Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita kimetoa wito kwa wanachama wake kuzingatia utulivu na kuheshimu taratibu zilizowekwa wakati wa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza na wanachama wa CCM katika Kata ya Uyovu Wiaya ya Bukombe, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo, amesema chama kimetangaza mchakato wa kuchukua fomu ifikapo Aprili mosi ya mwaka huu, lakini hakijaruhusu kuanza kwa fujo na harakati zisizo rasmi katika kata na majimbo.
“Tunaheshimu na kutambua uwepo wa madiwani na wabunge waliopo kwa sasa, ambao bado hawajamaliza muda wao. Hivyo ni muhimu kufuata utaratibu bila kusababisha migawanyiko ndani ya chama,” amesema Magambo.