Gazeti la tanzania daima kulikoni?

Gazeti la tanzania daima kulikoni?

segwanga

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
2,788
Reaction score
731
Gazeti letu maarufu la Tanzania daima sijaliona kwa muda wa siku mbili yaani jana na leo. Jana sikulipata mitaa niliyotembelea,mbezi,ubungo,posta na mwenge. Leo pia sijalipata mitaani mbezi,ubungo,kariakoo na ubungo. Kuna nini kimelisibu hili gazeti maarufu hapa nchini?. Lisipokuwepo gazeti la magamba a.k.a uhuru litatamalaki kwa propaganda zake bila kujibiwa. Je vipi huko mtaani kwako umeliona tanzania daima? Tupeane taarifa!
 
Ni gazeti dume lililobaki hivyo linasomwa sana na magamba wanachangia kwa kulinunua kwa wingi ili lisisambae. Wito kwa wenye gazeti hili wafuatilie usambazaji wake na uwepo wake mtandaoni uimarishwe.
 
ccm wamenunu copy karibu zote ili watu wasijue kinachoendelea
 
Habari zinazo andikwa nyingi huwa mwiba kwa serikali na viongozi wake, hivi karibu habari za mtekaji wa Ulimboka zilivyo fululiza, na hii ya Jk kukaliwa kushatkiwa kwa umoja wa mataifa nazo sio habari nzuri sana kwa magamba!
 
Gazeti letu maarufu la Tanzania daima sijaliona kwa muda wa siku mbili yaani jana na leo. Jana sikulipata mitaa niliyotembelea,mbezi,ubungo,posta na mwenge. Leo pia sijalipata mitaani mbezi,ubungo,kariakoo na ubungo. Kuna nini kimelisibu hili gazeti maarufu hapa nchini?. Lisipokuwepo gazeti la magamba a.k.a uhuru litatamalaki kwa propaganda zake bila kujibiwa. Je vipi huko mtaani kwako umeliona tanzania daima? Tupeane taarifa!
Mkuu kutoka na habari zilizo andikwa kwenye gazeti hilo siyo rahisi kulipata ukissubiri ifike saa saba soma online lakini lilikuwepo...
 
Mbona mmelisifia sana. Nitalitafuta nilisome nione huu ujogoo wake. Maana wengi walidhani kuwa kufungiwa kwa Mwanahalisi basi uandishi nao ulikuwa umefungiwa.
 
Mimi nalipata mtandaoni. Nadhani labda linauzika sana kiasi ambacho halibaki, au kuna watu wanayanunua yote ili yasisomwe.

Tanzania Daima - Sauti ya Watu

Eebwana wee,nimecheki kutumia hyo link uliyotoa,aisee! Kuna habari zinazoichoma kumtima serikali ya magamba. Kuna mauaji mengine mabwepande,na mateso ya dk ulimboka na mauaji ya mwandishi daudi mwangosi yamemponza daktar kikwetwe! Du kazi anayo sijui atakuwa anaenda kubembea wapi maana kwa obama wameshazinasa habari za mauaji na utesaji
 
Mkuu gazeti lipo ila yawezekana wakulu wamenunua copy zote mtaani..........
 
Habari zinazo andikwa nyingi huwa mwiba kwa serikali na viongozi wake, hivi karibu habari za mtekaji wa Ulimboka zilivyo fululiza, na hii ya Jk kukaliwa kushatkiwa kwa umoja wa mataifa nazo sio habari nzuri sana kwa magamba!

Hii ni kweli nami leo nimelitafuta sana tegeta, wanasema wiki hii linanunuliwa sana, hila nimelipata kumbe lipo sana Ulimboka ndiye anayewatesa magamba.
 
si kweli kwamba limenunuliwa na magamba. habari za ulimboka ziliwavuta wengi hata wale ambao hawana utamaduni wa kununua gazeti. wananua kwa haraka na kuisha.
 
Mnafanya promo enh? Endeleen.lingekuwa linauza kihvyo waandishi wao wasingekuwa wanadai mishahara hadi leo,kaulize utajuta kumfahamu mmiliki wake mana ndo anayelaumiwa kwa kuhamisha mapato ya free media kupeleka ktk biz zingine.linatolewa copy chache sana nowdayz.subirin taratibu litajiondoa sokon labda liuzwe
 
Back
Top Bottom