Geita: Wananchi wadaiwa kufuga Fisi na kuwatumia kama usafiri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Baada ya watoto watatu kuuawa na fisi huku watano wakijeruhiwa vibaya wilayani Nyang'wale mkoani Geita mkuu wa wilaya hiyo Bw.Wilson Shimo ameanzisha operesheni ya nyumba kwa nyumba huku akiwaonya wananchi wanaofuga makundi makubwa ya fisi kwa shughuli usafiri.

Akizungumzia matukio ya vifo hivyo mkuu huyo wa wilaya anasema tayari fisi ishirini na nane wameuawa katika operesheni hiyo na msako unaendelea usiku na mchana.

Kaimu afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Nyangwale Bw. Dickson Msumari anasema fisi hao ni tishio na wamekuwa wakiingia mpaka maeneo ya mjini nyakati za mchana na kuua watoto.

Aidha, Mbunge wa jimbo la nyangwale Hussein Nassoro anasema wameomba nguvu kutoka mkoa Shinyanga ili kuwawinda hao.

Chanzo: ITV
 
Itakuwa katika kuwaonyesha mabeberu kivitendo kwanini hasa hata chanjo zao hatuzihitaji.

Kwa hakika tuko vizuri kwani hata magari na ma bombardier yao hatuyahitaji kabisa.

Tuna vyetu vya asili tokea nyungu hadi fisi kwa usafiri.

Chezea Tanzania ya Magufuli wewe?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom