Gem Slaves: Tanzanite's child labour - Newest mapanki

Invisible

JF Admin
Feb 26, 2006
16,285
8,340
Gem-Slaves-logo.jpg
Mererani in northern Tanzania is the only place on earth where the precious stone tanzanite is mined. Although the industry is worth $300 million a year, the town's residents live in desperate poverty, with children bearing the heaviest load. Every day thousands risk their lives in poorly constructed mine shafts for barely a meal a day. Despite efforts to curb this deadly practice, the global thirst for tanzanite continues to drive these children underground.


[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]IRIN Films - Documentaries for an International Audience[/FONT]

real.gif
Realplayer
mediaplayer.jpg
Windows Media player (15:26 min)


HII ITAKUWA MAPANKI THE SECOND. KWASABABU NAJUA JK ATAMBIWA UONGO TENA AJE KUPAYUKA

LAKINI MIMI NAONA KILICHOMO HUMO NI UKWELI MTUPI. JE WEWE UNASEMAJE?
 
Admin,

Nina imani kwa kuwa uko karibu na hao jamaa huko, watakuwa wamepata ujumbe
 
Filamu ya Mapanki, kwa maoni yangu, inaonekana kuwa na ukweli kidogo na chumvi nyingi. Sasa kwa filamu ambayo inatakiwa iwe si ya kubuni bali mambo halisi (non-fiction), nadhani hii si sawa hata kidogo. Nachelea kusema kuwa baadhi ya madai ya kuhusika kwa serikali yetu kuwasaidia "waasi" katika hizi nchi za Maziwa Makuu katika kuwafikishia silaha yanaweza kuwa ya kukisia (speculative). Kwa nini, kwa mfano, isichukuliwe kuwa hizo silaha zilikuwa kwa matumizi ya majeshi ya nchi husika?

Mfano mwingine wa "chumvi nyingi" ni madai kuwa Watanzania na hususan wakazi wa Mwanza hawanufaiki na biashara ya samaki. Ni wazi kuwa katika mfumo wa uchumi unaotawala dunia ya utandawazi baadhi ya watu watanufaika na wengine wataumia; huu ndiyo ukweli. Mwanza naifahamu vizuri, na siamini kama kuna watu wanakula samaki wenye kutoa funza eti kutokana na uhaba wa samaki! Huko ndiyo kuzidisha chumvi. Wazungu wanasema "fiction thrives on exaggeration" na ndiyo maana filamu hii, kwa kiasi kikubwa, inakosa sifa ya kuwa non-fiction!

Kwa mantiki hiyo, mtu unaweza kupata shaka kuhusu nia ya kuandaa filamu ya
documentary yenye mwelekeo au upendeleo fulani. Ikumbukwe pia japo filamu ilitengenezwa siku kadhaa zilizopita ni miezi michache tu iliyopita ambapo ilionyeshwa kwenye televisheni Uingereza. Tujiulize, kwa nini ionyeshwe wakati huo? Unaamini katika "coincidence"?

Hii filamu ya Mererani (sipendi hata kutumia jina lake!) nayo tunasikia itaonyeshwa hapo New York (UN) wakati huu. Ieleweke kuwa JK naye atakuwa hapo hivi karibuni. Na sentesi ya mwisho wa filamu hii ni swali kwa rais! Bila shaka waandishi wa habari watatumia swali hilo hilo pia kumuuliza JK.

Tanzania kuna ofisi za ILO-IPEC, lakini afisa wa ILO aliyeongea katika filamu hiyo yuko Kenya. Labda pia ni "coincidence" na si kitu sana! Kwani sote tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na tunapendana!!

Ili kuzidi kujifikirisha tujiulize baadhi ya maswali, kama vile:
Nani anafaidika na nani anaathirika na filamu hii?
Je, filamu hii inaweza kuathiri biashara ya tanzanite?
Watakaoathirika ni wachimbaji wadogo wazawa, au wachimbaji wakubwa (soma AFGEM/TanzaniteOne)?
Madhara ya filamu hii kwa taifa ni zaidi kwa uchumi (economic) au sifa/rekodi ya Tanzania kuhusu haki za watoto na binadamu kwa ujumla (human rights)?
Filamu inasaidia vipi kutatua umaskini wa Tanzania au inaishia tu kuonyesha athari za umaskini na utandawazi (soma utandawizi)?
Je filamu ina uhusiano wowote na yale yalijadiliwa humu ndani (barazani), mintarafu "Kampeni na ahadi za CCM/JK huko Mererani wakati wa Uchaguzi"?
Je, filamu hii ina uhusiano na njama za kuangusha biashara ya tanzanite, kama ilivyowahi kudaiwa na Marekani kuwa fedha za tanzanite kutoka Tanzania zilitumiwa na Osama bin Laden? (jamaa walitaka kuzuia biashara ya tanzanite)

Maswali na mifano ya namna hii ni mingi. Kuna wakati Marekani iliwahi kudai kuwa Tanzania si salama (kiugaidi) na hivyo kuonya raia wake kusafiri kwenda Tanzania! Baada ya kubanwa waliomba radhi.

Kuna wakati fulani baadhi ya Wanasayansi walidai kuwa Mlima Kilimanjaro ulikuwa umepoteza theluji yake na unateketea. Baada ya kubanwa pia walikula maneno yao.

Hebu tuangalie picha kubwa (big picture) ya nini kimekuwa kikiripotiwa katika vyombo vya habari nchini Tanzania katika siku za karibuni kuhusiana na rasilimali zetu. Nitatoa mifano miwili. Kumekuwa na habari za vifo vya sokwe mtu huko Kigoma (Mahale Game Reserve) na ugonjwa na vifo vya simba huko Serengeti. Hii ni "coincidence"?

Tanzania sasa inakabiliwa na matatizo ya umeme (usiulize jamaa wa NetGroup walikuwa wanafanya nini siku zote na hawakujua habari za Mtera na Kidatu). Nadhani hiyo mitambo ya gesi ya Ubungo toka ifungwe ishaharibika kama mara tatu hivi. Nafikiri wakati fulani JK alitembelea pale Ubungo kwenye mitambo, wakati imeharibika, akawauliza watu wa Wizara kuwa mitambo inapoharibika mkataba unasemaje? Hii, kwa maoni yangu, ni kutaka kuwabana hao jamaa wasije wakawa wanafanya njama mitambo "inaharibika" kumbe hiyo yote ikiwa ni kuhujumu uchumi.

Nihitimishe maoni yangu kwa kusema kuwa ni vema wakati mwingine tukawa tunayaangalia matukio kwa mapana na marefu, na pia kujiuliza kama kuna "coincidence" baadhi ya matukio yanapotokea. Nafikiri wenzetu Wazungu hawana mambo ya "coincidence" hasa inapokuwa wanasughulikia masuala yenye maslahi ya taifa. Wengine, na pengine, wamekwenda mbali zaidi kiasi cha kukana uwepo wa Mungu kwani hawaamini katika mambo kutokea kwa bahati tu.
 
Mwanagenzi
Hapa alikuja mtu anaitwa tafiti kalala, sasa umekuja wewe utasinzia .Mimi natafuta muda nije tuendelee na hii mada maana naona unatupotosha na unapinda ukweli .Nitarudi
 
Mwanagenzi,

Kama nimekuelewa vizuri ni kuwa unamaanisha kuwa kuna kikundi cha watu, taasisi au mataifa flani ambayo yana deliberate conspiracy ya kuichafulia jina Tanzania, na awamu hii in particular. Is it? Kama ndivyo nnapata taabu kiasi kuelewa unakusudia ni kina nani na kwa nini.

Nashindwa ku-comment sana kwa sababu binafsi filamu ya mapanki sijaitazama.. nimesoma reviews na articles mbali mbali from both sides. Kwa juu juu maoni yangu ni kuwa both sides (mtengeza sinema na serikali yetu) wame exaggerate mambo, the former kwa kupotray things too negatively and the latter for the total denial.

I had a good laugh when I watched the video clip of fish industry in Tanzania at http://darwinsnightmare.net, man... the place and the entire process was too clean to be realistic.

I hope .. and this is just my hope .. that hii total denial ni strategy tu ya kusafisha jina la nchi tu while seriously working to resolve the issues raised by these documentaries. Whether it is a right strategy/approach or not.. kila mtu na maoni yake.
 
Swali kwako Mwanagenzi
Hivi ni kwa nini hii documentary Serikali imekataa kuiweka kwenye TVT watu wajionee na tupate nafasi ya kuijadili badala ya hivi sasa wakubwa wachache wameiona ndiyo wana tusemea juu ya ubaya huo mwaka huu 2006? Hayo mambo yalikuwa ya miaka na 60 na si sasa .Ile si ngono Serikali badala ya kukataa sana iweke hewani watu waone waamue inaona ugumu gani ?
 
Bw Mugishagwe,
Correction kidogo ... haya masuala ni ya mwaka 2004 sio miaka ya 60. Nijuavyo kelele zimeanza baada ya hii film kuonyeshwa mara kadhaa hapo London, ndipo wakubwa walipoamka. (Sijui hawakuwa na taarifa ilipoonyeshwa kwenye matamasha kadhaa duniani?!) Of course, exposure on TV ni kubwa zaidi kuliko katika matamasha.

I might be wrong, but I think TVT will need permission .. and probably pay ..to show this documentary on TV.. in the current situation, I don't think the two parties are in the mood to seek/give that permission.

Ref: http://www.darwinsnightmare.com/darwin/press/HubertSauper_BIOGRAPHY.pdf
 
Mwanagenzi,

To start with you have raised good points. "Speculations & Coincidences"

Katika Intelijensia hakuna kitu kinaitwa coincidence! nor speculations.

1.Kama umewahi kuwepo maeneo ya mipakani ya nchini mwetu, na hata kufanya shughuli zako mipakani nafikiri, utajiuliza maswali mengi sana on what is going on. niliwahi kuwa mpakani mwa Kenya na Sudan, kuna siku nilishuhudia kwa macho yangu silaha kubwa kubwa zikipitishwa tokea Kenya kwenda kusini Sudan. sasa tujiulize, Mtu kama Joseph Kony ana uhusiano mzuri sana na SPLA what does this mean na zile silaha. nikiwa kwenye moja ya timu ya UN ktk relief missions huko Congo, mambo niliyoyaona inasikitisha kuhus hizo silaha. Yes zinapita TZ kihalali kuelekea serikali ya Uganda, Rwanda etc, however zinapoishia at the end of the day ajuaye Mola, tujiulize pia Uganda na Rwanda wanafanya nini kule Congo. na Banyamulenge je?

2.Ni kweli hii sio coincidence kuwa waTZ hatunufaiki na maliasili/mazao yetu. Tujiulize samaki aliyetoka lake victoria ukimkuta huko europe anauzwa euros ngapi? Hivi ni kwa nini Wachagga waling'oa mikahawa yote na kupanda nyanya.
Tanzanite haipo sehemu nyingine duniani isipokuwa Tanzania tu. Hivi ni kweli tunafaidika na haya madini?. Majogo aliulizwa bungeni kwanini mchanga kutoka kwenye machimbo ya dhahabu unachukuliwa tani kwa tani na ndege kupelekwa nje, akajibu "eti hatuna utaalamu wa kuchunguza hapa nchini"!!!!, uliza leo wananchi wanafaidika?

3.Kuhus wakenya kuongelea maswala yetu, hawa watu siwaamini hata siku moja. however, ukweli unabaki pale pale kuwa madini hayo ya Tanzanite faida yake ni ngumu kuielezea. na usemi kuwa kuna watakaofaidika na watakao umia, ngoja nikuwekee sawa, wachache watafaidika na wengi wataumia. Na tena watanzania tusipo zingatia ELIMU, utandawazi utatumaliza.

4.Ni kweli theluji ktk mlima kilimanjaro imepungua saana saana. hii imesababishwa na mambo mengi, human activities ndani ya mlima huo being one of them.
 
Ndiyo Mlalahoi.
Niliposema hii si miaka 60 nilikuwa na maana kwamba kuwadanya watu ama kuwa fool kama kuwasemea etc wakati filamu inaweza kuonwa na wakati JK analia na watanzania wengi hawajaiona hii filamu watu wanazo wana amgalai hata TZ wamesha nunua DVD.Ndiyo ilikuwa maana yangu .

Ogah safi sana . Mimi nilimuonya huyu Mwanagenzi kwamba hapa andika ukiwa macho usifumbe macho nyeti zinakatwa sana hapa na kwa ushahidi sasa kaanza kuona.Utafiti hafifu hapa utagonga mwamba. Karibu mwanagenzi taratibu utaelewa nilicho kueleza mwanzoni .Sijasoma maelezo yako ndiyo maana sijachangia ila nitayasoma muda muaka niseme ila kwa uharaka niliona mawazo yako nikaona duh! Huyu atapewa data hadi atanawa .Sasa data hizo .Ogah asante mimi natoka kidogo niarudi kulonga baadaye .
 
Ndugu Mwanagenzi karibu sana hapa kwenye uwanja mbadala wa kutolea hoja.

Kwa kweli nimesoma maandiko yako sikuweza kuvumilia kukaa kimya,

Kwanza kabisa naomba kukuuliza je umeangalia/umeiona Filamu ya Mapanki au ni sawa na yale ya Kikwete kuzungumzia kitu ambacho hajakiona ila kaambiwa.
Filamu ya Mapanki siyo Filamu Chuku, bali filamu inayoonesha hali halisi, haikutengezwa ndani ya studio bali ilichukuliwa kwenye mazingira halisi. Kusema ina ukweli mdogo unamaanisha kinachoonekana kwenye hiyo Filamu ni kutoka nchi ya Kusadikika na siyo Mwanza au kwa maneno mengine unataka kuiambia jamii kuwa Muaandaji wa Filamu alitengeza hayo mazingira kabla ya kurecord

Pili, nashindwa kuwaelewa nyinyi na wengine mnaongangania swala la silaha ambalo halikuchukua hata asilimia kumi ya Filamu yote. Yaani mnaacha kuchambua matatizo makubwa ya kijamii mnakimbilia silaha, kwa maneno mengine basi mnadhihirisha wazi kuwa Filamu yote ni kweli isipokuwa sehemu ya Silaha tu.

Tatu, kwenye Filamu hakuna sehemu inayosema Serikali inawasaidia waasi bali inaonesha ni namna gani Tanzania hutumika kupitishia silaha zinazokwenda nchi jirani. Uwanja wa ndege wa Mwanza haujaanza kutumika leo kwa ajili ya nchi za Maziwa Makuu infact ndiyo uwanja pekee unatumika kama refueling centre kwa ndege kubwa. Ni nini kinachokufanya usiamini ndege zinazopitia zinaweza kuwa na silaha. Au ni nini ambacho hizo ndege hupeleka kwenye nchi hizo.
Hili swala la silaha lipo siku nyingi na infact kuna raia/kampuni moja ya Uholansi ilikuwa ije kujenga kiwanda cha silaha Mwanza. Hii ilikuwa inafanyika siri siri kati ya Tanzania na mhusika mpaka pale Bunge la Uholansi lilipopata habari kutoka Serikali za nchi za Maziwa makuu kuhusu athari za kuwa na kiwanda cha silaha maeneo hayo. Pia umesema silaha hizo zinaweza kuwa za majenshi ya nchi husika. Silaha za Majeshi ya nchi husafirishwa bila kufichwafichwa na huwa wanadeclare kabisa kwenye viwanja vya ndege. Kama zilikuwa silaha za majeshi ya nchi husika mbona serikali haijasema hilo.

Kwenye hoja yako ya Pili ya faida za samaki kwa wakazi wa Mwanza, bado sijaona hoja yenye kueleweka.
Sasa wewe kweli una tofauti na viongozi wetu wanaogawa mali zetu bure na kutoa misamahaa ya kodi kisa "UTANDAWAZI" Kwa hiyo wewe unapigia debe sera za kuwaumiza watoa mali ghafi. Kwenye filamu hamna sehemu inayosema watu wanakula mapanki kwa sababu ya uhaba wa samaki. Kuna tofauti kati ya uhaba na kukosa access au uwezo wa kupata samaki wazuri. Nadhani kama umesoma uchumi unafahamu kitu kinachoitwa scarcity and allocation of resources. Tatizo linaloonekana kwenye filamu ni allocation of resources kwa wazawa.

Filamu kutengenezwa na kuoneshwa kwenye Television ni vitu viwili ambavyo havina uhusiano wa aina yo yote ile (Non correlated circumstances). Kumbuka kwa Television kuonesha Filamu inahitaji kibali au ruhusa ya mtengenezaji pia inahitaji kupitia Baraza husika kuona kama inafaa kuoneshwa. Kwa hiyo kutokuoneshwa mara moja baada ya kutoka inawezekana kusabishwa na Televishion kutokuona umuhimu wa kuonesha awali au kuchelewa kupata ruhusa husika.

Kuhusu Filamu Gem Slave kuoneshwa New York (UN) ni sahihi kabisa kwani imetengenezwa na Pesa za UN kupitia wigo la Habari (IRIN) ambao makao yao makuu yapo New York. Kwa hiyo ulitaka wakaioneshe wapi? Pia kumbuka hii Filamu inaambatana na uzinduzi wa Filamu nyingine kibao. Na unafanyoka wakati huu kwa sababu ni wakti pekee ambao viongozi wa nchi zote wanachama wa UN watakuwepo pamoja na maofisa habari kutoka dunia nzima.

Kuhusu Ofisi za ILO-IPEC, ni kweli kuna ofisi Dar lakini ofisi inayohusika na Ajira ya Watoto makao yake yapo Nairobi.

Kuhusu nani anafaidika na filamu ni kwamba filamu haitengenezwi kufaidisha watu, ndiyo maana hutolewa bure kabisa. Lengo la Filamu ni kuonesha madhara na matatizo ya Ajira za watoto migodini.

Kuhusu kuathiri biashara ya Tanzanite, ni bora kuathiri hiyo biashara kuliko kuangamiza watoto wetu kwani watu wanaofaidika na biashara hii siyo watanzania bali wageni na wanasiasa, viongozi wa Serikali (10%)
Ili kuzidi kujifikirisha tujiulize baadhi ya maswali, kama vile:
Nani anafaidika na nani anaathirika na filamu hii?

Uchumi wa Tanzania hauwezi kuathiriwa na Filamu hii kwani Tangia Tanzanite ipatikane Tanzania haijawahi kuchangia hata 1% ya GNP or GDP


Maswali mengine uliyouliza naona hata aibu kujibu kwani kwa mtu mwenye logic hahitaji majibu yangu.
 
Mimi nashangaa sana watu wanaocriticize hizi sinema. Sijaiona hii ya Mererani lakini ukweli unabakia palepale. Watanzania walio wengi hawanufaiki na rasilimali zao fullstop! Wajua wakati mwingine tukiishi mijini au wale wengine waliobahatika kuishi ng'ambo wanaona hayo mambo kama viini macho, jamani watanzania walio wengi wanapigika sio mchezo. To this is a wake up call, serikali na wale watanzania walio neemeka jamani tusaidie mass ya watanzania walio kwenye lindi la umasikini. Its very shameful mtu ukiwa nje reference ya Africa is always watoto waliovimba matumbo na kung'ong'wa na nzi uso mzima & abject poverty. Nilipita kwenye duka moja la vito, pete ya Tanzanite inauzwa over £6,000. Then I ask myself yule mchimbaji alipata % ngapi ya hiyo value? probably less than 1%. Tuache kulumbana kuhusu ukweli, lets work diligently tusaidie watanzania wenzetu wanaopigika.
 
Ogah, Aljazeera,
Good points guys, good points. Kinachonishangaza ni watu hata kudiriki kusema kuwa wale walioonyeshwa katika hiyo filamu walilipwa (actors) Good grief! I saw the film, and I have lived in Mwanza. I have seen the pankis na harufu mbaya ya maeneo yanakotupwa hayo majitu. Those who are making money from this business are not even Tanzanians, kama ilivyo vile vile na madini ya Tanzanite. Kama ndio huo utandawazi basi nasema to hell!
 
Nashukuru kwa michango mbalimbali iliyokwishatolewa mpaka sasa. Naomba tuendelee kujadiliana, na wenye data zaidi walete!
 
Mwanagenzi,

Defence, defence, defence.... what are you trying to defend when there is othing to defend. This is evidence and the "owners" are obvious - the children involved - and you see them speaking - that if they had power they would stop this ad even put into jail those who use them this way.

Instead of adopting a defence stance let us use these revelations to define the problem clearly and solve it. Resolutions like "ajira kwa wote" or "elimu kwa wote" do ot take us far sometimes. The question then is which ajira and what type of education. We need effectine ajiras and education which cannot come out of defence for its own sake or ill-structured and ill-defined problem. I am glad I have seen this. It makes me reassess my pride in Tanzanite which except for the indicative name it appears in the market more as a product of other countries than Tanzania. Our children suffer and we get peanuts.
 
Mugishagwe said:
Swali kwako Mwanagenzi
Hivi ni kwa nini hii documentary Serikali imekataa kuiweka kwenye TVT watu wajionee na tupate nafasi ya kuijadili badala ya hivi sasa wakubwa wachache wameiona ndiyo wana tusemea juu ya ubaya huo mwaka huu 2006? Hayo mambo yalikuwa ya miaka na 60 na si sasa .Ile si ngono Serikali badala ya kukataa sana iweke hewani watu waone waamue inaona ugumu gani ?

TVT Walinyimwa kibali na Bwana Sauper
 
Kwa sasa niseme tu kama watu wana nafasi waangalie tena filamu hizi, na pia wachangiaji warejee maoni yangu. Kwa haraka haraka nijibu baadhi ya hoja huku nikiendeleza mjadala.
Katika Filamu ya Mapanki:
Nadhani suala si kupitisha silaha Tanzania. Nchi yetu inaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia kuwa hao jirani zetu ni "land-locked". Suala labda lingekuwa kama serikali haikulipwa stahili yake au fedha zilizolipwa zimeliwa na wachache. Tukumbuke kuwa hata nchi za kusini mwa Afrika zilisaidiwa na Tanzania wakati wa mapambano yao ya kujipatia uhuru/kupinga udhalimu na ubaguzi wa rangi. Ni wazi wakati huo na kwa kitendo hicho Tanzania haikufurahisha baadhi ya nchi/watu.


NB: Waliotaka kujenga kiwanda cha silaha walikuwa Wabelgiji na si Wadachi.

Suala la baadhi ya watu kushindwa kununua samaki (sangara) labda lihusishwe na kukithiri kwa umaskini kwa ujumla lakini siyo "biashara ya minofu ya samaki" au kuwepo kwa "viwanda" pekee. Na kama mtu ni maskini/fukara kabisa ina maana asingeweza kununua sangara wanaouzwa viwandani, sana sana angekula samaki wadogo wadogo wengine kama furu na dagaa; na hiyo ndiyo imekuwa kawaida kwa wakazi wenye kipato cha chini (kanda ya ziwa) kabla hata ya kuanzishwa viwanda vya kusindika samaki.

Filamu ya Mererani:
Ni ukweli kuwa hao watoto wanaofanya kazi mgodini hawakustahili kufanya hivyo. Lakini ni ukweli pia kuwa ni umaskini ndiyo umewafikisha hapo (angalia yule mama muuza mboga mwenyewe anakiri kuwa ni bora mwanae aendelee na "kazi" hiyo ili siku zipite, watoto wakue, labda siku moja watakuwa na maisha bora zaidi). Hizo ndiyo changamoto za nchi zetu.

Tujiulize tena: Je, filamu hii inaweza kusaidia kwa kiwango gani kuondoa Ajira ya Watoto (Child Labour) nchini? Je, hiyo unahitaji miradi mingapi ya aina ya kina Good Hope? Si kila mahali nchini kuna child labour?

Naamini leo hii hao watoto wakiondolewa kwenye kazi hiyo, wao na familia zao huenda wakawa maskini zaidi. Sana sana watakaonufaika ni kina AFGEM/TanzaniteOne. Je, hivi ndivyo tunataka? Nasema haya si kwa vile naunga mkono ajira mbaya kwa watoto, lakini najaribu kuwa mkweli (I consider myself a Realist).
Nadhani filamu ingetusaidia kama ingewahoji hao wawekezaji wakubwa ni kwa kiasi gani wanasaidia jamii inayowazunguka kama siyo kupigana risasi nao kila mwezi!
Kuna mchangiaji amebeza asilimia "ndogo" inayotokana na biashara ya vito hivi. Huyo amesimamia kwenye uchumi wa makaratasi (uchumi wa kina Mkapa!) Kumbuka kuwa unapozuia biashara hiyo unaathiri mlolongo wa Watanzania tunaoishi kwa kutegemeana (si unajua mambo ya extended family?) Hiyo asilimia inaonekana kuwa ndogo lakini umuhimu wake ni mkubwa sana kwa kuzingatia hoja niliyoitoa hapo juu. Je, ingekuwa asilimia ngapi ndiyo ingestahili sisi tushtuke?
Pamoja na kuonyesha watoto wanatumikishwa, filamu haionyeshi ni kwa vipi taifa linaweza kupambana katika mfumo wa biashara ya kimataifa.
Tangu enzi za Ukoloni Mkongwe mpaka leo hii, Afrika imekuwa mtoaji wa rasilimali tu na kamwe (au nadra sana) haifaidiki na rasilimali hizo ukilinganisha na hao Wakoloni wetu (watandawezi). Mifano ya kupunjwa ni katika kila rasilimali, iwe ni mazao kama pamba na kahawa, au madini na mbao.

Naunga mkono umuhimu wa Watanzania kusaidiana kukabiliana na athari na matatizo haya yanayotokana na utandawazi. Tusiishie kulalamikia tu mfumo uliopo. Pia tujue kuwa wanaonufaika na mfumo huu wanapenda hali hiyo iendelee na hivyo wanaweza kutumia mbinu kama hizo kutuchanganya tukaishia kupigana wenyewe kwa wenyewe huku wao wakikomba rasilimali zetu. Tuwe makini!
 
mTz,
Sijui niseme nini. Ndiyo maendeleo hayo? Lakini yule mama kidogo anasikitisha.
 
Back
Top Bottom