Gazeti Habari leo lina mpya kuhusu kifo cha Mwandishi

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
================================================================================================================
BOFYA HAPA: Mwandishi afa katika mkutano wa Chadema
===================================================================================================================

Gazeti Habari Leo linalomilikiwa na Serikali ya CCM limekuja na mpya kuhusu chanzo cha kifo cha Mwandishi wa Habari.

Bofya hapo juu uone kilichosemwa na Gazeti hili kwa kunukuu Jeshi la Polisi Makao Makuu.

Je, kama majibu ndio haya kuna umuhimu wa kuunda tume tena???

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Duh ungeileta habari hapa ungekuwa umetusaidia sana, lakini anyway ngoja tuifuate huko tutarudi later
 
Huyo mwandishi sijui anajisikiaje kuandika alicho andika. Kuna vya kutetea lakini sio hili
 
BOFYA HAPA: Mwandishi afa katika mkutano wa Chadema

Gazeti Habari Leo linalomilikiwa na Serikali ya CCM limekuja na mpya kuhusu chanzo cha kifo cha Mwandishi wa Habari.

Bofya hapo juu uone kilichosemwa na Gazeti hili kwa kunukuu Jeshi la Polisi Makao Makuu.

Je, kama majibu ndio haya kuna umuhimu wa kuunda tume tena???

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mkuu link haifunguki kabisa. Da tungeipata ingetusaidia kujua uozo wa hii kitu maana Habari Leo ni sister gazeti na Daily News ambalo ni la serikali!!! sorry SSM lakini kuna lile SSM proper ambalo ni UHURU na Mzalendo!!!!
 
Alichoandika ni sawa sijaona kosa ambalo marehemu alitakiwa apewe adhabu ya Kifo!! Ila yule askari muaji (Picha mwananchi) Nadhan polisi watajitahidi sana kumlinda!! Sijui kama wataweza kuchomoa kwenye Hili!!
 
Duh ungeileta habari hapa ungekuwa umetusaidia sana, lakini anyway ngoja tuifuate huko tutarudi later

Mwana Mpotevu

Kuna Link nimeiweka hapo juu, BOFYA uone jinsi wanavyoitetea hii habari kwa maslahi ya kisiasa. Mwandishi aliyeandika habari hii ametetea pasipo kuangalia uhalisia.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Last edited by a moderator:
MWANDISHI AFA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA

MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi, amekufa katika vurugu za kuwatawanya wafuasi wa Chadema katika Kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.
Mwangosi ambaye ni mwakilishi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten mkoani Iringa, alifariki akiwa mikononi mwa Polisi ambapo inadaiwa kabla ya kifo hicho, mwandishi huyo na mmoja wa maofisa wa Polisi aliyekuwa amemshikilia, walilipukiwa na kitu kilichowajeruhi vibaya.
Akisimulia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda aliyekuwepo katika mkutano huo wa Chadema, alidai kuwa kabla ya kufikwa na mauti, Mwangosi alikuwa katika majibizano na askari Polisi.
Kwa mujibu wa madai ya shuhuda huyo, kabla ya kuanza kwa vurugu hizo, viongozi wa Chadema na wafuasi wake walikuwa katika mkutano wa kufungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.
Alidai kuwa wakiwa eneo la tukio, polisi walifika katika tawi hilo na kuwataka wafuasi wa chama hicho kutawanyika kwa kuwa mikutano ya vyama vya siasa imepigwa marufuku kupisha kazi ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo imeongezewa siku saba baada ya muda wake wa awali kukamilika.
Kutokana na amri hiyo, mtoa habari alidai kuwa wafuasi hao walikataa kutawanyika na kuwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi kwa ni ya kuwatawanya.
Wakati wakipiga mabomu hayo, inadaiwa mwandishi mmoja wa habari (jina limehifadhiwa), aliwafuata polisi na kuhoji sababu za kutumia nguvu hiyo kutawanya wananchi.
Mtoa habari huyo alieleza mwandishi huyo alikamatwa na kusababisha Mwangosi kwenda kujaribu kumnasua mwandishi mwenzake kutoka mikononi mwa polisi.
Shuhuda huyo alidai kuwa polisi walimsihi Mwangosi aondoke katika eneo hilo ili waendelee na kazi yao na alipokaidi, walimkamata na yeye.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, wakati Mwangosi akiwa amezungukwa na askari Polisi wanaokaribia watano, kulisikika mlio wa mlipuko na baadaye Mwangosi na mmoja wa askari aliyekuwa amemshika walianguka chini.
Inadaiwa Mwangosi alifariki papo hapo baada ya kujeruhiwa vibaya katika mlipuko huo huku askari Polisi huyo anayedaiwa kuwa wa cheo cha juu, akikimbizwa hospitalini baada ya kujeruhiwa vibaya pia.
Gazeti hili liliwasiliana na Mhariri Mkuu wa Chanel Ten, Dina Chaali ambaye alikiri kupokea taarifa za kifo cha Mwangosi lakini hakuwa tayari kuzungumza chochote kuhusu kifo hicho.
Dina alisema baada ya kupata taarifa hiyo, wamelazimika kuwa na mkutano wa dharura na uongozi wa juu wa kituo hicho na baada ya hapo ndipo watatoa tamko.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael Kamuhanda alipopigiwa alisema yuko katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Iringa asingeweza kuzungumza wakati huo.
Hii ni mara ya tatu kutokea vifo katika vurugu zilizotokana na Chadema kukaidi amri halali za Polisi. Mara ya kwanza mkoani Arusha, watu wawili walikufa wakati wa vurugu za kutawanywa kwa wafuasi wa Chadema waliokuwa wamezuiwa kuandamana.
Hivi karibuni, mwishoni mwa mwezi uliopita, Chadema katika mikutano hiyo ya vuguvugu la mabadiliko katika Mkoa wa Morogoro, walikaidi amri ya kusitisha mikutano hiyo na kusababisha vurugu zilizozua kifo cha mwananchi mmoja aliyekuwa akijishughulisha na uuzaji wa magazeti.
Hata hivyo baada wa kifo hicho, Chadema walisitisha mikutano hiyo ili kuruhusu kumalizika kwa shughuli za Sensa ya Watu na Makazi ingawa mwanzoni walikaidi.
Mbali na kusitisha mikutano hiyo, Chadema walisisitiza kuwa muuza magazeti huyo aliuawa kwa risasi na Polisi jambo ambalo lilipingwa na taarifa ya daktari aliyemfanyia uchunguzi, ambayo iliweka wazi kuwa kifo hicho kilisababishwa na kupigwa na kitu kigumu kichwani.
Taarifa za awali kutoka Polisi Makao Makuu, zilieleza kuwa wakati wa vurugu hizo, Mwangosi aliamua kukimbia kutoka upande ambao kulikuwa na kikundi cha watu waliokuwa wakitawanywa huku wakikaidi amri ya Polisi, kwenda upande ambao walikuwepo askari Polisi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakati Mwangosi alipokaribia walipokuwepo polisi hao, kitu kama bomu kilirushwa kutoka upande kilipokuwepo kikundi hicho cha watu ambacho kililipuka na kumuua Mwangosi na kujeruhi askari kadhaa.
Taarifa hiyo ilitaja kuwa polisi aliyejeruhiwa vibaya katika tukio hilo ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCS), ambaye hata hivyo hakutajwa jina lake wala wilaya anayofanya kazi.
 
Ni ya kawaida sana tu sema mwandishi anajaribu kutaka tuamini kuwa pilisi hawakuua kwa makusudi....kwamba hata askari kajeruhiwa, kwa hiyo ni bahati mbaya 'bomu' lililipuka. Na kwamba marehemu alikuwa mkaidi kuondoka hivo 'wakamlipua!'
 
Mkuu link haifunguki kabisa. Da tungeipata ingetusaidia kujua uozo wa hii kitu maana Habari Leo ni sister gazeti na Daily News ambalo ni la serikali!!! sorry SSM lakini kuna lile SSM proper ambalo ni UHURU na Mzalendo!!!!

rudi kwenye post nimepaste habari nzima
 
Mkuu link haifunguki kabisa. Da tungeipata ingetusaidia kujua uozo wa hii kitu maana Habari Leo ni sister gazeti na Daily News ambalo ni la serikali!!! sorry SSM lakini kuna lile SSM proper ambalo ni UHURU na Mzalendo!!!!

Mkuu link imefunguka ila nimeshangaa ni jinsi gani uongo utatumaliza. Tunakubali kutumika kufunika maovu!!! Hata kama unaandikiwa gazeti la chama au nini huna sababu ya kutetea mauaji ya kinyama kiasia kile. Angali mwandishi usije ukavuna damu na wewe. Halafu habari ikishakuwa na jina na Mwandishi wetu jua ni fitina tu!!! Eti alikuwa anakimbia upande huu kwenda mwingine na kitu kikaruka kama bomu upande wa CDM!!! What a fake brain here full of water, gadem. Yaani polisi wamemshikilia Mwangosi marehemu, na silaha zinamlenga kabisa halafu unasema eti alikuwa anakimbia? Wanaharamu nyie Habari leo na serikali yenu!! Sasa picha zitatutua international media and human rights organisations lalafu ndipo mseme. Watanzania danganya toto wa leo asubuhi si wa sasa saa tisa na nusu alasiri.
 
MWANDISHI AFA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA

Mtoa habari huyo alieleza mwandishi huyo alikamatwa na kusababisha Mwangosi kwenda kujaribu kumnasua mwandishi mwenzake kutoka mikononi mwa polisi.
Shuhuda huyo alidai kuwa polisi walimsihi Mwangosi aondoke katika eneo hilo ili waendelee na kazi yao na alipokaidi, walimkamata na yeye.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, wakati Mwangosi akiwa amezungukwa na askari Polisi wanaokaribia watano, kulisikika mlio wa mlipuko na baadaye Mwangosi na mmoja wa askari aliyekuwa amemshika walianguka chini.

Taarifa za awali kutoka Polisi Makao Makuu, zilieleza kuwa wakati wa vurugu hizo, Mwangosi aliamua kukimbia kutoka upande ambao kulikuwa na kikundi cha watu waliokuwa wakitawanywa huku wakikaidi amri ya Polisi, kwenda upande ambao walikuwepo askari Polisi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakati Mwangosi alipokaribia walipokuwepo polisi hao, kitu kama bomu kilirushwa kutoka upande kilipokuwepo kikundi hicho cha watu ambacho kililipuka na kumuua Mwangosi na kujeruhi askari kadhaa.
Taarifa hiyo ilitaja kuwa polisi aliyejeruhiwa vibaya katika tukio hilo ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCS), ambaye hata hivyo hakutajwa jina lake wala wilaya anayofanya kazi.

Nilkuwa napataka hapo kwenye NYEKUNDU na BLUU ili muone contadictions zilizopo. Ukweli uko wapi?.
 
Nilkuwa napataka hapo kwenye NYEKUNDU na BLUU ili muone contadictions zilizopo. Ukweli uko wapi?.

ukweli upo kwenye mfululizo wa zile picha mkuu, na kama utakuwa ulisikiliza Radio One asubuhi kuna shuhuda amabye ni mwandishi wa habari ameeleza kuwa Polisi waliktumia nguvu na ndio chanzo cha kifo
 
Kama huyo Mwandishi alisikiliza kipindi cha Baragumu asubuhi ya leo Kilichoendeshwa na Kibwana Dachi mpaka sasa atakuwa ameinamisha kichwa chini anaona aibu kwa kufurahua kifo cha mwandishi mwenzake kwa sababu tuu yeye yuko magazeti ya serikali ,wananchi wamesema ukweli wote wametoa ushuhuda waliokuwepo ambao watazamaji umetuhakikishia kwamba jeshi la polisi linamkakati wa kuua wananchi wafuasi na viongozi wa chadema kwa manufaa ya seRikali na CCM peRiod
 
Mkuu link haifunguki kabisa. Da tungeipata ingetusaidia kujua uozo wa hii kitu maana Habari Leo ni sister gazeti na Daily News ambalo ni la serikali!!! sorry SSM lakini kuna lile SSM proper ambalo ni UHURU na Mzalendo!!!!

Nimejitahidi kui-copy lakini inanikatalia. Hivyo jaribu kuingia katika Website ya Gazeti habari leo utaikuta pale.

HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
A very stupid story,

Imekaa kama hadithi za once upon a time,

Marehemu Mwangosi, ametajwa kila mahali, source haijatajwa hata paragraph moja.

Ni story ya kutunga kabisa
 
Back
Top Bottom