TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
LEO 07/12/205 gazeti la Mwanahalisi kwenye ukurasa wa mbele limeandika kichwa cha habari kinachosema "MAWAZIRI WAVUJA" huku kukiwa na picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli na picha watu wanane, wakiwa Wabunge na wengine wasiyo Wabunge kuwa ni miongoni mwa Mawaziri wateule katika baraza la Mawaziri atakaloliunda rais.
Mwanahalisi hawana jipya hapa. wanatafuta tu sifa na jambo la kusema pindi tu Rais atakapotangaza bazara la mawaziri.
Pamoja na mambo ambayo wataandika baada ya baraza kutangazwa yatakuwa ni:
1. Rais amepangua baraza na kuja na majina mapya baada ya yale ya awali kuvuja na kuandikwa na gazeti hili(MWANAHALISI). Huu utakuwa ni upuuzi mtupu, yaani rais ajichimbie takribani mwezi mmoja kwa lengo la kujiridhisha na aina ya watu anaowataka halafu, kwa sababu tu MWANAHALISI limewaandika awaache?
2. MWANAHALISI lilishaandika majina haya kuwa ni miongoni mwa baraza la Mawaziri. hii ni endapo baraza atakalolitangaza rais, majina hayo yatakuwemo. MWANAHALISI wanafanyakazi kwa kubahatishabahatisha tu, kutafuta sifa sifa tu kuwa ni wachunguzi.
LAKINI lengo hasa la MWANAHALISI kufanya hivi na kutaja mjina hayo 8 ni nini? Baraza la Magufuli lina Wizara 8 tu? mbona hawajataja baraza zima? hapa MWANAHALISI hawana jipya, malengo hapa ni mawili tu:
1. wana mambo yao binafsi na hayo majina manane(8) na kwa namna moja au nyingine kutaka kuonesha kuwa wanafaa kuwa kwenye baraza la Magufuli au hawafai.
2. wanataka tu kuionesha Serikali ya MAGUFULI ambaye anakenda na kasi ya ajabu katika utendaji wake kuwa ama iko makini au haiko makini. kwa kifupi ni kutaka tu kuikosoa kupitia ujumbe wake kwa wananchi.
TAFAKURI: MWANAHALISI wanapaswa kujitafakari kwa kina hususani katika kuwahabarisha wananchi. Hii serikali ya awamu ya Tano watanzania wana imani kubwa sana nayo na wako tayari kuiunga mkono kwa kila jambo linalolenga kuwaletea watanzani maendeleo. Propaganda za kijinga kama ambazo wanaanza kuzianzisha zimeshapitwa na wakati. Siyo muda tena wa kuwaaminisha watu mambo ambayo hayana tija kwa taifa.
MWANAHALISI wamuache RAIS AANDAYE BARAZA LAKE LA MAWAZIRI, Rais Magufuli siyo wa MAGAZETI wanajisumbua bure.