Habari za Rais mstaafu, Jakaya Kikwete zaliponza gazeti la Mtanzania

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,297
2,000
1480585734407.jpg
Kufuatia gazeti la Mtanzania la Novemba, 20 na 22 kuandika habari ambazo zinamhusu Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuwa alizuiliwa kuondoka katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu nyerere, Serikali imetoa taarifa kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.

Katibu taarifa ambayo imetolewa na Kaimu Msajili wa Magazeti, Patrick Kipangula imesema kuwa taarifa hiyo haina ukweli na ina nia ya kumdhalilisha Kikwete ambaye aliondoka madarakani mwaka jana 2015 na nafasi yake kuchukuliwa na Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli

Hivyo kutokana na kuchapishwa kwa habari hizo, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Magazeti imetoa onyo kwa gazeti la Mtanzania na kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
1480586360078.jpg Chanzo : Dewji blog
 

LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,152
2,000
Serikali yake kila kitu kila jambo wanasingiziwa, hawajawahi kuja kukubali hata siku moja! Hivi kwanini huyu bwana anasingiziwa sana .......
 

MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
Sijui kwanini watu wamekua wazushi sana siku hizi
Kila mtu anajitahidi kuzusha ili mradi watu wamsikilize
Hiyo ndio downside ya utandawazi na social media, kila mtu anatafuta "Scoop"! Baadhi kwa nia njema ya kuhabarisha lakini wengi wao kwa nia ovu ya kudhalilisha wenzao kwa sababu wazijuazo wenyewe hawa mawakala wa ibilisi!
 

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
3,993
2,000
Wizara ya makanusho na matamko inahitajika haraka sana maana wapiga dili wamezidi uzushi!
 

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,080
2,000
kumekucha..................sirikali ndio inaamua kipi ni uongo na kipi ni ukweli
 

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,449
2,000
huu utetezi Wa kipuuzi mlipaswa kueleza ukweli Wa mambo kuliko kung'ang'ania eti ni taarifa za uongo. poor Tanzania
 

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
3,993
2,000
KWA NIABA YA WIZARA YA MAKANUSHO NA MATAMKO NASEMA HIVI HILO GAZETI LIFUNGIWE
 

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,530
2,000
Wanatoaje Onyo kabla ya kuwa- prove wrong

Nani kathibitisha kuwa Mtanzania walidanganya na wao serikali wanasema ukweli? Tanzia bwana, Yaani Kesi umefungua wewe, Mshati wewe, Mwendesha Mashataka wewe na Hakimu wewe Mwenyewe halafu unataka tukuamini???

BACK TANGANYIKA
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,455
2,000
Kuna vitu vya msingi tunataka ufafanuzi na sio hivyo,Leteni ufafanuzi kwanini mmezuia watu wasichukue hifadhi zao za jamii endapo wakiacha kazi wakati hata hiyo sheria mpya haijapitishwa? Fao la kujitoa mmezuia kwa PPF na NSSF mmeweka miezi 6 wakati mwanzo ilikuwa mwezi mmoja tu,je mbona fao la kutokuwa na ajira hakuna? Tupeni ufafanuzi.
 

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,512
2,000
Watafungia kila kitu kilicho ndani ya uwezo wao lkn hawataweza milele
 
Top Bottom