PreGE2025 Geita: Kamati mbalimbali zaundwa kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

PreGE2025 Geita: Kamati mbalimbali zaundwa kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Huku Serikali ikiwa inaendelea na juhudi za kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi haswa maeneo ya vijijini, kamati mbali mbali ambazo zimeundwa kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, hususani kwenye nyanja za Elimu na Afya, zimetakiwa kuhakikisha zinafuatilia hatua kwa hatua ukamilishaji wa miradi hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.

Akizungumza tarehe 11, Juni kwenye mwendelezo wa ziara maalumu ya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika Tarafa ya Busanda, Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu, Bi. Sarah Yohana, kwa niaba ya Mkurugenzi, amewataka wenye dhamana ya usimamizi wa miradi hiyo, kujikita kwenye maeneo ya muhimu kwa miradi iliyopo katika hatua za ukamilishaji.

Bi. Sarah ameongeza pia kwa kusema, Watendaji wa Kata wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanaitambua miradi iliyopo kwenye maeneo yao, pamoja na kufuatilia fedha ambazo zimetengwa na Halmashauri kwaajili ya kumalizia miradi hiyo.
 
Back
Top Bottom