PostGE2025 George: Nilipigwa risasi Oktoba 29, 2025 nikapoteza mguu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
"Nilikataa kukatwa mguu, lakini madaktari waliniambia nimechelewa kupata matibabu." Huo ni ushuhuda wa kusikitisha wa George Chipeta (24), fundi wa umeme wa magari mkazi wa Banana, mkoani Dar es Salaam aliyetoa maelezo mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025.

George, ambaye sasa analazimika kuishi bila mguu wake wa kulia, ameiambia Tume jana, Januari 19, 2026, kuwa alipigwa risasi na askari polisi mchana wa tarehe 29 Oktoba akiwa katika shughuli zake za kutafuta vipuri (spare parts) maeneo ya Vingunguti.

Siku ya tukio, George alikuwa ametoka ofisini kwake Banana kuelekea Tabata kununua booster ya gari. Wakati akirudi kwa kutumia pikipiki yake kupitia njia ya Vingunguti, alikutana na kundi la watu wapatao 50 hadi 70 wakikimbizana na gari la polisi (Defender). Amesema alipatwa na hofu akageuza pikipiki ili aondoke. Wakati anageuza, ndipo akapigwa risasi ya paja kutokea nyuma iliyokata mishipa ya damu.
 
Likitoka Ganda kwenye Risasi chuma kinachobaki kuingia ni kidogo sana lakini matusi/Athari kinayofanya ni makubwa, na hiyo ni silaha ndogo tu za kivita zile SMG 56.. Nilishangaa zaidi kumuona Askari amebeba na LMG ule ni ukatili usiojadilika.
 
Likitoka Ganda kwenye Risasi chuma kinachobaki kuingia ni kidogo sana lakini matusi/Athari kinayofanya ni makubwa, na ni silaha ndogo tu za kivita zile 56.. Nilishangaa zaida kumuona Askari amebeba na LMG ule ni ukatili usiojadilika.

Kasi ya ufyatuaji risasi ya LMG (Light Machine Gun) inatofautiana lakini kwa kawaida inafyatua risasi 6 hadi 25 kwa sekunde, au raundi 360 hadi 1500+ kwa dakika (RPM).

Kwanini utumie silaha kama hizi kama hujakusudia kuua maelfu kwa maelfu ya wananchi?
 
"Nilikataa kukatwa mguu, lakini madaktari waliniambia nimechelewa kupata matibabu." Huo ni ushuhuda wa kusikitisha wa George Chipeta (24), fundi wa umeme wa magari mkazi wa Banana, mkoani Dar es Salaam aliyetoa maelezo mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025.

George, ambaye sasa analazimika kuishi bila mguu wake wa kulia, ameiambia Tume jana, Januari 19, 2026, kuwa alipigwa risasi na askari polisi mchana wa tarehe 29 Oktoba akiwa katika shughuli zake za kutafuta vipuri (spare parts) maeneo ya Vingunguti.

Siku ya tukio, George alikuwa ametoka ofisini kwake Banana kuelekea Tabata kununua booster ya gari. Wakati akirudi kwa kutumia pikipiki yake kupitia njia ya Vingunguti, alikutana na kundi la watu wapatao 50 hadi 70 wakikimbizana na gari la polisi (Defender). Amesema alipatwa na hofu akageuza pikipiki ili aondoke. Wakati anageuza, ndipo akapigwa risasi ya paja kutokea nyuma iliyokata mishipa ya damu.
Dah inauma sana
 
ila Igp angekuwa muungwana angejiudhulu kwa haya yaliyotokea
 
Kasi ya ufyatuaji risasi ya LMG (Light Machine Gun) inatofautiana lakini kwa kawaida inafyatua risasi 6 hadi 25 kwa sekunde, au raundi 360 hadi 1500+ kwa dakika (RPM).

Kwanini utumie silaha kama hizi kama hujakusudia kuua maelfu kwa maelfu ya wananchi?
Bila shaka hz ndo zilibonda vichwa vya waliofarik,nilishindwa kuelewa ule ulengaji wa kichwa tu,
 
Kwamba risas 6 kwa sekunde sio mchezo
Yep ukiiweka kwenye mfumo wa automatic. Sijui walifikiria nini?

Hii tume uchwara ya Chande ilitakiwa kuuliza maswali kama haya kwanini silaha kama hizi zilitumika, nani alitoa ruhusa, kuandaa hii mipango na utekelezaji.

Nani anaficha miili ya maiti, nani amegoma kutoa maiti za waliowaua kuzikwa na wapendwa wao, nani anatoa amri kuendeleza vitendo vya utekaji, kutupa watu magereza bila kufuata taratibu.

Kwanini Simbachwene amezuiliwa kufanya genuine reforms kwenye jeshi la polisi?
 
Back
Top Bottom