Gazeti la Tanzania Daima linamilikiwa na Mhe. Mbowe?

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Kumekuwa na tafsiri tofauti kati ya watu kuhusiana na Gazeti la Tanzania Daima, wengi wakiamini kwamba limekuwa likimsafisha Rostam Aziz katika suala la Dowans. Watanzania wengi watafuta habari wanaamini kwamba Mheshimiwa Mbowe ni mmiliki wa hili gazeti. Nadhani ni wakati muafaka kwa Mhe. Mbowe kueleza wazi kama bado analimiliki gazeti husika au la. Maana hata kama anaruhusu liwe na uhuru wa kutoa habari, kwa kweli hapa linapingana na itikadi yake ya kupambana na ufisadi (ambayo twaamini ndiyo itikadi yake). Kama kweli gazeti hili lipo chini ya Mbowe basi atakuwa anatuchezea akili zetu.
 
Mkuu kweli umeongea point ya maana , Mbowe kama kiongozi wa Chama kinachompinga RA kwa nguvu kubwa kwenye suala la Ufisadi ni kinyume kabisa kwa gazeti hilo kuwa na habari ambazo hazina kichwa wala miguu, tatizo watu tunafikia hatua ya kujaji Mbowe na wala sio Tanzania Daima

au yameshamkuta yaliyomkuta Mtikila?
 
Gazeti la Tanzania Daima linamilikiwa na kampuni ya Mbowe. Lakini Mbowe hajihusishi na day to day running of the paper au hata day to day running of the company. Nadhani mtu wa kulaumiwa hapa ni managing editor ambaye anaruhusu makala kama hizo kuchapishwa gazetini.
 
Kumbuka Tanzania Daima linafata mahadili ya kiuandishi hivyo aliwezi kuwa bias!
 
Ni kweli Mkuu lakini Litamwaribia Mbowe,
watu wameshajua wamiliki wa Vyombo vya habari wanavyocontrol vyombo vyao, Mfano Mengi na IPP yake, Rostam na RAi, Mtanzania, JK na TBC na Daily news

Hivyo ni vigumu sana kwa mtu wa kawaida kuelewa kuwa Mbowe kawapa uhuru hao wanaoendesha hilo gazeti, na kingine kikubwa hilo gazeti lilishajulikana ni la mlengo gani kwa hiyo linapobadilika basi kuna kitu
 
Kumekuwa na tafsiri tofauti kati ya watu kuhusiana na Gazeti la Tanzania Daima, wengi wakiamini kwamba limekuwa likimsafisha Rostam Aziz katika suala la Dowans. Watanzania wengi watafuta habari wanaamini kwamba Mheshimiwa Mbowe ni mmiliki wa hili gazeti. Nadhani ni wakati muafaka kwa Mhe. Mbowe kueleza wazi kama bado analimiliki gazeti husika au la. Maana hata kama anaruhusu liwe na uhuru wa kutoa habari, kwa kweli hapa linapingana na itikadi yake ya kupambana na ufisadi (ambayo twaamini ndiyo itikadi yake). Kama kweli gazeti hili lipo chini ya Mbowe basi atakuwa anatuchezea akili zetu.
Huo ndio uongozi tunaoutaka hata kama kampuni ni yako hakuna kuingilia uendeshaji na maadili ya waandishi, gazeti liko neutral hadi watu wanashindwa kuelewa hiyo ni dalili nzuri kwa gazeti siyo kama Mtanzania au RAI au hata HabariLeo la umma magazeti ambayo unaweza ku-predict kesho yataandika nini.
 
Mkuu sio kwa Tanzania na kwa Watanzania, siasa za Tanzania zinaenda mbali sana
 
Ni kweli Mkuu lakini Litamwaribia Mbowe,
watu wameshajua wamiliki wa Vyombo vya habari wanavyocontrol vyombo vyao, Mfano Mengi na IPP yake, Rostam na RAi, Mtanzania, JK na TBC na Daily news

Hivyo ni vigumu sana kwa mtu wa kawaida kuelewa kuwa Mbowe kawapa uhuru hao wanaoendesha hilo gazeti, na kingine kikubwa hilo gazeti lilishajulikana ni la mlengo gani kwa hiyo linapobadilika basi kuna kitu
Sidhani kama hiyo mifano ndiyo bora kwako unataka Mbowe awe anaonekana front page kila siku kama Mengi kwenye ITV na Nipashe that is not good leadership.
 
Kumbuka Tanzania Daima linafata mahadili ya kiuandishi hivyo aliwezi kuwa bias!

Sawa. Lakini gazeti lazima liwe na msimamo wake kuhusu masuala mbali mbali kama vile ufisadi. T. Daima linajitambulisha vipi kuhusu ufisadi?
 
Mkuu sio kwa Tanzania na kwa Watanzania, siasa za Tanzania zinaenda mbali sana
Du ni kweli kabisa mboa huyo Rostam magazeti yake hayaandiki habari za Mbowe au Chadema? km kuuza sio huko.
Kwa Mbowe hata Club Billicana (zamani R.S.V.P.) kwa vile haingii kucheza Disco basi aiachie ifanye madudu hata kuuza unga?
Lazima awe km Rostam waandishi na wahariri (kina Kibanda) lazima wawe na muelekeo wa Bosi wao na kuwachukia wapinzani km wafanyavyo magazeti ya Uhuru, Mzalendo
 
Sawa. Lakini gazeti lazima liwe na msimamo wake kuhusu masuala mbali mbali kama vile ufisadi. T. Daima linajitambulisha vipi kuhusu ufisadi?

Makala yanaweza yakawa ni utafiti fulani au maoni ya mtu na siyo 'hard news'!
 
Mbowe kazi unayo fanya maamuzi ukijua kibanda ataondoka na waandishi wake ambao tayari wanashirikiana kuandaa jarida la umoja . Kila siku mnamlazimisha kikwete afanye maamuzi magumu leo zamu yako fanya maamuzi kwa ustawi wa kampuni yako
 
Kibanda bado anafaa kuendelea kuliongoza gazeti hilo hatan kama yeye ni rafiki wa mafisadi!1 Kitu ambacho Mbowe anapaswa kuwa makini nacho ni kutokuingizwa kwa urafiki wa Mhariri Mtendaji kwenye kazi zake. Tusikosee au kuchanganya mambo kama wana CCM wanavyo fanya, Gazeti la Tanzania daima siyo mali ya CHADEMA na wala si lazima gazeti liegemee CHADEMA!
 
Sawa. Lakini gazeti lazima liwe na msimamo wake kuhusu masuala mbali mbali kama vile ufisadi. T. Daima linajitambulisha vipi kuhusu ufisadi?

Ni kweli mkuu. Kila gazeti linakuwa na dira yake. Na hiyo dira huanzishwa na mmiliki. Kama mmiliki alilianzisha gazeti lake kwa malengo ya kufuata dira A na akamtafuta msimamizi ambaye kwa bahati mbaya kaleta dira B inayokinzana na dira A hapo basi hana budi kumfukuza huyo msimamizi; lakini kama utazidi kuziba masikio na kukubali aendelee kuongoza gazeti lako japo amebadirisha malengo yako ya awali bila shaka na wewe utakuwa umebadirisha dira. Huwezi ukawa wamlaumu RA kwa suala la Dowans kwenye majukwaa na wakati huo huo gazeti lako linatoa sumu kwa wananchi. Lazima uwe upande mmoja, ama upo upande A au upande B. Huwezi ukawa vuguvugu kwa kuruhusu kampuni yako kuendelea kukusanya pesa tofauti na imani yako. Ni sawa na Sheikh mkuu/askofu kuwa na kiwanda cha bia. Kwa hilo Mhe. Mbowe inatakiwa ajitambulishe yuko upande gani. Yasije yakawa mambo ya akina Mtikila bwana. Aseme anaamini nini? Na Je, gazeti la Mtanzania Daima ni lake?
 
Kumbuka Tanzania Daima linafata mahadili ya kiuandishi hivyo aliwezi kuwa bias!

KakaKiiza binafsi naamini kuwa biased ni pale pande zote mbili zinapokuwa na haki na wewe ukaegemea upande mmoja au pia hata pale upande mmoja ukiwa na haki wewe wataka kuupa haki upande usiokuwa na haki.
 
Makala yanaweza yakawa ni utafiti fulani au maoni ya mtu na siyo 'hard news'!
Mchungaji/Sheikh asijeuza cocaine kwa malengo ya kutaka kujua waumini wake wangapi wanatumia hiyo kitu!!!
 
Gazeti la Tanzania Daima linamilikiwa na kampuni ya Mbowe. Lakini Mbowe hajihusishi na day to day running of the paper au hata day to day running of the company. Nadhani mtu wa kulaumiwa hapa ni managing editor ambaye anaruhusu makala kama hizo kuchapishwa gazetini.

Mkuu kwa hiyo Mbowe kazi yake ni kupokea pesa ya gazeti tu, basi tutajie jina la huyo managing editor unaesema anaruhusu makala kama hizo za kusafisha mafisadi kuchapishwa gazetini, siku moja tutaona Makamba na Tambwe wanasifiwa na Tanzania Daima
 
Mbona kishatajwa humu kwenye hizi threads?
 
kibamba anamwamini lowasa na rostamu, pia magufuli yuko kwenye pay roll za hawa watu, itachukua muda sana kwa mbowe kufahamu hayo. mie siku izi sinunui tena hili gazeti
 
Watu wenye pesa kam lowassa na rostam nawaamini sana kwa kununua watu aina ya kina kibanda.kina deo balile wako wapi?yawezekana kibanda ameshanunuliwa na hao.salva hakununuliwa?shoo hakununuliwa?gazeti hilo laweza kupoteza mwelekeo.t daima,mwananchi na mwanahalisi ni kati ya magazet yanayouzika kinoma huku mitaani.
 
Back
Top Bottom