Gawio na michango ya Mashirika: Tuwe makini tusishushe ufanisi

Gawio na michango ya Mashirika: Tuwe makini tusishushe ufanisi

Vanilla2025

Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
5
Reaction score
2
Nyakati ambazo misaada kutoka nje inasua-sua na huenda ikazimika kabisa huko tuendako, kilichofanyika leo kinapaswa kupewa uzito zaidi na kutumika vizuri zaidi ili hatimaye kisaidie kama moja kati ya mbinu zitakazo tuwezesha kuondoa kabisa utegemezi wa kibajeti kwenye uchumi wa Taifa letu.

Ni kweli kwamba kuna dalili za wazi zinazoashiria kuwa faida imeanza kupatikana kwenye mashirika na makampuni ambamo Serikali ina hisa. Lakini ni kweli pia kwamba kuna maswali hojaji yanayostahili kujibiwa kwani tunafahamu Serikali imewekeza zaidi ya Sh.T. 96 kwenye taasisi hizi.

Bila shaka, kwa vigezo vyovyote, hii ni pesa nyingi sana; ni jasho la kutosha sana la nguvu kazi yetu wa-Tanzania. Hata hivyo, naomba nijielekeze katika kutathimini mfumo tunaoutumia kubaini taasisi zilizofanya vizuri na zile ambazo hazikufanya vizuri kwani tusipokuwa makini, mfumo utumikao unaweza kushusha kabisa ufanisi.

Mosi lakini, tunashawishika kuamini kwamba takwimu zinazotumika kukotoa faida na hivyo gawio, lazima zithibitike kuwa ni za kweli pasi na shaka yoyote kwa muda wowote. Hili likipuuzwa, zikaanza kuletwa takwimu zinazobeba gawio lililo mkopo wa moja kwa moja wa Banki, muda si mrefu upokeaji wa gawio na Michango hii, itakuwa ni mshumaa uliozimika, hauwezi kuwa na mwanga tena.

Pili, mfumo tunaoutumia ni kama vile unalinganisha Mlima Kilimanjaro na kichuguu au kichuguu wakati tunafahamu fika kuwa bidhaa au huduma zinazozalishwa na taasisi zilizotajwa idadi yake kuwa ni 308, zina utofauti sana wa thamani.

Hivi kwa mfano unalinganishaje taasisi inayofanya biashara ya au katika mnyororo wa biashara ya dhahabu na wale wanaozalisha bidhaa au huduma kama za Utumishi wa simu au huduma za ki-Benki?

Tatu, mfumo tunaoutumia ni ule unaoitwa top-bottom badala ya ule Bottom-up, wenye mawanda mapana zaidi na ambao unaweza kusajihisha maendeleo ya jamii kwa haraka zaidi.

Je, ni kweli kwamba Serikali haikuwekeza kwenye sekta au tasnia mbalimbali za kilimo? Kama jibu ni hapana, kwa nini hatukuona wawakilishi wa sekta ya kilimo, sekta ambayo inabeba idadi kubwa ya Wa-Tanzania? Je hii si kuthibitisha kwamba mfumo huu ni wa Top-bottom?

Nne, tuzo zinazotolewa na kuwekwa tu kwenye masjala au kumbukumbu bila ya kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa maisha ya kila siku ya wafanyakazi wa ngazi za chini wa taasisi husika, haziwezi kuhakikisha ufanisi mahala pa kazi unakuwa, endelevu.
 
Wafanyakazi wanaminywa kuliko maelezo, hiyo ndio habari ya mjini
 
Back
Top Bottom