Gazeti la mwana halisi linastahili pongezi!

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
5,711
Reaction score
1,914
Ndugu zangu wana JF mtu akifanya kazi nzuri anastahili pongezi. Tena ikiwa kazi ya utaalam anapewa award. Hili gazeti la mwana halisi linafanya kazi nzuri kabisa,hata kama ni biashara, maana linafanya watu in certain quarters hawalali.

Hiyo inaitwa investigative journalism ya Bwn Kubenea and company.

Hivyo nawaomba wana JF Hawa vijana tuwatie moyo kwa kazi hii ya kujituma na risk. Kumbuka yeye na Ndg yangu Ndimara waliwahi kumwagiwa tindi kali!!!!!!! Huo sio utani maana yake ilikuwa nia ya wahujumu ni kuwapofusha macho ili wasione waache kuandika. Lakini wanazidi kufukua uozo zaidi na hawana woga wa kutaja mafisadi wahusika moja kwa moja.

Isiwe wanapigana vita ya peke yao kumbe tutafaidi Watanzania wote tukishinda, bila kujali dini kabila wala chama cha siasa. Tuwapongeze tafadhari tubuni mbinu ya kuwatia moyo!!!!!!!!!!!!!!!! (Soma; Mwana Halisi Na.227 Juma Tano Feb 2-8, 2011)
 
Kuna habari gani ya kichunguzi toleo la leo.
 
Hawa ni miögon mwa watz wanaopgana kw vitendo sabab kuinvestgate na kutoa habar kama hiz yataka moyo,we hav to suport them my felw great thinkers.
 
wamefanya kazi yao,pongezi ya nini.Watanzania tunapotea kwa kukosa maarifa kidogo,hiyo ndio kazi ya gazeti magazeti yanatakiwa yaige hapo sasa ukisema pongezi tena maana yake unaondoa uhalisia wa kazi za gazeti.HIYO NI KAZI YAO NA HAWAHITAJI PONGEZI YOYOTE
 
Mi huwa nawakubali mwanahali.kimsingi huwa naona tunamagazet 3.mwananch,nipashe na mwanahalisi ambalo mpaka sasa halina mpinzani
 
Ndugu zangu wana JF mtu akifanya kazi nzuri anastahili pongezi. Tena ikiwa kazi ya utaalam anapewa award. Hili gazeti la mwana halisi linafanya kazi nzuri kabisa,hata kama ni biashara, maana linafanya watu in certain quarters hawalali.
Hiyo inaitwa investigative journalism ya Bwn Kubenea and company.
Hivyo nawaomba wana JF Hawa vijana tuwatie moyo kwa kazi hii ya kujituma na risk. Kumbuka yeye na Ndg yangu Ndimara waliwahi kumwagiwa tindi kali!!!!!!! Huo sio utani maana yake ilikuwa nia ya wahujumu ni kuwapofusha macho ili wasione waache kuandika. Lakini wanazidi kufukua uozo zaidi na hawana woga wa kutaja mafisadi wahusika moja kwa moja.
Isiwe wanapigana vita ya peke yao kumbe tutafaidi Watanzania wote tukishinda, bila kujali dini kabila wala chama cha siasa. Tuwapongeze tafadhari tubuni mbinu ya kuwatia moyo!!!!!!!!!!!!!!!! (Soma; Mwana Halisi Na.227 Juma Tano Feb 2-8, 2011)

Pamoja na kutishiwa mara kadhaa vikiwemo vyombo vya usalama lakini bado wanapambana kwa manufaa ya watanzania wote, wapo radhi kufa kwa kutetea haki, hawapo kibiashara zaidi kama tunavyoona vyombo vingine vya habari. Mungu aendelee kuwabariki watu hawa na kwa hakika sauti zao zitakuja kuleta tija.
 
Ndugu zangu wana JF mtu akifanya kazi nzuri anastahili pongezi. Tena ikiwa kazi ya utaalam anapewa award. Hili gazeti la mwana halisi linafanya kazi nzuri kabisa,hata kama ni biashara, maana linafanya watu in certain quarters hawalali.
Hiyo inaitwa investigative journalism ya Bwn Kubenea and company.
Hivyo nawaomba wana JF Hawa vijana tuwatie moyo kwa kazi hii ya kujituma na risk. Kumbuka yeye na Ndg yangu Ndimara waliwahi kumwagiwa tindi kali!!!!!!! Huo sio utani maana yake ilikuwa nia ya wahujumu ni kuwapofusha macho ili wasione waache kuandika. Lakini wanazidi kufukua uozo zaidi na hawana woga wa kutaja mafisadi wahusika moja kwa moja.
Isiwe wanapigana vita ya peke yao kumbe tutafaidi Watanzania wote tukishinda, bila kujali dini kabila wala chama cha siasa. Tuwapongeze tafadhari tubuni mbinu ya kuwatia moyo!!!!!!!!!!!!!!!! (Soma; Mwana Halisi Na.227 Juma Tano Feb 2-8, 2011)

mkuu kuna habari gani mkuu, huku mikoani bado halijafika, nitupie headline
 
Thumbs up to these fellas, seriously. When we talk of investigative journalism in Tanzania - Kubenea is soaring in his own distinguished planet. Thumbs up to Kubenea, Joster Mwangulumbi, Ezekiel Kamwaga, Ndimara and of course MwanaHALISI in its entirety. Bila kusahau Raia Mwema's gurus like the likes of General, Mbwambo, Rioba etc. These guys are significantly taking journalism discipline into higher levels. Those aspiring to be in this industry should considerably role-model these astute.
 
Hata kama ni kazi yao wanastahili pongezh. Mtuyoyote anapofanya au kutimiza wajibu wake vizuri anapongezwa, ndio maana hata maofisini kuna zawadi na tuzo ya mfanyakazi bora. WAO wanatimiza wajibu wao vizuri hivyo wanastahili PONGEZI. Na wale wasiotimiza majukumu yao vizuri tunawapa vidonge vyao kama tulivyowahi kufanya kwa habari leo,uhuru,mtanzania na tanzania daima walipopotosha habari ya sitta/mwakyembe na dowans.
 
Kubenea (km kiongozi wa kundi) na Timu nzima ya Mwanahalisi ni wapiganaji....kazi yao itabaki milele!
 
wamefanya kazi yao,pongezi ya nini.Watanzania tunapotea kwa kukosa maarifa kidogo,hiyo ndio kazi ya gazeti magazeti yanatakiwa yaige hapo sasa ukisema pongezi tena maana yake unaondoa uhalisia wa kazi za gazeti.HIYO NI KAZI YAO NA HAWAHITAJI PONGEZI YOYOTE

mtu akifanya vizuri mpongeze, kwani wasipofanya utawalaumu, mbona magazeti mengine hayafanyi hivyo?
 
quote_icon.png
Originally Posted by son of soil
wamefanya kazi yao,pongezi ya nini.Watanzania tunapotea kwa kukosa maarifa kidogo,hiyo ndio kazi ya gazeti magazeti yanatakiwa yaige hapo sasa ukisema pongezi tena maana yake unaondoa uhalisia wa kazi za gazeti.HIYO NI KAZI YAO NA HAWAHITAJI PONGEZI YOYOTE
mtu akifanya vizuri mpongeze, kwani wasipofanya utawalaumu, mbona magazeti mengine hayafanyi hivyo?

Mtamalizana kwenye jukwaa la lugha ila ujumbe umefika...
 
Mtu anapofanya vizuri ni ungwana kumpongeza, Mwanahalisi wanastahili pongezi za dhati. Pamoja nao wapo Raia Mwema na Mwananchi bila kusahau the East Africa ambao ndio walioiweka vizuri article kuhusu Dowans na Rostam Azizi katika toleo lao la Jumatatu hii.

Hiyo habari ipo wazi kwenye hukumu ya ICC inayotutaka tumlipe huyo ponjoli hiyo 94bn/=, lakini magazeti mengine yamekazania personalities za kina Sitta, Mwakyembe vs Lowasa na Rostam badala ya kuzama kwenye hukumu kisha mtu aje na article iliyoenda shule kama hiyo ya East Afrika Jumatatu na Mwanahalisi leo. Raia Mwema ya leo bado sijaiona.

Article ya East Africa na Mwanahalisi katika matoleo yao ya wiki hii kuhusu Rostam na Dowans ni ujumbe tosha kwa magazeti mengine nchini, hususani Tanzania Daima ambalo hivi sasa limejibainisha kuwa kundi moja na kina habari leo, uhuru, mtanzania na raia. WAANDISHI WA HABARI BADILIKENI, jifunzeni kwa wenzenu Mwanahalisi, Raia Mwema, Mwananchi na East Africa
 
wamefanya kazi yao,pongezi ya nini.Watanzania tunapotea kwa kukosa maarifa kidogo,hiyo ndio kazi ya gazeti magazeti yanatakiwa yaige hapo sasa ukisema pongezi tena maana yake unaondoa uhalisia wa kazi za gazeti.HIYO NI KAZI YAO NA HAWAHITAJI PONGEZI YOYOTE

Mtu akifanya kazi vizuri hupongezwa hata kama ni kazi yake. Kwa mwanahalisi ni dhahiri wanahitaji pongezi maana wanafanya kazi kwa namna ambayo wengine wameshindwa.
 
Sijaona walichoandika leo lakini natoa pongezi za dhati kwa ujasiri na uzalendo wao, naamini kama ni hela wangezipata nyingi kwa kuwa upande wa Rostam na watu wa aina yao. Kwa kuamua kuwa upande wetu, upande wa hatari na mgumu, watalipwa na riba kubwa ikifika siku ya malipo yao.

BIG UP SAED na timu yako, Mungu anaiona kazi yenu na atailipa kadri mnavyostahili... Kazeni buti
 
Mi huwa nawakubali mwanahali.kimsingi huwa naona tunamagazet 3.mwananch,nipashe na mwanahalisi ambalo mpaka sasa halina mpinzani

mimi nadhani hata RAIA MWEMA wanafanya kazi nzuri nao wanastahili thumb up!
 
Back
Top Bottom