Gazeti la kuhamasisha maendeleo kwa mkoa wa Kagera na kanda ya ziwa kuzinduliwa mwezi wa nane

frajomedia

Member
May 1, 2016
35
7
Kampuni ya Frajo Media House Limited yenye makazi yake wilaya ya Bukoba mjini maeneo ya National Housing,mkoa wa Kagera inatarajia kuzindua gazeti la Hamasa mwezi wa 8,lengo la gazeti ni kuhamasisha maendeleo kwa mkoa wa Kagera na kanda ya ziwa kwa ujumla.

Kwenye Takwimu za umasikini Tanzania,mikoa ya Kanda ya ziwa tumeongoza kwa umasikini kagera ikishika nafasi ya 3 ikifuatiwa na mwanza,hivyo gazeti ili litakuwa mkombozi kwa kuelimisha na kutoa mbinu mbalimbali kwa wakulima,wajasiriamali n.k,namna bora ya kujikomboa kutoka kwenye umasikini,pia litaburudisha

Tunaomba mtuunge mkono kuelekea kwenye mapinduzi haya ya kuelimisha jamii katika kuondoa umasikini.

Kwa wataalamu wote wenye maoni tofauti tofauti namna ya kuondoa umasikini,mnaombwa mtume maoni yenu kwenye email ya frajomedia@gmail.com au namba 0755764273 na 0689401669 pia tuna page facebook ya Frajo media House limited

Tulianza na Hamasa Talkshow katika kuelimisha jamii kupitia mazungumzo,unaweza kuangalia kipindi youtube kwa jina la Frajo Media.Pia tunaonesha vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana Kagera,tuna page facebook ya Kagera Tourism na website www.kageratourism.com

Lengo la Gazeti la Hamasa ni kuhamasisha maendeleo ili kuongeza vipato kwa wananchi na mkoa katika kuisaidia serikali kuondoa umasikini.

Tunaomba pia wakazi wa kanda ya ziwa mlioko nje ya mkoa na nchi ambao mnashiriki au mna vikundi vyenye kusaidia mikoa yenu muweze kuwasiliana na sisi ili kutangaza shughuli zenu na hatimaye kushirikiana kuondoa umasikini.

Asanteni sana,pamoja tunaweza kuhamasisha maendeleo na kuondoa umasikini.

hamasa 2.jpg

Pia unaweza kuangalia kuhusu Hamasa Talkshow hapa

update:
img_20160902_110549-jpg.392587
img_20160902_110601-jpg.392589
img_20160902_105522-jpg.392590
img_20160902_105017-jpg.392597
img_20160902_105053-jpg.392598
img_20160902_105053-jpg.392598
img_20160902_105536-jpg.392599
img_20160902_105003-jpg.392600
img_20160902_104948-jpg.392601
img_20160902_105115-jpg.392602

Gazeti lako la HAMASA la mwezi wa 9 likiwa na habari kemkem kama utalii wa utamaduni unavyoweza kuondoa umasikini Kagera,Taarifa kuhusu mradi wa Tushirikishane ulioanza Bukoba,taarifa kuhusu ujenzi wa soko,stendi ya mabasi Bukoba,namna ya kuondoa tatizo la ajira Kagera,maazimio yaliyofikiwa kwenye ziara ya waziri William Lukuvi na waziri Angela kailuki,sehemu ya pili kuhusu ugonjwa wa UTI,
Faida na changamoto za bodaboda,jinsi ya kujikwamua kiuchumi kupitia Wadau wa elimu,wanawake wanavyolazimika kujifungua njiani Bukoba vijijini,ziara za Balozi Kamala kwa wananchi wake,habari za kanda ya ziwa,wafahamu wasanii wa Kagera kama Be Friends wazee wa Nabumbuiga na Tamimu Omurungi mfalme wa Zuku Kagera
Matukio ya Fiesta Muleba,Historia ya Kagera,Shindano la kisura wa HAMASA linaendelea,ukitaka kushiriki wasiliana na sisi zawadi nono kutolewa,
Na habari nyingine nyingi za ujasiriamali,burudani,ubunifu,elimu,afya,uwekezaji,mitindo,urembo,mahusiano,riwaya,vitimbi na vichekesho,uchambuzi,makala,wasanii,sayansi na teknolojia,michezo,utalii,utamaduni,kilimo, nakadhalika.
 
Kwa nini msitoe gazeti lenye sura ya kitaifa ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika

Asante,matatizo ya watanzania ni yaleyale hayatofautiani uwezo wetu kwa sasa unaruhusu kuwa na waandishi kutoka kanda ya ziwa,hapo baadaye tutasogea Tanzania nzima,tunaomba mtuunge mkono kufanikisha ilo
 
Wahaya bana... Idd Amin angewahamishia kwake ndo mngeisoma namba kisawasawa:D:D:D:D

..... Unajua wakati naendesha lile vogue langu leo nililonunua milion 200, ghafla nikapokea simu nahitajika nyumbani, nikaendesha speed kurudi home, nilipofika nikafungua geti kwa rimoti maana nilitoka nayo, nikapaki kati ya ile V8 na BENZ niliyonunua juz tu ulaya, nilipoingia sebuleni nikafungua friji na kuchukua wine, nikajipooza kumbe wameacha FLAT screen moja kati ya tatu pale sebuleni ikiwa ON, nikaizima na kupanda sebule yangu ya kupumzikia ghorofa ya tatu, ili nimsikilize mke wangu anasemaje, nikajirusha moja ya sofa nilizonunua uingereza juz, nikawasha flat screen zote tatu kwenye sebule yangu, nikavua saa yangu ile ghali sana nakuiweka mezani ili niwe kwenye utulivu:D:D:D:D

Mhaya huyoo_Oo_Oo_O
 
Ingawa mie siyo Mhaya nadhani this type stuff is not fair to them.
 
Mkuu heshima kwako,hapa tupo serious mkuu sio utani.Asante
 
Sitaki kucheka asubuhi yote hii;
kuna maendeleo gani yakuhamasisha kupitia magazeti?
Nyie wahaya acheni mbwembwe jengeni kwenu;
 
Wahaya wanakera sana...yani Nyerere alibugi sana ...angemuacha Idi Amini awachukue hao wahaya...sioni faida tuliyoipata aisee
 
Mikoa yote iige mkoa wa Kagera maana bila mawasiliano maendeleo ni ndoto. Liwe gazeti kweli isije ikawa ni hadithi za IKENGYA!!!
 
Waache tu mkuu make wasipokaa na kuanza kuwadis wahaya hujisikia kuna kitu fulani wanapungukiwa maishani mwao, ndivyo walivyo.
Wahaya poleni sana! Nadhani utani wa Mwalimu uliwafanya Watanzania waamini kuwa ni ukweli. Wasi wasi wangu ni kuwa suala hili linaendelea kukua vizazi na vizazi. Pamoja na watu kutusema sana sie Wachagga ila wahaya mnasimangwa zaidi. Poleni sana Mwenyezi Mungu atawasaidia tu
 
Tz yetu ina roho ya ? sana. Kuwa mchawi si lazima utumie dawa, watz wengi ni wachawi sana tena wa kupindukia na ndo maana kama nchi hatuendelei ila daily tunadai mabadiliko. Anayedai mabadiliko ukimwangalia alivyo unajiuliza ni kwanini Mungu anampa shetani nguvu kiasi hiki ...ndo hivyo ndugu yangu.
 
Acheni u kabila eti hamasa mkoa wa kagera na kanda ya ziwa .....utafikiri huo mkoa sio miongoni mwa mikoa ya kanda ya ziwa
 
Back
Top Bottom