Gazeti la Mtanzania vipi?

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Nimepitia vichwa vya habari vya magazeti yote asubuhi hii, yakiandika kuhusu alichosema Kardinali Pengo kule Mwanza wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu Anthony Mayalla. Wakati magazeti mengi yakiandika kuhusu jinsi Pengo alivyowashukia mafisadi, Mtanzania limesema: 'Pengo aumbua makamanda wa ufisadi'. ukiisoma habari ya gazeti hili unaweza kudhani Pengo naye ni mmoja wa watu wasiotaka vita dhidi ya ufisadi. kwani kwake wanaopinga ufisadi ni wale ambao wamekosa 'opportunity' ya kuwa mafisadi na sasa wanawaonea wivu mafisadi. Kwa bahati mbaya sikumsikiliza Pengo alipokuwa akiongea jana. Nitaamini ninachosoma tu kwenye magazeti. Lakini kauli hii (kama kweli aliitoa) naona ni muhimu ianzishe mjadala.
 
Kwa yoyote aliemsikiliza Pengo gazeti la mtanzania limeandika alichoongea, wamegusa angle zote kuu mbili ya waraka na ya vita vya ufisadi,
 
Mimi mara nyingi nimekuwa sielewi hili gazeti la Mtanzania lina agenda gani na ufisadi unaomaliza taifa hili. Mfano mzuri ni jinsi walivyoandika taarifa ya leo kuhusiana na tamko alilotoa Kardinali Pengo.
Wameandika hivi Pengo aumbua 'makamanda' wa ufisadi

hii ni tofauti kabisa na magazeti karibia yote lakini inabidi hata waandishi wanaondika hizi habari wawe na mtazamo wakuliokoa taifa letu na sio kuweka maslahi mbele tu
 
Hakuna sababu ya kuwa na mjadala sababu gazeti hili linamilikiwa na kiranja mkuu wa ufisadi, Mh. Rostam Aziz
 
Hapo umenena! Labda amesahau kuwa c Ulimwengu anayelimiliki siku hizi ila ni.................
 
Nimepitia vichwa vya habari vya magazeti yote asubuhi hii, yakiandika kuhusu alichosema Kardinali Pengo kule Mwanza wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu Anthony Mayalla. Wakati magazeti mengi yakiandika kuhusu jinsi Pengo alivyowashukia mafisadi, Mtanzania limesema: 'Pengo aumbua makamanda wa ufisadi'. ukiisoma habari ya gazeti hili unaweza kudhani Pengo naye ni mmoja wa watu wasiotaka vita dhidi ya ufisadi. kwani kwake wanaopinga ufisadi ni wale ambao wamekosa 'opportunity' ya kuwa mafisadi na sasa wanawaonea wivu mafisadi. Kwa bahati mbaya sikumsikiliza Pengo alipokuwa akiongea jana. Nitaamini ninachosoma tu kwenye magazeti. Lakini kauli hii (kama kweli aliitoa) naona ni muhimu ianzishe mjadala.

Mimi nilifanikiwa kuangalia shughuli yote kupitia Star TV jana na sijaona sehemu Mtanzania walipokosea, lakini hebu tuangalie magazeti mengine

1. NIPASHE: PENGO ATEMA MOTO MAZISHI YA ASKOFU
- Ahoji kulikoni ufisadi kila kona
- Auliza wapiganaji ni wakweli?
- Aitaka Serikali isiwazonge maaskofu

2. HABARILEO: WARAKA NI NENO LA MUNGU - PENGO
- Asema si lazima Serikali ibariki nyaraka za kanisa
- Asisistiza kelele za 'ufisadi' zitajenga chuki
- Ataka wanaozipiga wajitazame

3. TANZANIADAIMA: PENGO ACHARUKA
- Sasa awageukia wapiganaji wa vita vya ufisadi
- Apasha wasio na dhamira ya kweli wanyamaze
- Aeleza sababu ya ufisadi kutomalizika nchini
- Amshambulia Kingunge kupinga waraka wao

4. MWANANCHI: PENGO AIPINGA CCM
- Ataka Maaskofu wasifundishwe kazi na wanasiasa

Sijui ni magazeti gani hayo unayoyasema yaliyoripoti Pengo kuwashukia mafisadi? Magazeti yote yameripoti alivyohoji dhamira ya hao wanaoshabikia vita ya ufisadi, na ndivyo walivofanya gazeti la Mtanzania, sioni walipokosea, labda kama unataka kuhoji hiyo kauli ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
 
Jamani hakuna haja ya kuwa na mjadala kwa hili maana ni wazi Mtanzania linamilikiwa na Kiranja Mkuu wa Ufisadi, Mh Rostam Aziz.
 
Kuna msemo wa kiingereza unasema "shedding crocodile tears". Unajua mamba akikuvuzia ili akukamate akikukosa uwa analia machozi! Ukimwangalia unaweza ukafikiri anakuonea huruma kwa kulia kwake! Hiyo ndio mantiki ya Kardinali Pengo. Kwamba usikute katika watu wanaopiga kelele za ufisadi kuna wengine wanafanya hivyo kwa vile wamekosa kwenye mgao wa ufisadi (shedding crocodile tears) lakini ndani ya mioyo yao wanautamani ufisadi! That is the gist of Pengo's yesterday's sermon.
 
Kuna kitu kinaitwa Spin, tupebnde kuwaaminisha watu Pengo ameumbua wapiganaji vita. lakini kumbuka alikuwa anauliza dhamira si ya wapiganaji tu ila ya wale wanaostahili kuchukua hatua. Kwamba kila kukicha maovu yanongezeka. hata kama aliuliza wanapiga vita inatoka moyoni kweli au wamekosa nafasi za kula? hii ni kwa sababu kweke haioni matokeo ya kuchukuliwa hatua madhubuti.

Lakini kama mmoja alivyosema hapo juu, kweli kila chombo kina wajibu wake. Kwani mwisho wa siku mbwa hamng'ati bosi wake!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom