Gazeti la Mwananchi jaribuni kumheshimu Rais, kampeni zimeshaisha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Ni Gazeti ambalo tokea mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais wa CCM ulipoanza na hadi alipopatikana Dkt. Magufuli na hata kipindi chote cha Kampeni na kama haitoshi mara baada ya ushindi wa Magufuli na kutawazwa kwake kuwa Rais bado tu hili Gazeti lilionyesha dhahiri shahiri kuwa linatumika vibaya Kisiasa kwa maslahi ya huyo au hao wanaomtegemea / wategemea.

Kama Wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa kiuandishi wa hili gazeti la MWANANCHI utakubaliana nami kuwa hili gazeti lina CHUKI ILIYOKOMAA dhidi ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli kwani hata kama akifanya JEMA gani kesho yake MWANANCHI hawataandika KIUELEDI zaidi ila watakuja na reporting ya KINAFIKI na KIUCHOKOZI.

Kilichonisikitisha hasa ni kitendo cha Kichwa cha Habari cha gazeti la MWANANCHI la leo tarehe 2, May 2016. Jana ilikuwa ni MEI mosi ambapo kitaifa ilifanyika Mkoani Dodoma ambapo pia ndipo Makao Makuu ya nchi yetu ambapo Mheshimiwa Rais Magufuli aliweza kutoa Hotuba yake ambayo ilionyesha dira yake KIUTENDAJI kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Rais jana alizungumza mengi sana lakini kama ilivyo ada wengi wetu tulikuwa tumetega masikio kusikia kama Mishahara na fursa zingine zitaongezeka vitu ambavyo Rais alivitolea UFAFANUZI mzuri tu hadi kila Mtu akaridhika.

MAUDHI kama siyo KERO ya KIUELEDI leo MWANANCHI wamekuja na Kichwa cha Habari kwa kusema PAYE imepunguzwa kwa Tsh 1,100/= tu. Kila siku Watanzania tunasisitizana kuwa tuweke UZALENDO kwa nchi yetu hivyo nikajiuliza mno maswali kwamba au kwakuwa Management nzima ya MWANANCHI COMMUNICATION LIMITED 85% ni WAKENYA

Nilikuwa najiuliza kila siku kwanini Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mkogwe katika TASNIA ya Uandishi wa Habari Richard Mghamba aliamua kuondoka MCL na kurudi zake IPP Media ambapo sasa ndiyo Executive Editor / Managing Editor. Kwa ninavyomjua Richard Mghamba alivyo MWELEDI na anaijua vizuri sana FANI yake ukiona anaachana na Ofisi au Kampuni fulani jua hapo alipotoka kuna UOZO wa hali ya juu.

MWANANCHI hamjamtendea HAKI Mheshimiwa Rais na Watanzania kwa aina yenu ya Kichwa cha Habari mlichokiweka leo. Japo siyo Economist ila sidhani kama punguzo la PAYE alilolisema jana Mheshimiwa Rais la kutoka 11% hadi 9% ni sawa sawa na hiyo Tsh 1,100/= mliyoiandika leo. Binafsi mmenisikitisha mno na naanza sasa kutilia shaka PROFESSIONALISM yenu na yawezekana ikawa hali hii ndiyo hata imesababisha waliokuwa Waandishi wenu wa Habari MAHIRI kama Alex Bitekeye, Edward Qorro, Ibrahim Yamola, Lasteck Alfred, Aidan Mhando na wengineo wengi tu wameachana na nyie na sasa wanafanya vizuri sana huko waliko.

Tafadhali msituletee, wenu hapa na Mheshimiwa Waziri Nape anza sasa KULIMULIKA hili Gazeti na ikibidi hata Kampuni yao yenyewe ili baadae hili gazeti lisije kusababisha kilichoikumba nchi ya Rwanda mwaka 1994 kulikofanywa na Redio ya UCHOCHEZI iliyokuwa ikiitwa RTLM ( Radio Transmission Le Milcoline ) ambayo ilikuwa chini ya MHUTU aitwae Rwegosora ambaye sasa anatumikia Kifungo cha maisha alichohukumiwa na ICTR.

Nawasilisha!
 
Mkuu umenena kile ambacho hata mimi nimekuwa nikikiwaza!
Nina mashaka Na dhamira ya hili gazeti kwa nchi yetu!
Hii sio mara ya kwanza au ya pili!
Kuna agenda behind what we see!
Nadhani sio Nape tu wa kuachiwa jukumu la kuwafuatilia nadhani watu wa usalama nao walifuatilie kwa ukaribu!
 
mtoa mada labda ww sio mfanyakazi au mwathiriwa wa PAYE,,,chati nzima imekaa kinyonyaji na inatakiwa kufumuliwa yote,,hata wakishusha mpaka 5 bado effet ndogo kama hiyo chati haijafumuliwa,,mwenye mshahara mkubwa anatakiwa akatwe zaidi kuliko mwenye mshahara mdogo,,haiwezekani mwenye laki saba akatwe sana na wa million 30
 
Mkuu, huenda walimaanisha kuwa kuna ngazi fulani ya mshahara ambayo punguzo la 2% ni shilingi 1,100/=.
 
Mleta uzi porojo nyingiii hivi hilo gazeti kuandika ukweli ndo uchochezi? Kwanini usiwakemee uvccm na kabango kao kule zenji MACHOTARA. Mbona hukuibuka na kulaani. Sasa hao waandishi walohama mwananchi walienda gazeti la uhuru na habari leo? Kwa hiyo mnataka kutugeuza mandondocha hakuna kuhoji,
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli, namba hazidanganyi. Kama mnataka apambwe na sifa zakijinga yapo magazeti yanafanya kazi hiyo kma uhuru,habari Leo, Daily noise, tazama nk. Kanunue hayo usome ufurahi Kama mvutabangi anavyofurahia vitu visivyokuwepo
 
....
MWANANCHI hamjamtendea HAKI Mheshimiwa Rais na Watanzania kwa aina yenu ya Kichwa cha Habari mlichokiweka leo. Japo siyo Economist ila sidhani kama punguzo la PAYE alilolisema jana Mheshimiwa Rais la kutoka 11% hadi 2% ni sawa sawa na hiyo Tsh 1,100/= mliyoiandika leo. Binafsi mmenisikitisha mno na naanza sasa kutilia shaka PROFESSIONALISM yenu na yawezekana ikawa hali hii ndiyo hata imesababisha waliokuwa Waandishi wenu wa Habari MAHIRI kama Alex Bitekeye, Edward Qorro, Ibrahim Yamola, Lasteck Alfred, Aidan Mhando na wengineo wengi tu wameachana na nyie na sasa wanafanya vizuri sana huko waliko.

......
Nawasilisha!
Asante kwa kutujuza kadhia hii ya mwananchi.
Lakini na wewe unapotosha watanzania . PAYE imetoka 11% na kurudi 9% wala hakurudi 2%. Pili imegundilika kuwa PAYE itawanufaisha wale wenye mishahara kuanzia TZS. 720,000/= kurudi chini. Wale wa juu yake hawahusiki na punguzo hili la PAYE. Vinginevyo kuwe kumetolewa taarifa nyingine.
 
Wahariri wengi wa gazeti la Mwananchi ukiwafuatilia mmoja mmoja ni watu wenye chuki dhidi ya serikali. Wengine nawafahamu huwa naona comment zao kwenye mitandao ya kijamii. Lakini pia kwa kiasi kikubwa wamejisahau na kudhani wao ni Wakenya kumbe ni watanzania. Inabidi kuchunguza pia uraia wa baadhi yao kwani wanatoka mpakani na Kenya.
 
Back
Top Bottom