Gekul amepata nafasi ya kusikilizwa?

Gekul amepata nafasi ya kusikilizwa?

Hii habari inaonekana ya kutengeneza na inawezekana Gekul haungi mkono kundi fulani ndani ya CCM, so walimpandisha ili waje kumshusha kwa aibu ili jimbo sasa lirudi CCM. Maana hayo yanayosema siyo rahisi kutendwa na mwanamke kama Gekul.

Tatizo statement ya RPC na Katibu wa Mbunge zinapishana. RPC kadai walienda kumkamata huyo bwanamdogo kwenye hoteli ya huyo Gekul kwa tuhuma za kutaka kumuwekea sumu kwenye chakula.

Statement ya Katibu wa Mbunge inadai kuwa huyo mhanga alikamatwa kwenye hoteli ya Gekul akiwa na lengo la ushirikina. Yani alikuwa analenga kuchota mchanga ndani ya hiyo hoteli na kumpelekea mganga aliyekuwa anasubiria kwenye hoteli shindani na hiyo ya Gekul.

Kama RPC na Katibu wa Mbunge wanakiri Jambo Hilo kutokea, utaitaje uongo?. Na wote wanamtetea Gekul.
 
Zile tuhuma ni nzito mnoo, Natamani uchunguzi wa wazi ufanyike ili kuthibitisha hayo madai. Nina uhakika ni tuhuma za uwongo ama zimekolezwa chumvi. Yeyote anaweza kurekodi ile clip na kumchafua mtu yeyote.
Kabla ya utenguzi prezdaa kwa kutumia vitengo vyake atakuwa alijirizisha kuwa kuna jambo baya lilitendwa na mteuliwa.
 
Kwa kweli jambo analotuhumiwa nalo Pauline Gekul ni zito sana na linaleta ukakasi sana akilini!

Siungi kabisa tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Ila pia lazima tukubali kwamba tuna jamii yenye matatizo makubwa sana!

Tuna Jamii yenye kupenda kutoa maamuzi pasipo kusikiliza pande zote.
" Nobody should be condemned unheard" , hear both parties!
Hiyo ni principle ya natural justice.

Huyo Kijana anasema, Pauline Gekul aliagiza wavuliwe nguo waingiziwe chupa!
Sasa watu wamesha conclude kwamba waliingiziwa chupa, je imethibitika kwamba waliingiziwa chupa?!

Binadamu tuna mambo mengi sana,yawezekana pia ikawa vijana baada ya hilo sakata wakawa coached na wabaya wa Pauline Gekul kutumia hiyo technic ya assertion ya " kuingiziwa chupa" ili kum- pull down Pauline Gekul?!

Hapo ndipo uchunguzi wa kina unapohitajika ili ukweli ubainishwe na haki iweze kuonekana imetendeka kwa pande zote husika!

Tujizuie kuwa wepesi sana wa kutoa judgements ambazo hatuna details na facts zake!

Halafu siku hizi raia akionewa huwa anaonekana muongo. Hata yule Rama wa Mtwara angelalamika polisi wanataka kumuua mngemuita muongo. Ila alivyouawa ndio watu wamejua kweli polisi walikuwa wanamtesa.
 
Sijui kwanini kila nikimtazama yule mwanamke namuona anafanana na kile anachotuhumiwa nacho

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Unawaza kama mimi kabisa naizoom picha yake anavyooneka mpole kwenye picha ukishaona ile miwani yake unaanza kudauti unaangalia mkao wake wa mabega unagundua ni aina ya watu wanaokataa jambo kwa mabenga hapo sasa unakua 50/50 coz tunajua tabia za hao watu
Anywa nakazia kwa mkuu hapo juu
 
Una uhakika ni kweli tuhuma ni za kweli au zimetengenezwa kumchafua kisiasa

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app

Halafu siku hizi raia akionewa huwa anaonekana muongo. Hata yule Rama wa Mtwara angelalamika polisi wanataka kumuua mngemuita muongo. Ila alivyouawa ndio watu wamejua kweli polisi walikuwa wananmtesa.
 
Huwa mnalilia utawala wa haki na sheria..au siyo nyie
?

Wewe naye hujitambui kabisa. Waziri katumbuliwa ili uchunguzi na upelelezi ifanyike kwa haki. Maana bila kutumbuliwa angeweza kutumia mamlaka yake kuficha ushahidi. Hiyo sio haki?. Ulitaka aendelee na uwaziri? Huku kukiwa na tuhuma Kama hizo?. Acheni kujifanya daraja la juu na kudharau raia maskini.
 
Watu wengi watasukizwa chupa nyie chekenichekeni tu

Ova
 
Kibatala awe wakili wa mtoto
Haiwezekani haujui utaratibu wa kesi za jinai .Mtoto atakuwa shahidi upande wa mashtaka ambao ni serikali . (Mawakili wa serikali )
Mawakili binafsi wanatetea watuhumiwa
 
Sheria ni msumeno

Tusimuhukumu Gekui tusubiri maamuzi ya DPP au Mahakama

Ahsanteni sana

Nawatakia Dominica Njema 😄
Ila na polisi waliosimamia ule ushenzi wanatakiwa wawajibishwe equally kwasababu sheria ipo wazi na miongozo ya jeshi ipo wazi hawaruhusiwi kufuata unlawful orders, wanaliaibisha jeshi la polisi, juzi tu serikali imetumia mamilioni kwenye tume ya haki jinai leo polisi na bunduki anakaa anasimamia ufirauni
 
Sheria ni msumeno

Tusimuhukumu Gekui tusubiri maamuzi ya DPP au Mahakama

Ahsanteni sana

Nawatakia Dominica Njema 😄
Ataenda kusikilizwa mahakamani nafas aliyovuliwa ni ya uteuzi na SI ya kuchaguliwa ndio maana bado ni mbunge na huko mahakamani ikithibitika tuhuma zinazomkabili basi avuliwe uanachama wa ccm na automatically atakuwa amepoteza sifa ya kuwa mbunge.
 
Wewe naye hujitambui kabisa. Waziri katumbuliwa ili uchunguzi na upelelezi ifanyike kwa haki. Maana bila kutumbuliwa angeweza kutumia mamlaka yake kuficha ushahidi. Hiyo sio haki?. Ulitaka aendelee na uwaziri? Huku kukiwa na tuhuma Kama hizo?. Acheni kujifanya daraja la juu na kudharau raia maskini.
Mbona Yule wa tamisemi hakutumbuliwa kupisha uchunguzi.
Na tume ikaundwa kuchunguza akiwa kazini.
Naami hadi Rais kumtengua huyu mama ni either vyombo vyake vimechunguza vimegundua ni tukio la kweli vikamtaarifu.
Au pia inawezekani ni laana tu za usaliti Kwa cdm za huyu Dada zinamrudia katengenezewa tukio
 
Back
Top Bottom