Gari ya push to start kugoma kuwaka

sisi ni ndugu

Senior Member
Sep 4, 2018
121
135
habari za jioni wakuu, niliazima gari ya rafiki yangu kwenda nayo sehemu flani, wakati wa kuondoka sehemu hiyo nilijaribu sana kukanyaga brake ili ni push the button kuwasha gari ila ikagoma kabisa,

Pembeni kulikua na bodaboda wengi nkajaribu kuomba msaada wakaniambia eneo hilo kuna minara mingi sana ya ofisi mbalimbali na mitandao ya simu, hvyo gari ukizima hadi lisukumwe hadi sehemu flani ndio liwake sababu hua sensor inakata. Mwingine akasema hua eneo hilo tatizo hilo lipo, akampigia simu mtu fulani akaja ndani ya dakika 2 hv, akaingia ila cha ajabu yeye alivyokanyaga brake naku push tu the button gari ikawaka, na ikabidi nimpe buku 5.

Si kwamba funguo niliiweka mbali wala ilikua mkononi mwangu hapo hapo na gari haikuwaka. Je nawe ushakutana na changamoto hiii? hakuna uhuni unaofanyika katika sensor hizi? a Au ndio ushamba ?
 
Chukua ufunguo bonyeza nao hicho kifufe Cha start, betri ya funguo ipo low.

Pia gari zingine Zina sehemu maalumu ya kuweka ufunguo ukiwa ipo low battery weka ufunguo hapo washa
mkuu amini kabisa hatua zote hizo nilichukua, sema kuna shida tu somewhere bado hatujaigundua, maana wanasema ni kawaida eneo hilo sensor kugoma
 
mkuu amini kabisa hatua zote hizo nilichukua, sema kuna shida tu somewhere bado hatujaigundua, maana wanasema ni kawaida eneo hilo sensor kugoma
Kuna alama ya ufunguo kwenye dashboard? Au Kuna Alam yeyote? Vinginevyo piga picha msg unayopata kwenye gari tukupe solution
 
Kuna alama ya ufunguo kwenye dashboard? Au Kuna Alam yeyote? Vinginevyo piga picha msg unayopata kwenye gari tukupe solution

Yap alama ilikuja na ilikuja tu baada ya kufika eneo lile, hakukua na alarm yyte, na kama battery low mbona baada yakuondoka sikupata shida yakuwasha tena na funguo ilikua mfukoni kabisa?
 
Maeneo ambapo hizi gari (push to start/press button) zinasumbua sana kuwaka unapozima ni pale junction ya Tazara/ Bakhressa/ Dar Group Hospital/.. Nilikuwa pia napata sana shida, ila suluhisho ni kuweka hiyo sensor (funguo) palepale kwa start button unapo switch on gari yako..
kumbe sipo peke yangu niliyepata shida hyo, nashukuru sana mzee hapo umenitoa upofu, pamoja sana
 
Maeneo ambapo hizi gari (push to start/press button) zinasumbua sana kuwaka unapozima ni pale junction ya Tazara/ Bakhressa/ Dar Group Hospital/.. Nilikuwa pia napata sana shida, ila suluhisho ni kuweka hiyo sensor (funguo) palepale kwa start button unapo switch on gari yako..
Umempa jibu sahihi, Sensor unaiweka palepale kwenye button ya start na una push hiyo button uku ukiwa umekanyaga break na gari itawaka
 
Back
Top Bottom