Nimepitia vichwa vya habari vya magazeti yote asubuhi hii, yakiandika kuhusu alichosema Kardinali Pengo kule Mwanza wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu Anthony Mayalla. Wakati magazeti mengi yakiandika kuhusu jinsi Pengo alivyowashukia mafisadi, Mtanzania limesema: 'Pengo aumbua makamanda wa ufisadi'. ukiisoma habari ya gazeti hili unaweza kudhani Pengo naye ni mmoja wa watu wasiotaka vita dhidi ya ufisadi. kwani kwake wanaopinga ufisadi ni wale ambao wamekosa 'opportunity' ya kuwa mafisadi na sasa wanawaonea wivu mafisadi. Kwa bahati mbaya sikumsikiliza Pengo alipokuwa akiongea jana. Nitaamini ninachosoma tu kwenye magazeti. Lakini kauli hii (kama kweli aliitoa) naona ni muhimu ianzishe mjadala.