Gavana Shilatu atembelea Maghala ya Ufuta

Gavana Shilatu atembelea Maghala ya Ufuta

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
*GAVANA SHILATU ATEMBELEA MAGHALA YA UFUTA*

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe *Ndugu Emmanuel Shilatu* ametembelea Maghala ya vyama vya msingi yanayopokea ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ya Mihambwe na Michenjele yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ili kujionea utaratibu unaotumika.

*"Kazi ya Serikali ni kuwasimamia, kuona mambo yanaenda vyema. Nimekuja kuwatembelea ili kuona changamoto zilizopo ili kuzitatua na pia kujiridhisha na utaratibu unaotumika. Kwa taarifa mlizonipatia mnakiri malipo yanaenda vyema kwa ufuta uliouzwa tayari. Kwa upande wa Mnunuzi ajitahidi sana kuja kuuchukua mzigo wake kwa wakati mara tu afanyapo malipo."* alisisitiza Gavana Shilatu.

Wakulima wanaendelea kujitokeza kwa wingi kuleta ufuta ghalani na hadi sasa minada minne mikubwa imefanyika ya kuuza ufuta ambapo 60% ya makusanyo yote mpaka sasa yameshauzwa na Wakulima wameshalipwa fedha zao.
FB_IMG_1563894051320.jpeg
 
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe *Ndugu Emmanuel Shilatu* hajaridhishwa na ujenzi mradi wa ghala uliotumia Tsh. Milioni 40 lakini umeshindwa kukamilika na kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi mara moja juu ya ujenzi huo na namna fedha hizo zilivyotumika.

Gavana Shilatu aliyasema hayo alipotembelea ghala hilo lililopo Kijiji cha Kitama Shuleni kata ya Kitama na kusikitishwa namna ambavyo fedha nyingi zikitajwa kutumika huku mradi ukiwa haujafika ukamilifu tarajiwa kiasi kinachopelekea kijiji kukosa mapato jambo ambalo ni kero kwa Wanakijiji waliokuja kulalamika kwa Afisa Tarafa huyo.

*"Serikali imetoa fedha tangu 2012 lakini mpaka sasa mradi haujakamilika na hivyo kunapelekea mapato yanakosekana ambayo yangesaidia kuleta maendeleo kijijini na maeneo mengineyo pia. Hili halikubaliki hata kidogo, naiagiza TAKUKURU kuanza uchunguzi mara moja juu ya ujenzi huu wa ghala."* Alisisitiza Gavana Shilatu.

Mradi huo wa ujenzi wa ghala lililopo eneo la Kitama Farmers Group kwenye kijiji cha Kitama Shuleni ulianza tangu mwaka 2012 lakini hadi Leo hii haujakamilika na hivyo kukosesha Serikali mapato.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kijiji Kitama Shuleni, Halmashauri ya Serikali iliyokuwepo Madarakani na ya sasa pamoja na Wazee maarufu Kijijini hapo ambao wote hawakuridhishwa na matumizi ya fedha ya ujenzi wa mradi huo.
FB_IMG_1564070696933.jpeg
FB_IMG_1564070701034.jpeg
FB_IMG_1564070705189.jpeg
 
Mkuu naona unajitahidi sana kujipigia debe ili mkulu akuone, Ila ndo hivyo tena mkulu kashaharibu huko na hana habari kabisa kufuatilia masuala ya huko.
 
Bei elekezi shilingi ngapi?
*GAVANA SHILATU ATEMBELEA MAGHALA YA UFUTA*

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe *Ndugu Emmanuel Shilatu* ametembelea Maghala ya vyama vya msingi yanayopokea ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ya Mihambwe na Michenjele yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ili kujionea utaratibu unaotumika.

*"Kazi ya Serikali ni kuwasimamia, kuona mambo yanaenda vyema. Nimekuja kuwatembelea ili kuona changamoto zilizopo ili kuzitatua na pia kujiridhisha na utaratibu unaotumika. Kwa taarifa mlizonipatia mnakiri malipo yanaenda vyema kwa ufuta uliouzwa tayari. Kwa upande wa Mnunuzi ajitahidi sana kuja kuuchukua mzigo wake kwa wakati mara tu afanyapo malipo."* alisisitiza Gavana Shilatu.

Wakulima wanaendelea kujitokeza kwa wingi kuleta ufuta ghalani na hadi sasa minada minne mikubwa imefanyika ya kuuza ufuta ambapo 60% ya makusanyo yote mpaka sasa yameshauzwa na Wakulima wameshalipwa fedha zao.View attachment 1160575
 
Back
Top Bottom