Gazeti Botswana lalia na Mbeki kuhusu Kikwete

darcity

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2009
Posts
9,283
Reaction score
18,349
Gazeti la Sundaystandard la Botswana limemlaumu Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki kuwa nyuma ya kushindwa kwa Mgombea wake Pelonomi Venson-Moitoi katika uenyekiti wa AU.

Gazeti linaamini kwamba Mbeki ambaye alitumia jitihada kubwa wakati wa utawala wake kuijenga AU ndio 'masterminder' wa kumuingiza JK kama mwenyekiti wa AU kwa kigezo cha kuwa ndiye mgombea mwenye hadhi na linashuku kuwa Mbeki ndiye mzizi wa fitina wa Matatifa ya Afrika Magharibi kukacha kupiga kura ili kuruhusu JK aingie na tayari ameshamkabili JK kumshawishi kugombea.

Gazeti hilo pia limelaumu maamuzi ya Rais wa Botswana kutohudhuria vikao vya AU na na vikao vyengine kama kile alichoitisha Obama kwa viongozi wa Afrika.Gazeti limemshauri Pelonomi Venson-Moitoi kujitoa kwani tayari kwani Rais mstaafu JK anatoka toka taifa lenye ushawishi mkubwa Afrika ( African powerhouse)

Pitia hapa kwa habari kamili
:http://www.sundaystandard.info/venson-moitoi-should-withdraw-contest-lead-african-union-commission

epa00811787-south-african-president-thabo-mbeki-r-tanzanian-president-fj3dyt.jpg
image-14-300x229.jpeg
 
Sasa umekuja kumshtaki kikwete hapa JF au umekuja kuomba ushauri.
Haujuia kwamba Tanzania na South Africa tuna undugu wa mda mrefu tangu kipindi cha Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela hivyo Mbeki anaona akipata Kikwete ni kama imepata South Africa kutokana na historia za Tanzania na South Africa pia Mbeki ameona Kikwete anastahili hiyo nafasi kwa kuwa ana sifa zote za kimataifa na kidiplomasia.
 
Hapana ni taarifa tu mkuu sio ushauri au kumshtaki JK
 
Jakaya Kikwete kishasema hataki kuandika barua kuomba kazi yoyote kwa kuwa kishafanya kazi kubwa zaidi Duniani ya Urais. Sasa ni jukumu la Africa wakimtaka Jk basi wawapige chini wagombea wote
 
Ma sha Allah.

Wanamgombania kimataifa.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.
Duh...this is too low for you my dear, mwenyekiti wa AU si anakuwa Rais wa nchi mwanachama inayokuwa na zamu ya kuwa mwenyekiti, na kama ni ukatibu si ni lazima uombe na JK aliapa katu hawezi thubutu sasa wewe unataka kutueleza upumba.vu gani huu?
 
JK nae apumzike, sasa kutoka urais wa nchi hadi AU kufanya nini? Ndo maana nchi nyingi zimesusia uchaguzi sababu ya ubabaishaji uliokuwepo. Amewafanyia nini watanzania hadi sasa atamani kuwatumikia waafrika ambao ni wengi zaidi? Hata kama ni uzalendo, nafuu aende mtu mwingine lakin sio Kikwete, inamshushia hadhi maana hata wagombea wenzake hawana hadhi yake. Kama wewe ni kidato cha nne, unashindana na darasa la saba; ikitokea bahati mbaya ukashindwa-aibu huwa mara mbili.
 
Ma sha Allah.

Wanamgombania kimataifa.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.
Bibi unanifurahisha. Mwaka jana 2015 kuna mtu nilimwambia kwamba Kikwete na Zitto ni wanasiasa makini alibisha ila sasa hivi ukweli unaanza kuonekana.
 
Nabii hakubaliki kwao tu,watz tulipata rais aliyekuwa akiongoza kwa kutomshurutisha wala kumuamrisha mtu tukamuona hafai tukawa tunamzunguka nakufanya mambo ndivyo sivyo...........
 
JK nae apumzike, sasa kutoka urais wa nchi hadi AU kufanya nini? Ndo maana nchi nyingi zimesusia uchaguzi sababu ya ubabaishaji uliokuwepo. Amewafanyia nini watanzania hadi sasa atamani kuwatumikia waafrika ambao ni wengi zaidi? Hata kama ni uzalendo, nafuu aende mtu mwingine lakin sio Kikwete, inamshushia hadhi maana hata wagombea wenzake hawana hadhi yake. Kama wewe ni kidato cha nne, unashindana na darasa la saba; ikitokea bahati mbaya ukashindwa-aibu huwa mara mbili.
Unashauri Jk apumzike japo kishasema hatagombea wala kuandika barua ya kugombea cheo chochote.
Ila utakuta unaunga Mkono Waziri Mkuu mstaafu kugombea uenyekiti wa kitongoji wa upinzani
 
Hatukomoani ndugu, sio kila wakati ni wakati wa CCM na UKAWA. Kuna nyakati ni zetu sisi na akili zetu, wakati huo usiweke akili pembeni. JK ana heshima an anafahamika kimataifa, hahitaji kuiongoza AU ili apate jina. Hii AU ya sasa imejaa upepo ndo maana watu makini kama Magufuli hawajaipa kipaumbele. Rais wa Botswana nae harembi, ndo maana anaipotezea AU.

Kusema na kutenda ni tofauti-vijikazi vya kimataifa alivyopewa miezi kadhaa iliyopita vinaonyesha hatasita kuchukua nafasi ya AU. Nimejifunza kutosikiliza analosema bali analotenda.
 
Inakuaje Umshauri Jk apumzike wakati hajasema kama atakubali au atakataa?
Jk anafanikiwa kwa kuwa anachukiwa na Watu waliolaaniwa akiwemo Tapeli mmoja anaejifanya kufufua Misukule
 
Haya mkuu, sio kila anayekosoa ana chuki. Wengine tunatambua kuwa akiadhirika mtanzania mmoja tumeadhirika wote. Ushauri wangu una mantiki maana pamoja na kwamba kakataa, hachelewi kusema wazee wameniomba kama kawaida ya wanasiasa wetu.
 
41 Years kwny Ulingo wa siasa mpaka kufikia level ya Urais aje achukue ushauri wa kisiasa Mtandaoni?
 
Kwani kwenye hiyo miaka 41 amefanya nn ambacho wewe na yule mtashindwa kukifanya? Sijaona muujiza wowote ktk uongozi wake.
 
Back
Top Bottom