heshima nicholaus
Member
- Dec 26, 2011
- 16
- 3
ANDIKO LA KUTOKA GAZETI MAARUFU DUNIANI FORBES
LIKIMUONGELEA JACKLINE NTUYABALIWE MENGI NA MAISHA YAKE YA BIASHARA.
Malkia wa Urembo kutoka Tanzania Anayejenga Himaya ya Samani
Akijivinjari ndani ya jiji la Dar es salaam kwenye foleni mida ya mchana ndani ya gari lake jeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo mwembamba mwenye miaka 38, akiwa ameduwaa akiiangalia picha ya samani za kulia chakula kwenye simu yake. Kwa kutumia kidole chake chembamba, kwa madaha, anaiwasha simu yake ili kunionesha picha ambazo anaziangalia.
“Hii ni moja ya seti ya samani zetu,” anasema, huku akionesha kwa kidole picha ya seti ya samani 5. Ni moja ya bidhaa zinazotegenezwa na Molocaho by Amorette, kiwanda cha kutengeneza samani ambacho amekianzisha hivi karibuni. “Hii samani imetengenezwa kwa mabaki ya mbao ya boti ya mizigo iliyochakaa kutoka Bahari ya Hindi katika mwambao wa pwani ya Tanzania,” akisema mjasiriamali mwenye kujituma.
Samani za kulia chakula, ananiambia, ameombwa na familia moja kutoka Ulaya ambayo ilitembelea duka lake la samani hivi karibuni Dar es salaam wakati wa likizo majuma kadhaa yaliyopita na anakaribia kuzisafirisha kwa wateja wake wapya wa Ulaya. Lakini anakwenda kwanza mara moja kwenye kiwanda chake kuzikagua mwenyewe hizo samani kwa mara ya mwisho kabla hazijasafirishwa ili kuhakikisha zinatengenezwa vizuri.
Jacqueline Ntuyabaliwe, mwenye kiu ya mafanikio ni mwanamke makini sana. Licha ya kuwa na shughuli nyingi pia (ni balozi wa kiafrika wa shirika la kulinda wanyama pori duniani WildAid na huudhuria baadhi ya mikutano ya bodi; mama mwenye watoto wawili mapacha wa kiume; mke wa mmoja ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa barani Afrika na anasimamia mfuko wa hisani kwa ajili ya elimu), Ntuyabaliwe huhakikisha anakagua mwenyewe kila samani inayotengenezwa na kampuni yake kabla haijauzwa au kusafirishwa kwenda nje.
“Napenda vitu vyenye ubora wa hali ya juu!” anasema kwa hisia aliyekuwa malkia wa urembo Tanzania na mwanamuziki, akivuta pumzi kuonesha msisitizo. Kila kitu tunachotengeneza Molocaho lazima kiwe na ubora wa hali ya juu,” anasema. “Tunashindana na makampuni makubwa sana duniani kwa hiyo kama hatutazingatia ubora, itabidi tufunge virago vyetu turudi nyumbani.”
Ntuyabaliwe, mzaliwa wa Tanzania, aliyepata mafunzo ya ubunifu wa ndani nchini Uingereza, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya kitanzania ambayo hubuni na kutengeneza samani zenye ubora wa hali ya juu, samani na vyombo, mbunifu wa mavazi, mapambo, samani za nje na bustanini. Molocaho imetengeneza samani za kiafrika zenye ubora wa hali ya juu kwa kuchanganya kwa ustadi vitambaa vya kitanzania na kuviweka katika mwonekano wa kisasa, ubunifu wa kimataifa wenye uwezo wa kuvuka mipaka ya mabara. Molocaho ni moja ya kampuni za samani Afrika Mashariki zinazokua kwa kasi kubwa, imajijengea umaarufu kwa kuhakikisha kwamba mbao na malighafi za kitanzania zenye ubora wa hali ya juu zinatumika kutengenezea samani zenye mvuto wa hali ya juu.
“Malengo yetu ni kuwa na samani kutoka Tanzania zinazotambulika ulimwenguni. Hakika itachukua muda fulani kufikia hatua hiyo, lakini tuko thabiti,”ananiambia huku tukitembea ndani ya duka kubwa la samani katika mtaa wa jirani maarufu unaojulikana kama Masaki jijini Dar es salaam.
Ntuyabaliwe ni sura maarufu sana Tanzania. Mnamo mwaka 2000, alishinda Taji katika shindano la Ulimbwende nchini Tanzania na kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya Ulimbwende wa Dunia. Baada ya hapo, aliingia kwenye tasnia ya muziki na kujizolea umaarufu mkubwa na aliimba nyimbo nyingi ambazo zilishika chati ya juu Afrika Mashariki. Lakini shauku yake kubwa ilikuwa ni ubunifu wa ndani.
Anasema, hakika “Mimi nina kipaji cha ubunifu,” “Ninakumbuka, nilikuwa natamani kuwa mbunifu wa ndani na samani, Sanaa na mitindo- na nimekuwa na shauku kubwa ya kufuatilia historia na masuala ya ubunifu. Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikichora vitu mbalimbali. Ni moja kati ya vitu ambavyo nilikuwa navipenda sana.”
Baada ya kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki, alihisi kwamba ameshaikuza tasnia ya muziki na kuamua kufanya kitu kingine katika maisha yake. Alikwenda nchini Uingereza kujifunza ubunifu wa ndani ili kukinoa kipaji chake cha ubinifu, mnamo mwaka 2012, akaanzisha Amorette, kampuni yake ya ubunifu iliyopo jijini Dar es salaam. Amorette imekuwa na mafanikio makubwa na Ntuyabaliwe amefanya kazi na watu wengi na kampuni za kimataifa nchini Tanzania, akichanganya kwa ubunifu mitindo mbalimbali, rangi na kuiboresha vizuri kuendana na mazingira ya wateja wake.
Wakati huohuo, alianza kidogokidogo ubunifu wa kuchora samani. “Ninapenda samani, labda kwa sababu ya kazi yangu ya ubunifu wa ndani, lakini pia kwa sababu samani huwaelezea watu ni wa aina gani. Mwanzoni nilikuwa tu nikichora picha za samani, lakini mara nyingi, mume wangu aliiona baadhi ya michoro na kunipongeza. Aliniambia nilikuwa nachezea bahati. Alikuwa akiniambia nitilie maanani michoro yangu na nifungue kampuni,” Anaeleza Ntuyabaliwe.
Mume wake anaitwa Reginald Mengi, mfanyabiashara mkubwa Mtanzania ambaye amejipatia utajiri wake kupitia vinywaji vya Coca-Cola, uchimbaji wa madini na umiliki vituo vya luninga na magazeti.
“Unapokuwa na mtu mwenye mafanikio unahamasika kuongeza bidii. Kwa hiyo niliandaa mpango wa biashara nikaajiri wafanyakazi na kuitimiza ndoto yangu.”
Amorette, kampuni yake ya ubunifu wa ndani tayari ilikuwa maarufu miongoni mwa jamii ya watu wenye uwezo na jina lake lilikuwa likikua sana. Kutokana na mafanikio ya Amorette, mwezi September 2016, Ntuyabaliwe alizindua Molocaho by Amorette kama kampuni ya ubunifu na utengenezaji wa samani. Kwa muda mfupi tangu ianzishwe, kampuni imefanya vizuri na bado inaendelea kufanya vizuri.
“Tumekuwa na kazi nyingi sana,” anasema. “Sikutegemea kupata hata theluthi ya faida tuliyoyapata kwa kipindi cha miezi michache iliyopita.”
Ntuyabaliwe ndiye Mbunifu Mkuu. Kwa kutumia mbinu ya kiasili ya utengenezaji katika mazingira ya kisasa, Ntuyabaliwe hufanya kazi ya ubunifu wa samani za majumbani na maofisini. Samani za Molocaho zinafahamika kwa mistari ya kawaida na uhalisia ndiyo kitu kinachofanya ubunifu wake ukupe raha. Lakini ukiziangalia kwa karibu utagundua kuwa hiyo mistari imeficha ubunifu wa hali ya juu.
Na hivyo ndivyo Ntuyabaliwe anavyozipenda samani zake-zina mwonekano wa kawaida lakini zenye ubora wa hali ya juu. Shauku ya Ntuyabaliwe kuanzisha kampuni ya ubunifu wa samani ya Molacaho ilitokea tu. Mara chache, kitu cha asili kinaweza kukuhamasisha kuwa mbunifu, yaani ni kama radi-ndiyo siri ya mafanikio ya mauzo makubwa ya Molacaho ya kiti cha Radi, ambacho kimejaribu kuiga alama ya zigizaga ya bolti kikiwa katika hali ya kawaida. Kiti hiki kimekuwa kikipendwa sana na wateja wa ndani na nje ya nchi.
Molacaho inafanya kazi kwa kupokea oda, yaani kazi zake nyingi huwa ni za oda.
“Wateja wetu huwa wanaangalia katalogi yetu, huchagua samani wanayoitaka, kisha hutuambia kama kuna kitu chochote cha kuongeza au kurekebisha. Hii huhusisha majadiliano marefu na mteja ili kuelewa vizuri mahitaji yao,” anasema Ntuyabaliwe.
Mara nyingi samani za kutengenezwa kwa oda huwa na gharama kubwa zaidi kwa sababu hutengenezwa kulingana na mahitaji ya mteja. Ntuyabaliwe anakiri kwamba bei ya bidhaa zake ni kubwa na watanzania wengi wa kawaida hawawezi kuimudu. Asilimia kubwa ya watanzania ni masikini; kwa sababu gharama za bidhaa za Molacaho zinaanzia dola 250 kwa stuli mpaka dola 6000 kwa kitanda. “Tupo kwa ajili ya wateja wanaojitambua,” anasema bila kumumunya maneno. “Bidhaa zetu sio za bei rahisi wala ghali sana. Mwisho wa siku, tunapata mrejesho kutoka kwa wateja kwamba bei zetu zinaendana na thamani ya bidhaa zetu.”
Licha ya Ntuyabaliwe kuingiza tu hela, pia anafanya jitihada za kuendeleza mafundi nchini Tanzania. Mwanzoni mwaka huu, Amorette, kampuni yake ya ubunifu wa ndani, ilianza kutoa programu ya mafunzo kwa mafundi wa kitanzania
Madhumuni ya programu ya mafunzo inayotolewa na Amorette ni kuwapa fursa mafundi wa kitanzania kutengeneza bidhaa zinazokidhi vigezo vya kimataifa. Kwenye hizi programu washiriki ambao tayari wana uzoefu wa useremala, kutengeneza makochi au fani nyingine huudhuria mafunzo kwa muda wa miezi miwili chini ya usimamizi wa wataalamu maarufu wa kimataifa. Madhumuni ni kuwapatia teknolojia na maarifa watanzania.
Molocaho inajitahidi kutunza na kulinda mazingira kadiri inavyowezekana. Ndiyo maana Molocaho hupunguza matumizi makubwa na kuepuka matumizi mabaya pia. Kampuni hutumia mabaki ya mbao kutoka kwenye vyanzo tofauti na inaunga mkono mpango wa upandaji miti Tanzania nzima.
“Mwisho wa siku, biashara haitakiwi kuangalia faida tu pia inatakiwa kuisadia jamii ambayo inafanya nayo biashara,” anasema.
Sasa hivi, Molocaho imeajiri zaidi ya wafanyakazi 30 wa kudumu na kampuni iko mbioni kuanza kupata faida ndani ya mwaka mmoja.
“Ndiyo kwanza tumeanza,” anasema huku tukiondoka kwenye duka la Molocaho. “Lakini tutamjenga huyu mtoto na kuwa himaya siku moja. We angalia “
Source : forbes
The Beauty Queen From Tanzania Who Is Building A Furniture Empire