Gavana wa Benki kuu Afghanistan ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gavana wa Benki kuu Afghanistan ajiuzulu

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Jun 28, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Gavana wa benki kuu nchini Afghanistan Abdul Qadeer Fitrat amejiuzulu kutoka wadhifa huo akihofia maisha yake.
  Rais Karzai analaumu washauri wa kigeni kwa hasara iliotokea kwenye benki ya Kabul


  Bw Fitrat amsema vigogo serikalini wanamzuia kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu wa dola nusu bilioni kutoka benki ya Kabul.
  Lakini msemaji wa Rais Hamid Karzai, ametaja hatua ya gavana huyo kuwa uhaini mkubwa.
  Waheed Omar amesema kuwa uchunguzi ulikuwa umeanzishwa kuhusu utenda kazi wa gavana huyo wa benki kuu.
  Uchunguzi umeonyesha kuwa benki hiyo ilitoa mikopo ya mamilioni ya dola bila kufuata maadili, hali iliotishia kuifilisi benki hiyo.
  Serikali ya Afghanistan mwaka jana ililazimika kutumia pesa zake kuinusuru benki hiyo.
  Rais Karzai aliahidi kuwa uchunguzi utafanyika kuhusu sakata hiyo ya ufujaji wa pesa katika benki hiyo na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote.
  Bw Fitrat ambaye sasa yuko uhamishoni, anasema alikuwa na matumaini kuwa uchunguzi huo ungefichua wahusika kwenye sakata hiyo lakini badala yake umechochea matatiza maishani mwake.
  "Maisha yangu sasa yamo hatarini. Hii ni baada nilipozungumza bungeni na kufichua watu ambao walihusika na sakata hiyo katika benki ya Kabul" ameelezea Bw Fitrat.
  Baadhi ya watu waliotajwa na gavana huyo kuhusika na kashfa hiyo ni ndugu yake Rais Karzai, Mahmoud Karzai.
  Idara ya kuchunguza ufisadi nchini Afghanistan ilifichua kuwa zaidi ya dola milioni 467 zilitolewa na benki hiyo kama mikopo kwa vigogo nchini humo bila kufuata utaratibu.
  Lakini Rais Karzai alisema nchi yake haina uzoefu wa kutosha kusimamia benki hiyo na amelaumu washauri wa kigeni kwa hasara hiyo iliotokea.

   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huu wizi kasababisha Marekani na washirika wake!
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Huyu mjanja amegeuziwa kibao.

  Arrest warrant for ex-Afghan bank chief over 'fraud'
  Afghan officials have issued an arrest warrant for the former governor of the central bank, Abdul Qadeer Fitrat.

  He is being investigated in connection with massive fraud at the privately owned Kabul Bank and the printing of unauthorised amounts of currency.

  Earlier, it emerged Mr Fitrat had fled Afghanistan for the US - he said his life was in danger for exposing fraud.

  He said the Afghan government had hindered his attempts to investigate corruption.
  BBC News - Arrest warrant for ex-Afghan bank chief over 'fraud'
   
Loading...