Geita: Wananchi wamuua aliyemshambulia Askari

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
4,212
2,000
Kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 20-25 amefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi baada ya kumjeruhi kwenye taya na kidevu Askari wa Usalama Barabarani kwa kumpiga na chuma cha kupondea mawe (Moko), wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi Mtaa wa Mwembeni, barabara ya Katoro Ushirombo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuvamiwa na kujeruhiwa askari wa barabarani namba H1619 John Charles lililopelekea wananchi wenye hasira kali kuingilia kati na kumuuwa muhusika kwa kipigo.

Aidha, Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi wenye migogoro binafsi na Askari kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zinazostahiki.

Geita.jpg

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, akionesha chuma kilichotumika kumjeruhi Askari
 

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Apr 16, 2018
1,501
2,000
Huu mwezi una majanga!Tozo mpya,jamaa ampiga mwenzie na risasai na kujiua na yeye,mwanamke kamchoma moto mpenzi na kufa,jamaa auwawa kwa kumpiga polisi!Wazee wa dini iombeeni nchiTutaangamia. Bado corona phase3 kama umeme wa vijijini phase3!Hatari kamili.
 

Ismoo

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
328
500
Ukija kufuatilia vizuri hilo tukio unashangaa ji mchaga huyo
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
6,499
2,000
HAHAHAHHA.jpg

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, akionesha chuma kilichotumika kumjeruhi Askari

Kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 20-25 amefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi baada ya kumjeruhi kwenye taya na kidevu Askari wa Usalama Barabarani kwa kumpiga na chuma cha kupondea mawe (Moko), wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi Mtaa wa Mwembeni, barabara ya Katoro Ushirombo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuvamiwa na kujeruhiwa askari wa barabarani namba H1619 John Charles lililopelekea wananchi wenye hasira kali kuingilia kati na kumuua mhusika kwa kipigo.

Aidha, Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi wenye migogoro binafsi na Askari kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zinazostahiki.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,686
2,000
Askari aliyepewa mafunzo tena akafuzu kuwa ni shupavu wakati wa pass out anashambuliwa na kijana wa miaka 20 mpaka aokolewe na wananchi? Nashauri arudishwe mafunzoni

Lakini siku zote taarifa za awali za polisi huwa ni questionable, hebu tusubiri.
Rreference:
  1. Wafanyabiashara wa madini wa Mahenge
  2. Kifo cha Daudi Mwangosi
 

Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,581
2,000
Halafu kuna watu wanasema Askari hawapendwi, hongera kwa wana Geita mliomuokoa Askari
Chuki dhidi ya Polisi imechangiwa 98% na ccm!
Just imagine vile chama cha majambazi wamegeuza jeshi letu la polisi kama tawi lao, wanalitumia kihuni kufanikisha malengo yao ya kisiasa wakati huo huo maslahi ya askari hao kubaki duni, yani wanatumika kama toilet paper.

Hapa ndipo umuhimu wa katiba mpya unapoonekana, hatuwezi kuwa na Igp anayeteuliwa na mwanasiasa(rais), maRPCs wanaoteuliwa na ikulu(kwenye kivuli tunaona wameteuliwa na jeshi la polisi), na maOCDs wanaowekwa kwa utaratibu huo huo. Upandaji wa vyeo wa hawa watu umekaa kisiasa zaidi, RPC ili apande cheo lazima "awasulubu" na kuwasingizia kesi wapinzani, OCD ruhusu mikutano ya wapinzani wilayani kwako uone kama utapanda cheo!

Tunahitaji katiba mpya ili kuondoa huu ushenzi wa matumizi ya kihuni ya jeshi letu la polisi, hatutaki tena taasisi hii kutumika kisiasa, tunahitaji uteuzi wa viongozi wake usihusishwe wala kuingiliwa na wanasiasa! Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake irekebishwe, waziri wa mambo ya ndani asitoe maelekezo yake ya kisiasa kwa polisi!

Jeshi la polisi liwe autonomous, hao askari ni wazazi, ni ndugu zetu, ni jamaa na marafiki, tunawapenda kama tu wataacha kufungamana na wahuni wa kijani!
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,068
2,000
Chuki dhidi ya Polisi imechangiwa 98% na ccm!
Just imagine vile chama cha majambazi wamegeuza jeshi letu la polisi kama tawi lao, wanalitumia kihuni kufanikisha malengo yao ya kisiasa wakati huo huo maslahi ya askari hao kubaki duni, yani wanatumika kama toilet paper...
wacha ngonjera mkuu.

usichojua polisi hawatoki jupiter, ni hawa hawa ndugu zetu na binamu zetu.

yaani ukimdhuru polisi basi, mpenzi wako au mwenye nyumba wako, au boss wako kazini, au dereva wako atakujulisha kwamba hatakuhudumia, maana kafiwa au anauguliwa.

chuki dhidi yao ni za kiasi tu, wala zisije kukupoteza ukadhani anaweza kudhulika au kuuawa watu wakampa zawadi mtendaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom