Mwenezi Makalla: Awamu ya 6 Ndio Serikali Pekee Iliyoongoza Kutoa Pesa Nyingi za Maendeleo

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
8,776
10,163
Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM chama Dume amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mwanamama jasiri na profesa wa Siasa Samia S.Hassan ndio awamu pekee Iliyoongoza kumwaga na kumimina mabilioni ya miradi ya Maendeleo Vijijini na Mijini.

Bwana Makala alikuwa akizungumza mjini Manyoni kwenye Mkutano wa hadhara.
---
Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk. Samia ndiyo awamu pekee inayopeleka fedha nyingi za maendeleo kwa wananchi.

Makalla alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mji wa Manyoni mkoani Singida ikiwa ni siku ya kwanza kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Emmanuel Nchimbi katika mikoa mitano iliyoanzia mkoani hapa.

"Mkoa huu ulikithiri kwa umaskini, tulikuwa tunajulikana kwa nyumba za tembe lakini sasa hali ya umasikini imepungua kwa kiasi kikubwa. Huoni tembe tena kwani kilimo cha alizeti, vitunguuu na biashara vimechochea maendeleo makubwa.

Alibainisha: "Rais Dk. Samia ameingia kwenye rekodi ya kuboresha maisha ya wananchi wa Mkoa wa Singida kwani kila kijiji kuna jambo limefanywa na serikali."

Makalla alisema mkoa huo una vijiji 441 ambapo hadi sasa vijiji 420 vimepatiwa umeme na kubakisha vijiji 29 ambavyo vitapatiwa nishati hiyo hivi karibuni.

My Take
Kazi za Mama Samia zinaongea na kumnadi ,haihitaji propaganda.Pia soma RC Mongella: Sijawahi ona Rais anayetoa pesa nyingi kwa pamoja kama Samia. Kazi hii ina Thawabu kwa Mungu

Itoshe kusema Mama Anatosha na Chenji inabaki.👇👇

---
RC RUVUMA AKAGUA MIRADI UJENZI WA MAJENGO MAPYA YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amekagua miradi ya ujenzi wa majengo ya hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma katika Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea.

Akitoa taarifa ya mradi huo,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea Dr.Magafu Majura ameyataja majengo yanayotekelezwa kwenye mradi huo kuwa ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la huduma za mionzi na jengo la huduma za kuchuja damu(Dialysis unit).

Amesema kuwa serikali imetenga shilingi bilioni nne kujenga jengo la OPD lenye ghorofa moja ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 75 na kwamba mradi unatarajia kukamilika katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Akizungumzia mradi wa jengo la mionzi,Dr. Majura amelitaja jengo la kutolea huduma za kichunguzi ya mionzi ambalo ndani yake kuna mashine mbili za CT Scan na Digital X ray ambazo zinazofanya kazi,limekamilika kwa asilimia 100 na limeanza kutoa huduma za CT Scan.

Dr.Majura ameutaja mradi wa huduma za kiuchunguzi za Radiolojia kuwa una thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni mbili ambapo utekelezaji wa mradi huo ulianza Machi 2023 na huduma za CT Scan zilianza kutolewa Aprili 2023.

“Huduma ya CT Scan imepunguza adha kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao walikuwa wanapata huduma hii katika hospitali ya Kanda ya Mbeya na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili’’,alisema Dr.Majura.

Mradi mwingine ambao unatekelezwa ni ujenzi wa jengo la kisasa la kusafishia damu ambapo Dr.Majura amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Januari 2024 na unatarajia kukamilika Julai 2024 na kwamba jengo linagharimu shilingi milioni 600.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amepongeza serikali kutekeleza miradi hiyo inayokwenda sanjari na ununuzi vifaa vya kisasa katika hospitali hiyo ambapo ametoa rai kwa wananchi kutumia huduma za kisasa zinazotolewa katika hospitali hiyo.
 
Maendeleo sio vitu ni watu? Ndio mana pamoja na yote hayo bado kiwango cha umasikini kipo juu kuliko maelezo hii inamaanisha mnaangalia Macro economy ila kwenye Micro economy ambako ndio wananchi wengi wanaguswa hakuna lamaana sasa watu watakula mabarabara au madaraja? Wananchi wanataka kuona haya maendeleo mnayosema yanachochea vipi ustawi wa maisha yao?unajenga majengo ya hospital bila kuwa na wataalamu wa afya wakutosha au dawa zakutosha pia mwananchi kupata huduma kwa gharama ambazo ni affordable,ni heri kua na hospitality chache zenye madaktari wakutosha,vifaa tiba na dawa zakutosha na gharama nafuu kwa wananchi kupata huduma zauhakika kuliko kuwa na majengo lukuki yasiyokua na msaada
 
Kote huko Samia anawapa watu tabasamu.Kila mwaka Toka ameingia amekuwa akitoa Ajira zaidi ya 30,000 na Mwaka huu pekee Ajira 45,000 Zinaenda kutoleaa na sekta zinazonufaika zaidi ni
-Afya
-Elimu
-Usalama(Polisi,Uhamiaji,Jeshi)

View: https://twitter.com/ortamisemitz/status/1796570144535142574?t=r1qHQA5SDVTk06-l_VIuvQ&s=19
 
Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM chama Dume amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mwanamama jasiri na profesa wa Siasa Samia S.Hassan ndio awamu pekee Iliyoongoza kumwaga na kumimina mabilioni ya miradi ya Maendeleo Vijijini na Mijini.

Bwana Makala alikuwa akizungumza mjini Manyoni kwenye Mkutano wa hadhara.

View: https://www.instagram.com/p/C7jpM7sIrRE/?igsh=cWNnaHdsbWJyeTRi

My Take
Kazi za Mama Samia zinaongea na kumnadi ,haihitaji propaganda.Pia soma RC Mongella: Sijawahi ona Rais anayetoa pesa nyingi kwa pamoja kama Samia. Kazi hii ina Thawabu kwa Mungu

Itoshe kusema Mama Anatosha na Chenji inabaki.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C7kI34FMEb8/?igsh=MTI0ZGE2MTBocTQ2Mw==

Asubirie kwanza na yeye mwakani 2025 azunguke nchi nzima kutushawishi ili tumpigie kura. Endapo atapita, hapo mtakuwa na kila sababu ya kumsifia.

Lakini kwa sasa, anasafiria Nyota ya shujaa wa Taifa ili tangu Uhuru naye si mwingine bali Hayati JPM.

Hivyo, anayestahili sifa kwa yote yanayoendelea hadi mwakani ni JPM na siyo mama yenu.
 
Back
Top Bottom