luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,295
- 8,261
Kumbe huko usukumani ushirikina Ni nje njeMlemhola wamayo nabha bhabha,, koyomba gwa nhana gete eeee mbiti tolenajo neyo jiletwambeleja gete gete
Niliwahi kuishi Same Kilimanjaro sehemu moja inaitwa Gonja-Maole na wasambaa, kuna mzee nilitofautiana nae kidogo ni mzee wa kisambaa
Kiufupi alinikopesha pesa na nikamuahidi siku ya kumrudishia, ilipofika siku yenyewe sikuwa na pesa ya kumpa akadhani namfanyia makusudi kuwa nataka kumdhurumu
Akanitishia ushirikina kuwa atanifanyia kitu mbaya,, aliponiambia nilipata ujasiri wa kumdhurumu kabisa maana niliamini hawezi nifanyia chochote
Nikamuambia kabisa mzee sikulipi pesa yako nasubiri utimize kwanza ulichoniahidi, tukawa tunapishana tu namsalimia anaitikia kwa unyonge mpaka miezi miwili na kitu ikapita
Baadae nahis aliamini kweli namaanisha sina mpango wa kumlipa ikabidi aende kwa mwenyekiti wa mtaa
Mwenyekiti aliponifuata nikaona isiwe kesi ndo nikamlipa,,,, Nimekulia mtaaa fulani unaitwa Kigoma Road upo Halmashauri ya Mji Geita kata ya Kasamwa
Nadhani wanaofahamu matukio ya pale wataelewa nilikuwa natembea usiku mnene peke angu bila woga
Kuna ndg yangu ni kiongozi wa ngoma ( jamii ya wachweji) mkoa wa Geita nadhani hapa pia watu wa usukumani mnawajua wachweji ni watu gani, kanifundisha vitu vingi sana
Niliwahi kushuhudia tukio lake la kuua wachawi wawili waliokuwa wameenda kwenye sherehe kuiba nyama lililotokea Kata ya Bulela Halmashauri (mji) Geita
Kiufupi bila yeye kuwepo wachweji hawafanyi lolote huwa naona mnavyowasifia kina Mshana Jr nabaki kusema tu hamjui mlitendalo
Sent using Jamii Forums mobile app