Gas ya Songo Songo haijatusaidia Zanzibar: Mbunge wa CCM Zanzibar

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Unajua kuna wakati mtu unajiuliza juu ya uwezo wa kufikiri wa baadhi ya hawa waheshiwa wetu Wabunge. Mfano ni huyu Mbunge wa Kitope upande wa Visiwani, Makame Mshimba Mbarouk (CCM), ambaye amedai sababu mojawapo ya kutoutaka muungano ni kwamba Zanzibar haijafaidikia na kuwapo kwa gas upande wa bara.

Suala la kujiuliza ni kwamba, ikiwa sehemu kubwa ya hii gas inazalisha umeme ambao unapelekwa Zanzibar, ambako kwa muda mrefu wamekuwa hata hawaulipii huo umeme, ni nani anayefaidika zaidi na hiyo gas kati ya bara na Zanzibar?

Pia ni katika njia zipi zaidi ya umeme ambazo bara wanafaidika zaidi na gas ya Songo Songo kuliko Zanzibar?

Najiuliza kama tatizo letu kubwa la muunguno wa Tanzania ni kuwa na wanasiasa wa aina ya kina Makame Mshimba Mbarouk.

Source: IPP Media
 
hizo facts umezitoa wapi? je umesahau kulikua na kipindi ambacho kulikua hampa umeme Zanzibar kwa siku tatu?
 
Kwani umeme unaokwenda zanzibar ni wa gesi ya songosongo au ni HYDRO ELECTRIC POWER? Anyway hivyo sivyo alivokusudia, kwani umeme huo zanzibar wananunua kama zilivyo nchi nyengine zinavyonunua umeme kutoka kwa nchi jirani, cha msingi hapo ni mapato yake yakoje? Kwani si gesi na mafuta si mambo ya muungano? Basi mapato yake yawe kimuungano na sio upande mmoja tu!! Au mwaonaje?
 
hizo facts umezitoa wapi? je umesahau kulikua na kipindi ambacho kulikua hampa umeme Zanzibar kwa siku tatu?

Kwa hiyo Zanzibar kukosa umeme siku tatu maana yake hawafaidiki na gas ya songo Songo na muungano uvunjwe? Kama kufikiri kwa Wazanzibar ndio huku basi bora muungano uvunjwe.
 
Kwani umeme unaokwenda zanzibar ni wa gesi ya songosongo au ni HYDRO ELECTRIC POWER?

Ukiweza kusema kitu kama hiki hupaswi hata kutamka neno juu ya mambo makubwa kama ya muungano. Tulia nyumbani watu wenye busara wafanye maamuzi.
 
Hawa walizungumza kuwa maswala ya gas na mafuta si maswala ya muungano. Iweje leo waanze kuulizia kuwa hawajafaidika na gasi ya Sogosongo? Ni baada ya ksikia kuwa gas na mafuta kule Mtwara na Lindi ni nyingi? Mawazo na akili zao kuwa waarabu watawasaidia lakini ikumbukwe kuwa hakuna mtu bahiri kama mwarabu. Wale watu ni matajiri kweli lakini ni mabahiri ile mbaya hata pale maafa yanapotokea husikii nchi za kiarabu kutoa msaada wowote. Hawa ni kuwaachia kisiwa chao kama hao jamaa watawapa msaada labda kuwaletea tende na nyama wanazogawa wakati wa majira fulani ya mwaka.
 
TANESCO imeisaidia Zanzibar kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Sehemu mojawapo TANESCO wanakotoa umeme huo wote ambao Visiwani wakua wakitumia kwa mkopo usiolipika ni pamoja na Songo Songo. Mheshimiwa Mbunge, ni kweli umelisahau hta hili????
 
Uwezo Tunao, mheshimiwa hana uwezo wa kuyajua hayo!
Angeulizwa sisi tunafaidka vipi na karafuu miaka yote hii?
 
Amegundua kuwa gas haisaidii zanzibar ila inasaidia wapi? Kiufupi hamna sehemu gas inasaidia zaidi ya umeme ulio kote
 
Unajua kuna wakati mtu unajiuliza juu ya uwezo wa kufikiri wa baadhi ya hawa waheshiwa wetu Wabunge. Mfano ni huyu Mbunge wa Kitope upande wa Visiwani, Makame Mshimba Mbarouk (CCM), ambaye amedai sababu mojawapo ya kutoutaka muungano ni kwamba Zanzibar haijafaidikia na kuwapo kwa gas upande wa bara.

Suala la kujiuliza ni kwamba, ikiwa sehemu kubwa ya hii gas inazalisha umeme ambao unapelekwa Zanzibar, ambako kwa muda mrefu wamekuwa hata hawaulipii huo umeme, ni nani anayefaidika zaidi na hiyo gas kati ya bara na Zanzibar?

Pia ni katika njia zipi zaidi ya umeme ambazo bara wanafaidika zaidi na gas ya Songo Songo kuliko Zanzibar?

Najiuliza kama tatizo letu kubwa la muunguno wa Tanzania ni kuwa na wanasiasa wa aina ya kina Makame Mshimba Mbarouk.

Source: IPP Media

Mbona Hiyo Gas haijaisaidia Tanganyika pia... Imewasaidia Viongozi wa CCM... Makame inabidi aitishe Mkutano wa

Halmashauri kuu ya CCM kuulizia 10% yake iko wapi kwanza, halafu awajali hao wananchi GAS itawasaidiaje

Umeme unaozalishwa ha Hiyo GAS ni mdogo sana... Mikataba ni Mibovu
 
Deni la 50 billion ambazo TANESCO imeisamehe Zanzibar juzi!
Ilikuwa TANESCO inadai mahari SMZ?
 
Back
Top Bottom