Gen. Ndomba amrithi Shimbo

Status
Not open for further replies.
MANENO ya kuokoteza hayana mpango mzee shimbo alikuwa mtu muadilifu sana jeshini, kosa lake kubwa aliwabana walaji ndio ikawa chuki kubwa dhidi yake, hata Ndomba NI MTU MUADILU SANA kaondoka kule JKT jamaa wanashangilia kwa sababu aliwabana sana walaji.
 
Wakurya basi tena. Major General Ryoba ndiye kapelekwa ofisi ya Waziri Mkuu?
 

sasa kama alikuwa muadilifu, matrilioni ya south na hela za askari waliokuwa UN yalitoka wapi? pia sijawahi sikia akikanusha au kutoa maelezo. labda utupe ufafanuzi zaidi
 
Asante kwa elimu hii. Hata mimi nilikuwa najiuliza juu ya haya mambo.
 
Hongera yake, huyu Samuel Ndomba alishawahi kuwa mkuu wangu wa wilaya. Na sasa mtoto wake Allan ni mwanasheria wetu dah!

siyo wilaya mkuu alikuwa mkuu wa mkoa wa Arusha kabla hajarudishwa tena jeshini na JK kuwa Chief of Personnel
 
Haya sasa mbona kimyaaa! Sijasikia la udini? Hii ina re assure imani yangu - pamoja na mapungufu kibao iliyonayo mkulu, sio mdini! Cheki wakuu wa TRA,PCCB, JWTZ, BoT, TSAF, P/Minister, Finance Minister, etc.

Hapoo hahihitajiki Madrasa
 
..hivi inawezekana kweli Chief of Staff wa JWTZ aibe tri 3 bila kuwashirikisha Amiri Jeshi Mkuu, Waziri wa Ulinzi, na Mkuu wa Majeshi??

..inaelekea waTanzania bado hatujajifunza kutokana na kesi za Mahalu na Mramba.
 
sasa kama alikuwa muadilifu, matrilioni ya south na hela za askari waliokuwa UN yalitoka wapi? pia sijawahi sikia akikanusha au kutoa maelezo. labda utupe ufafanuzi zaidi

ulikua unataka kila umbeya atakaosikia autolee maelezo basi angekua hana kazi ya kufanya maana nchi hii kuzushiana hakuishi na dawa yao kuwachunia waongee mpaka midomo iwaume
 
Nawasalimu wakuu,
Nimezungumza na mdau mmoja toka idara nyeti nchi hii na mmoja wa maafisa waandamizi wa JWTZ ambao kila mmoja kwa wakati wake amenieleza uteuzi wa mnadhimu mkuu wa JWTZ kwa kada wa CCM ambae ametunukiwa Luteni Jenerali ndg Ndomba ni maandalizi ya CCM kugoma kukabidhi madaraka.

Hoja yao ni:-
Kushinda katika sanduku la kura sio kigezo pekee cha kupewa nchi lazima idara ya usalama wa taifa na JWTZ wakubaliane na ushindi huo kwa kuwa dakika ya mwisho ndio unakuwa mnadhimu mkuu wa vyombo vyote. Kwa kulitambua hili CCM imeamua kumpa nafasi hiyo kada wake Ndomba ili ikishindwa katika sanduku la Kura Ndomba and the likes waongoze uasi wa kukabidhi nchi kwa chama kingine.

Ikumbukwe Ndomba miaka mitano nyuma alikuwa Luteni Kanali na alikuwa mkuu wa wilaya baade mkuu wa mkoa ambaye kwa nafasi hizo ni mjumbe wa wa kamati ya siasa za chama mkoa na wilaya, nafasi ya ukuu wa mkoa na wilaya zimethibitishwa hivi karibuni bungeni na Mh waziri mkuu ni kuwa nafasi za makada ili waendelee kuilinda serikali ya CCM.

Wanahoji unadhani kwa mtu aliyepanda ghafla kwa ranks kubwa hivyo na kuna wenzake wanasota years and years, kwa ukada wake wa dhahiri kwa CCM atakubali kumpigia saluti rais toka nje ya CCM?

Lipumba, Slaa and the teams wake up
 
Hili halina ubishi. ukiwa kiongozi ni lazima uone mbali. JK ni mwanajeshi na amepata urais akiwa kanali, sasa anajua mbinu zote za kijeshi ktk kuhakikisha rais anashinda! Hakuna jinsi, ccm lazima ishinde 2015.
 
Hayo ndio yafanyikayo katika nchii iliokosa waledi wa demokrasia kwa ajili ya kulindana. Sishangai matokeo yakawa tofauti na wananchi wengi wapenda mabadiliko nchini mwetu na jinsi tutarajiavyo 2015. Harufu ya machafuko inaanza kuvuma taratibu upande wa Tanzania.
 
..hivi inawezekana kweli Chief of Staff wa JWTZ aibe tri 3 bila kuwashirikisha Amiri Jeshi Mkuu, Waziri wa Ulinzi, na Mkuu wa Majeshi??

..inaelekea waTanzania bado hatujajifunza kutokana na kesi za Mahalu na Mramba.
Ndiyo inawezakana kama walikuwa kambi moja na ba mwanaasha!! kwani hukumbi Mramba alikuwa kambi tofauti na huyo dhaifu bin visasi wenu?
 
Duh! Nchi Hii Inamambo Mazito Sana
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…