Gazeti la majira linapogeuka ""ijumaa"",""sani"";aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la majira linapogeuka ""ijumaa"",""sani"";aibu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Pdidy, Mar 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,719
  Trophy Points: 280
  src
  majira nyuzpepa
  Nudug zangu wa majira nahsi mnaelekea kwa shigongo nowdays ..si vyema kuandika story na kuishia kutaja waziri huyu jina tunalihifadhi..kwenye gazeti kama majira

  Waziri amwaga milioni 60/- kufadhili sherehe za dini  *Yadaiwa lengo ni kujitakasa kwa kanisa urais 2015
  *Waumini watofautina, wasema angetoa Gongolamboto
  *Baraza Kuu UVCCM kuwasha moto, viongozi wakamiana


  Na Mwandishi Wetu

  VIBWEKA vya wanaCCM wanaotajwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka
  2015 vimeanza kwa kasi huku mmoja wa mawaziri akitajwa kumwaga mamilioni ya fedha kufadhili sherehe moja ya kidini.

  Chanzo cha kuaminika kimelidokeza gazeti hili kuwa miongoni mwa mikakati inayofanywa na makada hao sasa ni kuangalia namna wanavyoweza kuteka ngome za kidini kwa lengo la kuungwa mkono kwenye uchaguzi huo.

  Mbali na hilo wanasiasa hao wanajaribu kujipanga kwa kutumia makundi mengine muhimu ndani ya jamii kwa lengo la kuhakikisha wanafanikisha mkakati huo ambao unaonekana kuwa ushindani mkali kutokana na kipindi cha rais wa sasa Jakaya Kikwete kumalizika kwa mujibu wa katiba.

  Chanzo chetu kimedokeza kwamba moja ya maeneo yanayotupiwa macho na wagombea hao katika kuhakikisha wanafanikisha mkakati wao ni kufanya kila linalowezekana ili wakubalike na dini kuu mbili zenye mtandao mkubwa nchini, yaani Waislamu na Wakristo.

  Ili kufanikisha hilo wagombea hao wanadaiwa kujaribu kufanya kila linalowezekana kugusa hisia chanya za dini hizo kwa imani kwamba wanaweza kulamba tufuru kwenye kinyang'anganyiri hicho.

  Katika kile kinachoonesha kuthibitisha mkakati huo, mmoja wa wagombea wanaotajwa kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 anadaiwa kuchangia jumla ya sh. milioni 60 kufanikisha shughuli moja ya kidini inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

  "Tumeshangaa, ni kawaida Wakatoliki tunapokuwa na sherehe mbalimbali tunatoa kadi kwa waumini wetu na watu wengine kuchangia. Michango hii ni ya kawaida kwa kadri mtu alivyojaliwa, hatulaumu lakini inatia wasiwasi kigogo mmoja anatoa sh. milioni 60 kuchangia sherehe za kuwekwa wakfu Askofu wa Jimbo la Dodoma," kilisema chanzo chetu na kuongeza;

  "Michango ya namna hii inapoteza maana yake hata kama mtoaji alikuwa na nia njema. Si makosa watu wakisema huku ni kujaribu kujipendekeza kwa kanisa ili kuungwa mkono kwa madhumuni fulani. Milioni 60 ni fedha nyingi sana kutoa kama mchango tu kwa sherehe za namna hii, kwanini mtu huyu asitoe fedha hizo kwa waathirika wa mabomu Gongolamboto?"

  Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zilisema kuwa kigogo huyo alitoa fedha hizo kwa awamu mbili, kwanza alitoa milioni 45 na baadaye alimalizia sh. milioni 15, jambo ambalo limezua maswali mengi kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo.

  "Inawezekanaje mtu mmoja kuchangia fedha zote hizi kwa shughuli hii? Inawezekana hapa pana ajenda ya kisiasa nyuma yake, ni mbinu za 'kuvalisha kanisa miwani' ili aonekane."

  Majira lilipojaribu kuwasiliana na viongozi wa kanisa hilo kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu zao hazikupatika hewani na zingine ziliita pasi kupokelewa.

  Hata hivyo mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo aliyeomba kutotajwa jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa kanisa hilo alithibitisha kupokewa kwa fedha hizo na kukataa kuzungumzia zaidi suala hilo.

  Mwanakamati mwingine alidai kuwa mchango huo 'wakutisha' kwa sherehe za kawaida kama hizo, unaweza kuligawa kanisa hilo kwa kuonekana linageuzwa kuwa jukwaa la baadhi ya watu kutafuta njia za kukidhi matakwa yao kisiasa.

  Wakati huo huo hali si shwari ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa kile kinachodaiwa kuwepo taarifa za zengwe la kuwang'oa baadhi ya viongozi wake kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja huo unaoatarajiwa kufanyika Jumamosi mjini Dodoma.

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya wanasiasa wamejipenyeza ndani ya umoja huo kwa kuwatumia baadhi ya wajumbe kuhakikisha wanawang'oa viongozi wanaoonekana vikwazo katika kukidhi malengo yao.

  "Tupo macho, ingawa kuna taarifa kwamba baadhi ya watu wana mpango wa kuvuruga UVCCM kwa kuhakikisha viongozi ambao wamekuwa kikwazo katika kutekeleza malengo yao wanawekwa kando," alidokeza mmoja wa wajumbe wa baraza hilo.

  [​IMG]
   
 2. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  No comment
   
 3. c

  core Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napata harufu ya udaku kwa mbaliiii
  :focus:
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  aisee hata mimi nimesoma asubuhi hii nimeshangaa sijalikuta jina la waziri sasa kulikuwa na haja gani ya kuweka front page, mbona wanakuwa kama TBS wameweka habari ya kwanza eeeti kunachama kinadhaminiwa kuleta fujo halafu habari inachunguzwa! sasa unaleta ili wananchi wachunguze au!?
   
 5. Babamzazi

  Babamzazi Senior Member

  #5
  Nov 8, 2013
  Joined: Oct 27, 2013
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Majira hamjiamini na taarifa zenu au mnaogopa kufungiwa kama Mwananchi?
   
 6. Babamzazi

  Babamzazi Senior Member

  #6
  Nov 8, 2013
  Joined: Oct 27, 2013
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa upuuzi kama huu wa majira huna cha kusema?
   
Loading...