Gazeti la The East African: Katuni ya Kejeli kwa Tanzania, Olympic

Uganda imechukua Gold ya marathon, hajawatendea haki!!

Yap, this is a premature opinion (cartoon). They should have waited until the games are over. Otherwise, it's really funny & very true for Tz.
 
Miaka 32 Tanzania haijawahi kupata medali yoyote ya Olympic, nadhani mchoraji wa katuni hii anastahili kupewa medali
 
Wabongo bana tukiambiwa ukweli tunahamaki.


Ndiyo akili ya watu/jamii ya wasiokuwa na upeo wa kuona mbali. Inasikitisha lakini ndivyo ilivyo hapa kwetu, ukiongea ukweli watu wanakushangaa ama wanakudharau. Ukiwadanganya keshokutwa Jay Z anakuja kufungua studio mpya ya Bongo fleva, mashabiki wanajaa na kufunga barabara za mjini. Yaani sielewi tu, hii jamii yetu ikoje.
 
Mi sisemi lolote, hapa kabisa umeongea ukweli ila angalia kuna watu humu JF wanachukia watu kama wewe na wako tayari kukupiga mawe kupitia computer. Wanakuona we si mzalendo kwa sababu ya kusema ukweli kwani wanataka uridhike na hali halisi ya ujinga tulio nao.
 
Labda tuwaombe kamati ya Olympics waongeze mashndano ya kubwabwaje! Huenda tukapata Gold hapo!
 
sisi ni manenozz... wangeweka ata shindano la kusutana kwenye olimpik jaman angalau tungeondoka na medali moja
 
nimefuatilia mashindano ya olympics mwanzo hadi mwisho, naiunga mkono 100% eti mwanariadha tegemeo ni samson ramadhani kamaliza wa 66 its a shame... nilikuwa nafuatilia mada ya olympics juzi kwenye kituo cha KTN kenya guys wako serious na haya mambo, sio hawa wenzangu na mie wanaoona ufahari kwenda kupiga picha na 50% siku si tutaona picha hapa mhishimiwa akiwa na USAIN BOLT sitashanagaa kwa sababu ubinafsi uko mbele utaifa umekufa ndio tuna lundo la wanaobwabwaja tu... mchawi aliyeturoga keshakufa...
 
Tanzania Tulipeleka viongozi na wake zao kufanya matembezi, kuna mmoja wapo mkewe kaugulia huko na ikawabidi kumrudisha kabla ya m,ashindano kuisha ili kumtibu TZ. Futa michezo yote na kuanzisha ligi ya UONGO NA MAJUNGU ndio tuwezalo.
 
Mnakumbuka ile katuni iliyokuwa imechapwa kwenye gazeti la Kenya ikonesha wana habari wa Tanzania wakilamba viatu vya JK. Ililalamikiwa sana ingawa ilikuwa na ukweli fulani. Sasa imewekwa katuni kwenye gazeti la The East African kama ilivyo hapa chini. Sijui tena tukasirike au tukubali ukweli?

Walifanya Haraka... UGANDA imepata GOLD ya Marathon iliwaacha Wakenya Mbaali Sana
 
Tafsiri yangu, Tz blah blah, Rwanda...dada kapendezaaa ila amesinzia, Burundi hata sura hatambuliki ni mavazi tu, Uganda mbabe kifua mbele kafanikiwa ingawa anapiga mluzi mmoja (medali moja?) na huku mkenya ingawa kapata medali ameshapigika sana katika fani zake...k.m marathon, 5000 women etc...anaona sooo.....
 
Huyu jamaa ana akili sana. Ni kweli kuwa sisi tuna rundo la medali za blah blah.
 
[

Pia tuwaelewe wakenya kwamba siyo washirika wetu. ni wapinzani na washindani wetu. Tz hatujawachora kwa upuuzi wao wa kuingia Somalia kwa sababu ya wazungu wawili tu waliotekwa nyara. sasa hivi wanalizwa kila kona ya Nairobi.
[/QUOTE]

Huyo mchoraji ni Mtanzania anayefanyia kazi Kenya. Lakini ukweli ameupatia vizuri kabisa. Tunapata medali kwa maneno mengi yasiyo na pointi. Kikubwa kabisa, wananchi tunashindwa kuwawajibisha wote waliopewa dhamana ya uongozi au hata matayarisho ya timu ya olimpiki. Tunaye mtu ambaye interest yake si hali bora ya wananchi bali his oversized humongous ego. Cross him (tena in very trivial and most inconsequential things), and you will end up in jail for life.
 
Back
Top Bottom