George Floyd kuzikwa leo Juni 9, jijini Houston

George Floyd kuzikwa leo Juni 9, jijini Houston

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki dunia mikononi mwa polisi kimekuwa ishara tosha ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani na kwingineko ulimwenguni.

George Floyd anazikwa Jumanne wiki hii huko Houston, jiji ambalo alikulia na kwa muda mrefu alikuwa ni mtu mkarimu kwa wakazi wa mji na mcheshi kwa kila mtu, watu walioishi pamoja wamesema.

Kifo cha George Floyd kilizusha maandamano makubwa katika miji mbalimbali nchini Marekani na nje ya nchi hiyo, hususan barani Ulaya.

George Floyd, mwenye umri wa miaka 46, ambaye alikuwa anapima urefu wa karibu mita mbili na baba wa watoto watatu alikuwa anachukuliwa na ndugu zake kama mtu "mpole" ambaye alihubiri amani na upendo, huku akitia mbelr michezo na upendo wa Mungu.

Mama yake alihamia Houston mara tu baada ya kuzaliwa George Floyd huko North Carolina mwaka 1973. Alilelewa katika eneo la "Third Ward", kitongoji cha watu weusi na maskini kinachopatikana katikati mwa jiji kubwa la Texas.

"Kwa kweli hatukuwa na mengi, lakini tulikuwepo kwa kila mmoja," binamu yake Shareeduh Tate amesema wakati waibada ya kuaga mwili wake huko Minneapolis wiki iliyopita.

Mwalimu wake wa zamani, Waynel Sexton, aameliambia shirika la habari la AFP kwamba baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, alitaka kuwa "jaji wa Mahakama Kuu".

Kwenye Shule ya Upili ya Jack Yates, alikuwa na kipaji cha kupendwa na kila mtu katika eneo lake. "Alifundisha vijana jinsi ya kuishi na watu kwa sababu alikuwa aliona mengi wakati wa ujana wake," alisema kaka yake mdogo, Philonise Floyd, wakati wa ibada ya kuaga mwili wake.
 
Kazi kuhangaikia visivyowahusu wakati hata hawawasikilizi wala kujali lolote from blacks living in Africa.
.
bro serikali yako inaruhusu watu wanapigwa risasi na wengine kushambuliwa makao makuu ya nchi mmebung'aa tu yakitokea kwingine mnapapatika ujinga kabisa
 
Kazi kuhangaikia visivyowahusu wakati hata hawawasikilizi wala kujali lolote from blacks living in Africa.
.
bro serikali yako inaruhusu watu wanapigwa risasi na wengine kushambuliwa makao makuu ya nchi mmebung'aa tu yakitokea kwingine mnapapatika ujinga kabisa
Mbona wanafuatilia kuhusu Makonda, Lissu na sasa Mbowe?
 
Black race matter.
R.I.P MARCUS MOSIAH GAVEY.
 
Unafatilia ubalozi wao sio raia wao!
Tanzania miraia mimbea mbea tu kazi kushupalia yasiyowahusu
Hivi hoja yako ni ipi? Kwamba raia wao hawafuatilii habari za kimataifa au wanafuatilia habari za kimataifa ila hawafuatilii habari za waafrika?
 
Back
Top Bottom