe ile gari haina oil. Kapiga misele day 1 kidogo akapaki!..
Oil muhim mkuu ...Muhim tena ili awe na aman amwage zote engine na gear box ili asiwe na mashaka
Hicho kisa ulichosimuliaa kina mengi ya kujifunza.

Hata coolant nayo ni muhim sana kuchek kuona kama iko ok japo toyota angalau ila kitu nissan coolant sio ya kucheza nayo kabisa
 
Mkuu unasema tu ...ila gari jipya na la kwanza weeeeeh

Japo ushauri wako ni mzuri na unakomboa gharama
Sasa ndio ukweli.. Kitu cha kwanza ni kumwaga oil... Labda na kukagua kidogo kwenye engine kama kuna sehemu inavujisha ili kama unaipeleka gari mbali isikusumbue njiani
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom